Tupike simple cake ya Unga Robo

Tupike simple cake ya Unga Robo

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,457
Reaction score
61,465
Hi guys hope mko poa,. Tupike pamoja keki hii simpe na tamu sana

1. Utaweka blueband 200g na sukari 150g kwenye bakuli utatumia mixer kuchapa
IMG_3558.jpeg

2. Utachapa mpaka ibadilike rangi iwe inaelekea kwenye weupe,. Then utanza kuweka mayai ( nimetumia mayai manne ),. Utaweka moja unachapa then unaweka jingine hivyo hivyo hadi umalize yote manne
IMG_3575.jpeg

3. Utaendelea kuchapa kwa mda kidogo then utaweka vanilla nusu kijiko cha chai,. Utaendelea kuchapa tena kama kwa sekunde 30
IMG_3577.jpeg

4. Utaweka unga wako wa ngano robo ambao imeuchuja vizuri usiwe na vibonge bonge( usiweke unga wote kwa mara moja, ugawe mara mbili ),. Utaweka na baking powder robo kijiko cha chai,. Then utakoroga taratibu kwa kutumia mchapio wa mkono
IMG_3578.jpeg

5. Utaweka maziwa kikombe komoja kidogo,. Mie niliweka maji kwasabu niliyekuwa nampikia hatumii maziwa,. Nayo ni kipimo kile kile kikombe kimoja kidogo,.. utaendelea kukoroga taratibu taratibu hadi mchanganyiko wako ulanike
IMG_3567.jpeg

6. Utaandaa baking tin yako utaipakaza blueband kidogo ndani na pembeni then itaweka baking paper na utamiminia mchanganyiko wako,. Utapiga piga chini kidogo ili kuondoa poles
IMG_3568.jpeg

7. Utaweka kwenye oven,. Utabake kwa moto wa 150 juu na chini kwa dakika 45,. Ila make sure ulishaiwasha oven dakika kumi kabla
IMG_3569.jpeg

8. Usifungue fungue oven dakika ishirini za mwanzo,. Then mda ukishamalizika utachukua toothpick uchome kama imeiva hadi ndani na yangu ikawa imeiva,. Nikaitoa ipoe kwanza kabla sijaanza kuipamba
IMG_3623.jpeg


Bad luck kabla sijafanya chochote simu yangu ikawa imezima na umeme ukakata,. so sikuweza kusnap nilivyokua napamba hatua kwa hatua ila nilimwambia mhusika ikimfikia anipigie picha anitumie simu ikiwaka nitaiona nipost,. And it was 10/10 alivyosema😂😂🙈
E922F79C-E56C-4160-9A84-4A1B4F1B3232.jpeg


Haya muwe na jioni njema,. Nawapenda🥰😘
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom