Tupe maujanja!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Kuna barua muhimu ya kijeshi inabidi ipelekwe mji B kutoka mji A.Kati ya mji A na mji B hakuna kituo cha mafuta.Gari iliyopo ikijazwa 'full tank',ina uwezo kusafiri nusu ya umbali kati ya A na B.Licha ya hii gari hii,kuna gari zingine tisa zenye uwezo sawa na gari hili.Hakuna kamba ya kuvutia gari,hakuna uwezekano wa gari kubebana wala kusukumana,hakuna vifaa vya ziada vya kubebea mafuta.Mji A na mji B kuna vituo vya mafuta vyenye mafuta ya kutosha.(SWALI)Kwa kutumia idadi yoyote ya magari kati ya yaliyopo(10),utafanyaje kuisafirisha barua hii muhimu kutoka A hadi B.(HINT):huruhusiwi kuitelekeza gari yoyote njiani kati ya mji A na mji B.
 
itaenda kiongeza mafuta kwenye kituo kilihopo kati ya mji A na mji B
 
Watatumia ndege zao za kijeshi kama walivyomsafirisha Freeman Aikael Mboye: Mji A Dar na B Arusha. Nshapatia eheeeeeeeeee!
 
teeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh! :caked:nawashauri watumie gari (semi-trail) linalojaza mafuta katika vituo ndani ya hiyo miji miwili!

Kuna barua muhimu ya kijeshi inabidi ipelekwe mji B kutoka mji A.Kati ya mji A na mji B hakuna kituo cha mafuta.Gari iliyopo ikijazwa 'full tank',ina uwezo kusafiri nusu ya umbali kati ya A na B.Licha ya hii gari hii,kuna gari zingine tisa zenye uwezo sawa na gari hili.Hakuna kamba ya kuvutia gari,hakuna uwezekano wa gari kubebana wala kusukumana,hakuna vifaa vya ziada vya kubebea mafuta.Mji A na mji B kuna vituo vya mafuta vyenye mafuta ya kutosha.(SWALI)Kwa kutumia idadi yoyote ya magari kati ya yaliyopo(10),utafanyaje kuisafirisha barua hii muhimu kutoka A hadi B.(HINT):huruhusiwi kuitelekeza gari yoyote njiani kati ya mji A na mji B.
 
Kwani kati ya mji A na B ni tambarare??! Tatumia free mingi kwenye mteremko na gia kubwa wakati wote... mepatia eeh?
 
Yaani tangu mchana nafikiria ila sijapata jibu, ngoja nichakachue....

Kwa kuwa kuna magari kumi na full tank ya gari moja itawawezesha kufika nusu ya safari, basi ningewashauri wafungue Tank moja la gari nyingine kisha waijaze mafuta na waibebe kama ziada kwenye gari itakayosafiri.. Kisha wajaze Tank ya hilo Gari, kwa mantiki hii watafika mwisho wa safari bila tatizo lolote..

......... Lol
 
Yaani tangu mchana nafikiria ila sijapata jibu, ngoja nichakachue.... Kwa kuwa kuna magari kumi na full tank ya gari moja itawawezesha kufika nusu ya safari, basi ningewashauri wafungue Tank moja la gari nyingine kisha waijaze mafuta na waibebe kama ziada kwenye gari itakayosafiri.. Kisha wajaze Tank ya hilo Gari, kwa mantiki hii watafika mwisho wa safari bila tatizo lolote.. ......... Lol
Tawire umepatia
 
Duuh! Ngumu kiasi. Nimejaribu maujanja haya, inawezekana isiwe sahihi lakini tutapata pa kuanzia:

Tuseme ikiwa masafa ni kilomita 10, magari yakifika kilomita 5 yataishiwa na mafuta. Kwa hivyo kituo cha kubadilishana barua kitakuwa kilomita ya 5. Kwa hivyo, zitahitajika gari 6: 3 katika kituo A na 3 katika kituo B. Gari tuziite X, Y na Z kutoka kila upande.
Zitaondoka zote 3 kutoka kila upande na zikifika kilomita ya 2 ½ , gari Y litaigawia gari Z nusu ya mafuta yaliyobakia ambalo litakuwa na mafuta ya kutosha kwenda na kurudi hadi pale kilomita ya 2 ½
Kumbuka kuwa gari Z na Y zitakuwa hazina tena mafuta. Itabidi gari X ifanye safari mara 2 kurudi kituo A kuchukua mafuta kwa ajili ya magari Z na Y ili yaweze kurudi kituo A.
Nyendo hizo hizo zitafanyika kwa magari 3 ya kituo B
 
Hii kali, lakini ngoja nijaribu.
Kuna gari 10 zenye full tank na zote zitaishia katikati ya safari kabla mafuta hayajaisha. Itakuwa hivi. Zitaondoka zote hadi robo ya safari. Gari tano zitatoa mafuta yake yaliyobaki kwa gari tano, hivyo gari hizo zitafika katikati ya safari zikiwa na mafuta ya ziada. Pale magari matatu yatafaulisha mafuta yaliyobaki kwenye magari mawili yaliyobaki ambayo yataenda hadi robotatu ya safari na gari moja litaachia mafuta yaliyobaki kwa gari moja litakalomaliza safari na kuwahisha barua hiyo muhimu
 
Hii kali, lakini ngoja nijaribu.Kuna gari 10 zenye full tank na zote zitaishia katikati ya safari kabla mafuta hayajaisha. Itakuwa hivi. Zitaondoka zote hadi robo ya safari. Gari tano zitatoa mafuta yake yaliyobaki kwa gari tano, hivyo gari hizo zitafika katikati ya safari zikiwa na mafuta ya ziada. Pale magari matatu yatafaulisha mafuta yaliyobaki kwenye magari mawili yaliyobaki ambayo yataenda hadi robotatu ya safari na gari moja litaachia mafuta yaliyobaki kwa gari moja litakalomaliza safari na kuwahisha barua hiyo muhimu
Upo sahihi lakini magari utayatelekeza njiani,nenda na hii solution katika swali la tupe maujanja part 2!
 
Back
Top Bottom