Tumezindua Sera mpya ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake, 2023

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
543
3,575
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 8 Machi, 2024 Dodoma, Chamwino ambako pia TUMEZINDUA SERA MPYA ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023 mbadala wa ile ya mwaka 2000.

Sera hii ya Mwaka 2023 imezingatia maeneo mapya kadhaa (tutaendelea kuelimisha) na kubwa ni imejumuisha masuala ya maendeleo ya wanaume siyo wanawake tu kwani, imetambua kuwa, maendeleo na ustawi imara na endelevu ni ule unaogusa Jinsia zote kike na kiume.🤝

Ahsante Sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule kwa ushirikiano wako.

Pongezi ziende kwa Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wizara mpya na Sera mpya.

Ahsanteni Wadau wote na wananchi wote kwa ushirikiano wenu kwenye kutoa maoni kwa ajili ya kuandaa sera ya 2023, ahsante kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkitoa ushirikiano wa maoni, mawazo na kutenda pamoja na Wizara yenu ya Jamii

Tuendelee kushirikiana tunapoelekea kuboresha sheria, mipango na mikakati ya kisekta ngazi zote, Ili iakisi sera hii mpya.

Shukrani

IMG-20240308-WA0117.jpg
IMG-20240308-WA0076.jpg
IMG-20240308-WA0062.jpg
IMG-20240308-WA0072.jpg
 
Mngesaidia kutuwekea hapa walau tuipakue hiyo sera na kuipitia.

Otherwise, Pongezi Kwa kuadhimisha Siku yenu Wanawake.
 
serikali kuweni makini sana sana na sera zinazo mbeba mwanamke!
ustawi na maendeleo ya ujumla kwa taifa mchango wa mwanamke hata iwe namna gani hautazidi robo.

ipo siku tutatafuta palipotuangusha baada ya kuteleza.
 
Uzuri hii imembeba na mwanaume kikamilifu. Ni moja ya maeneo yaliyotambuliwa na kuzingatiwa. Tuwekeni tu sasa mipango na mikakati ya kisekta isome shughuli husika sambamba na sheria zake kisekta. Ahsante kwa hoja yako....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ni lini tutakua na sera ya jinsia na maendeleo ya wanaume ?

Mana vijana wakiume maisha yakiwa magumu hata kua na familia wanaogopa, mwisho wa siku wanatia mimba na kukimbia.

Muwakumbuke wanaume nao
Tayari eneo hilo la wanaume limetambuliwa kwenye hii sera. Mje sasa tushirikiane kwa maoni kuweka mipango, mikakati, sheria na kila utekelezaji wa kisekta tukumbuke kuwa, tunajielekeza siyo kwenye mashindano ya ME na KE Bali wote waendelee na kustawi. Kwa sasa ME Yuko mbali kimaendeleo na kiustawi kamwacha KE hukoooo

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
serikali kuweni makini sana sana na sera zinazo mbeba mwanamke!
ustawi na maendeleo ya ujumla kwa taifa mchango wa mwanamke hata iwe namna gani hautazidi robo.

ipo siku tutatafuta palipotuangusha baada ya kuteleza.
Nchi zilizo endelea walianza hivi hivi kuwaweka wanawake juu kabisa ..
Halafu kilichofata ni "watu wa jinsia moja" kuja juu ya wanawake...
Wanawake walitumika kama "chambo" now mpaka Kanisa Katoliki liko mbele kabisa ....kuwapa Haki zaidi watu wa jinsia moja ...halafu ndo wanafata wanawake...
Wanaume wanakandamizwa...ukioa ukiacha nusu ya Mali zako zinaenda..
Kumtongoza mwanamke Tu unaweza shitakiwa Kwa sexual harassment...
 
Naona ulimwengu wa sasa mwanamke,mwanamke anapambana kweri kweri awe sawa na mwanaume,mpaka kwenye kutoa maamuzi ndani ya nyumba

Ova
 
Naona ulimwengu wa sasa mwanamke,mwanamke anapambana kweri kweri awe sawa na mwanaume,mpaka kwenye kutoa maamuzi ndani ya nyumba

Ova
Mapambano haya hayaelekei huko ulikosema, ila utaelewa tu kadri tunavyoelimisha na kutoa taarifa. Tusichanganye mwelekeo wa mtu binafsi na tabia zake na mwelekeo wa kitaasisi. Tushirikiane jamani. Ila ahsante kwa kuuliza, ndiyo mwanzo wa kuelewana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Tuendelee tu kumeza haya mambo kama yalivyoanzishwa na wazungu pale Beijing na kuyashadadia huku Africa.

