Unga hivi maharage kama hupendi/hutumii mafuta

Unga hivi maharage kama hupendi/hutumii mafuta

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,722
Reaction score
62,689
Hi guys hope mko poa,.
Tupike pamoja
1. Maharage yako ambayo yashachemshwa na chumvi utaweka maji kidogo na uweke jikoni yapate moto
IMG_3484.jpeg

2. Katakata kitunguu karoti na hoho uweke na uache vichemke kidogo
IMG_3486.jpeg

3. Ikichemka kiasi weka ngogwe/ nyanyachungu na nyanya kidogo
IMG_3487.jpeg

4. Koroga kidogo na ufunike uache vipikike kwa mda kidogo kama dakika nne au tano
IMG_3488.jpeg

5. Yakishachemka na nyanyachungu zikishalainika vizuri utapunguza moto halafu utaweka tui la nazi kikombe kimoja na utaacha yapikike yakiwa wazi huku unakoroga taratibu taratibu
IMG_3491.jpeg

6,. Kama kwa dakika mbili hivi au tatu maharage yako yatakua yameiva na yako tayari kuliwa,.
IMG_3493.jpeg

7. Utakula na chochote kile,. ( wali ugali chapati au chochote tu unachopendelea)
Sie tuliyala kwa wali,. And yalikua matam sana👌🤗
IMG_3495.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom