Watumishi Wanawake wa Wizara ya Fedha walivyoadhimisha siku ya Wanawakekatikati ya viwanja vya Chinangali II jijini Dodoma

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
PIX 1 (1).jpg
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo (mbele) akiwaongoza baadhi ya watumishi wanawake wa wizara ya Fedha kwa niaba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, waliojitokeza katika maandamano kusherehekea kilele cha Siku ya Wanawake yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma.
PIX 2 (1).jpg
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, akiwapungia mkono waandamanaji (hawapo pichani) wakati wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kujitambulisha.
PIX 3 (1).jpg
PIX 3b.jpg
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo, (kushoto) akiwa katika maandamano kuelea kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma ambapo kilele cha maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani yamefanyika Kitaifa.

PIX 4 (1).jpg
Baadhi ya Watumishi Wanawake wa Wizara ya Fedha wakishangilia katikati ya viwanja vya Chinangali II jijini Dodoma eneo ambalo maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanafanyika Kitaifa, mara baada ya kuwasili katika eneo hilo na bango la Wizara ya Fedha.

PIX 5 (1).jpg
Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Chinangali II wilayani Chamwino mkoani Dodoma

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
 
Hongereni kuadhimisha Siku ya Wanawake.

We Men do real love you

Bila ninyi mnadhani Wanaume tungezaa na nani watoto wetu.
 
Back
Top Bottom