Tupike mchuzi wa samaki wa nazi

Tupike mchuzi wa samaki wa nazi

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
20,274
Reaction score
49,245
I hope mko vizuri
Na mnaendelea na majukumu
Leo tupike samaki wa nazi(fish curry)
Mahitaji
Samaki waliokaangwa
Karoti,hoho,kitunguu maji 1,tangawizi,kitunguu swaumu punje chache,nyanya moja,mafuta ya kupikia,chumvi
Nazi mimi nimetumia halis unaweza tumia hata ya pakt pamoja na curry powder

Hatua ya kwanza
unaandaa viungo vyako kata hoho size unayopenda saga carrot,nyanya,tangwa pia kitunguu swaumu na tangawiz
IMG_20251023_191846.jpg

Hatua ya pili
Bandika sufuria jikoni weka mafuta kidogo sana yakipata moto weka kitunguu maji kaanga hadi kilainike weka kitunguu swaum na tangawiz usikaange sana kisha weka carrot nazo kaanga kidogo weka nyanya pamoja na curry powder

Mimi nimetumia nyanya moja sabbu sipend nyanya nyingi huwa natumia carrot nyingi funika acha viive
IMG_20251023_192524.jpg

Vikiiva weka hoho pamoja na tui la nazi la pili kama unatumia nazi ya asili acha vichemke kisha weka tui bubu(tui la kwanza) koroga kisha tumbukiza samaki wako koroga taratibu tui isikatike ikichemka acha kwa dakika 5 kisha ipuka kama unatumia nazi ya pakti baada ya nyanya kuiva utaweka maji kidogo kisha utaweka nazi ya pakti

Mbogayako itakuwa tayari
Unaweza kula na ugali wali na chochote unachopenda
Mimi nilichagua kula na ugali

IMG_20251023_194433.jpg
IMG_20251023_195551.jpg
 
Hongera sana ........ mambo nipendayo....hapo unakula ugali unashiba balaa, ukipata na glass ya mtindi bariid kama ni mchana unalala kabisa 😊 😃
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom