Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Sijaona formula mkuu.
Hii hapa
20260804_113626.jpg
 
Nani mwingine ana changamoto kwenye Ms Excel? Kazi za ofisi zisikufanye uwe unalala usiku wa manane, kama ni mambo ya mahesabu tuwasiliane hapo tufanye namna ili uwe unalala saa mbili punde tu baada ya kuangalia taarifa ya habari[emoji846]
 
Kwenye Invoice au Risiti. Kama unataka idisplay tarehe na muda wa kuiandika, enter the following formula. =now() . Hapa kila kitu utachofanya itajiupdate muda automatically.
Na ukitaka iweke taarifa za leo tu ni =TODAY() 👍
 
Unakosea kutype, usitumie curled bracket...tumia bracket za kawaida (curved) kama hii () na sio {}
Nimetumia bracket za kawaida hebu angalia vizuri kwenye hiyo attachment nimetype kama ilivyo, wewe umeitest hii formula.?
 
Nimetumia bracket za kawaida hebu angalia vizuri kwenye hiyo attachment nimetype kama ilivyo, wewe umeitest hii formula.?
Ndio, formula inafanya kazi bila shida. Attachment yako nikiizoom maandishi yanafifia, nashindwa kuiona vizuri ili nijue unapokosea
 
Sawa mkuu, lakini mbona amount imekuja ndogo sana, hiyo amount inatakiwe igaiwe kwa 4 ili taxpayer alipe kwa awamu nne, so kwa case hiyo hapo anatakiwa alipe 1500 kwa installment moja.
Asilimia 3 ya laki 2 ni 6,000/=
4.2M inadondokea kwenye range ya 4M to 7M, ambayo rate yake ni 3% ya kinachozidi kwenye 4M
 
Imekubali, kwanini tusingeanza na kubwa kwenda ndogo let say 100,000,000 badala ya 4,000,000
Vyovyote tu utakavyoweka, màana formula huwa inazunguka pote kutafuta sehemu ya kudondokea na kama kùna chaguo zaidi ya moja basi formula itadondokea katika chaguo la karibu zaidi na alama ya =. Kama itatokea formula imekosa pa kudondokea itaandika FALSE mfano ukiandika amount ambayo haijawa considered ktk utengenezaji wa formula eg 120,000,000/=
 
Imekubali, kwanini tusingeanza na kubwa kwenda ndogo let say 100,000,000 badala ya 4,000,000
Mfano ukiandika if(A1>21, "F", if(A1>41,"D")), ukiandika 50 ktk A1, out itaandika F na sio D kwa sababu statements zote zitatoa jibu la TRUE (50 ni kubwa kuliko 21 na pia ni kubwa kuliko 41)
 
Mfano ukiandika if(A1>21, "F", if(A1>41,"D")), ukiandika 50 ktk A1, out itaandika F na sio D kwa sababu statements zote zitatoa jibu la TRUE (50 ni kubwa kuliko 21 na pia ni kubwa kuliko 41)
Na pale juu mbona kuna greater than na equa na kuna sehemu zingine ni greater-than na AND hii tofauti yake nini kwa mfano kwenye formula ya PAYE zote ni greater-than na hamna AND na ime workout ?
 
Na pale juu mbona kuna greater than na equa na kuna sehemu zingine ni greater-than na AND hii tofauti yake nini kwa mfano kwenye formula ya PAYE zote ni greater-than na hamna AND na ime workout ?
Aisee! mbona hiyo ni shule tena, wewe shukuru Mungu kwanza case yàko imekuwa solved japo mtaalam hata soda hajapata
 
Back
Top Bottom