Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Imegoma mkuu, ambapo ukiingiza 10,000,000 kwenye ile template ya TRA inakuja 3,000,000 kama provisional tax, wakati kwa hii formula uliyodevelop inakuja 90,000 mimi kwa ile formula inakuja 3,850,000 kwahiyo tumekosea kaka.
Kwa kutumia hizi rate za kwenye table, income ya 10Milion, tax yake haiwezi ikawa 3Milion.

Tuma link ya hiyo calculator ya TRA nikutengenezee formula
 
Kwa kutumia hizi rate za kwenye table, income ya 10Milion, tax yake haiwezi ikawa 3Milion.

Tuma link ya hiyo calculator ya TRA nikutengenezee formula
Cheki huo mpangilio mkuu
 

Attachments

  • Screenshot_20250306_181345_Chrome.jpg
    Screenshot_20250306_181345_Chrome.jpg
    132.3 KB · Views: 21
Cheki huo mpangilio mkuu
Ukiweka income ya milion 10, hiyo online calculator ndio inaleta tax ya milion 3? Au ulikusudia kuandika 100,000,000?

Hata hivyo income ya 100M, tax yake ni 3,115,000/= sio 3M. Nipatie majibu ya calculator pindi income inapokuwa ni 6M, 9M na 15M ili nione majibu gani
 
Naomba kujulishwa jinsi ya kuandaa matokeo ya mtihani, jinsi ya kuwapanga wa mwanzo hadi mwisho kwa kuzingatia column ya JUMLA bila kuathiri mpangilio wa alama za masomo kwa kila somo.
Simple
 
Wadau,

Kujua Excel Spreadsheets ni muhimu sana...

Tunaweza tukashirikishana tricks mbalimbali katika Excel hapa ili tujifunze wote..

Unaweza pandishwa CHEO au Kupata kazi kirahisi Kwa kujua EXCEL vizuri.. Watanzania wengi udhaifu wao upo hapo.. So Unaifanya WEAKNESS hiyo kuwa Strength kwako.Kwenye Ofisi yeyote mtu ambaye haogopi excel huwa anaonekana ni kichwa sana.. unaweza pia ukamvutia bosi wako kama utaijua kumshinda yeye na atakufanya rafiki yako ili usimuumbue...

Kwenye Interview ndio utawamaliza kabisa ..ukikutana na viherehere wakakuchokoza hapo ndio unawaonesha ujuzi wako wote... wengi huwa hawaijui kwasababu ya uvivu... Kwa hiyo usiogope..Niliwahi ulizwa swali na panelist kwenye Interview nikaenda deep mpaka akaogopa maana kuna vitu alikuwa havijui na yeye akaamua apotezee hilo swali akarukia kitu kingine kukwepa aibu..

Weka Trick yako hapo chini ili wengine wafaidi au kama unaswali uliza nitakujibu mimi au wadau wengine...

Ingependeza sana pale unapokwama uulize swali hapa.. Ili tujadiliane vitu ambavyo ni useful katika mazingira yetu ya shule au kazini...

Dunia ya sasa sio lazima uende darasani.. Unaweza tumia muda wako na MB zako vizuri mtandaoni na ukaongeza Ujuzi polepole

**Kama unatafuta kazi na umeandika Kwenye CV kwamba una ujuzi na Excel fuatilia huu uzi na group uwe updated na vitu mbalimbali ili usije umbuka siku ukiwa unafanya written au Oral Interview

** Nitakuwa naelezea Common questions ambazo waajiri hupenda kuuliza kukupima uelewa wako katika Spreadsheets.. Ni Muda na MB zako tu.. Sihitaji kingine...

Please NOTE

** Usiulize kitu unachokijua kupima watu Bali andika trick unayoijua ili wengine wafaidi na kama unaswali ULIZA wataalam tutakusaidia

PS:
Kama upo Telegram unaweza Ingia Kwenye Public Channel ipo hapo chini Kwa vitu ambavyo haviwezekani kuelezewa hapa vizuri..Kama video na files. Ni public channel ya kusoma na Sio sehemu ya chatting!

Naomba kuwasilisha!

Ethos
Nimeweka kambi hapa
 
Back
Top Bottom