Mwanaume ni mwanaume tangu Mungu alivyoumba ulimwengu, na mwanamke ni mwanamke toka ulimwengu ulivyoumbwa.
Kuvimba shingo na hizi 50/50 kutakuja kutuletea shida sana duniani hasa pale dunia itakapoamua kwa dhati sasa iwe 50/50 sidhani kama itafika 5yr kabla Mwanamke hajasurrender.

Mwanaume ndio mhimili wa dunia, akianguka Mwanaume na dunia ndio imeishia hapo, Akinaa mama wanapokimbia nafasi yao waliyoumbiwa ni kusaliti uumbaji na matokeo yake ni mabaya Sana.
 
Nchi zilizo endelea walianza hivi hivi kuwaweka wanawake juu kabisa ..
Halafu kilichofata ni "watu wa jinsia moja" kuja juu ya wanawake...
Wanawake walitumika kama "chambo" now mpaka Kanisa Katoliki liko mbele kabisa ....kuwapa Haki zaidi watu wa jinsia moja ...halafu ndo wanafata wanawake...
Wanaume wanakandamizwa...ukioa ukiacha nusu ya Mali zako zinaenda..
Kumtongoza mwanamke Tu unaweza shitakiwa Kwa sexual harassment...
Salaam ndugu. Kuna wakati huwa naona Bora nikumbushe kuwa, madhambi hayo uliyosema yalianza enzi za sodoma na gomora maelfu ya miaka hata hizo sera nadhani hazikuwepo. Tanzania hatujaja na sera ya maendeleo ya Jinsia Ili kuelekea huko, mtaona kwenye taarifa zetu za utekelezaji na mijadala yetu ambayo tutafanya pamoja. Tuendelee kufuatilia.

Ahsante kwa hoja maana hoja ndiyo mwanzo wa kuelewana ndugu zangu.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
50/50 isiishie kwenye mambo marahisi tu iwepo mpaka kwenye yale magumu magumu

Ipo kazi moja mahala jamaa waliamua kuajili wamama kama sehemu ya 50/50 na Ile Sera ya wanawake tunaweza, kilichotokea baada ya mwezi pale mahala wakuu wavitengo walianza kugoma kabisa kuajili wamama, viuno na migongo viligoma, wengine walikuwa wanaingia kwenye siku zao bila tarehe kufika tena mara kwa mara, lakini kazi hiyo ilifanywa na wanaume miaka yoote bila hizo shida.

Mama yangu Mh Waziri, nguvu kubwa sana ilipaswa kuelekezwa kwa mwanaume maana ndiye aliyeumbwa kuwa kichwa.
 
Nchi zilizo endelea walianza hivi hivi kuwaweka wanawake juu kabisa ..
Halafu kilichofata ni "watu wa jinsia moja" kuja juu ya wanawake...
Wanawake walitumika kama "chambo" now mpaka Kanisa Katoliki liko mbele kabisa ....kuwapa Haki zaidi watu wa jinsia moja ...halafu ndo wanafata wanawake...
Wanaume wanakandamizwa...ukioa ukiacha nusu ya Mali zako zinaenda..
Kumtongoza mwanamke Tu unaweza shitakiwa Kwa sexual harassment...
bado mimi binasfi na wengi wetu tunakuwa wa mwisho kuamini akili ya mwanamke katika uongozi, hivi jana tu moja wapo wa viongozi mwanamke amepiga marufuku kwa mwanamke kumpigia kura mwanaume, aina hii ya akili sio afya kwa taifa, kauli kama hii imetoka kwa mwanamke msomi tena shule zinazo tambulika kuwa bora, hii shida sio shule ama kiwango cha elimu bali ni ile selfish aliyo nayo mwanamke .
 
Haya mambo ya jinsia na usawa naona kabisa tumeparamia mtumbwi wa wamagharibi bila kuelewa jahazi linaelekea wapi.

Itafikia kipindi a male child will need social support to survive. Hii sio sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom