Tupate uthibitisho wa tuhuma zinazomkabili ASP Jumanne shahidi Na. 8 wa Jamhuri kesi ya Mbowe

Mimi ninaamini hii kesi itakapoisha all the accused will be acquitted. Ninaamini Mbowe na wenziwe wataachiwa tu.
Lakini ninaamini hii kesi will backfire kwa hawa watu. Hizi tuhuma zao zinafika kwenye masikio ya wenye mamlaka.
Hawa watu ninauhakika watakamatwa na baada ya hapo tutasikia mengi yenye kutia aibu yakiibuliwa.
Let's wait and see
Tunaweza kuamini hivyo lakini si kwa nchi ambayo imegubikwa na vyeo vya kihisani. Tujiulize ni kwanini hadi sasa Jumanne hajafunguliwa mashtaka kesi ya kumbambikia mstaafu meno ya tembo? Tujiulize kwanini jaji anatumia nguvu kubwa kuwahami jamhuri pale walipoyapuyanga? Tujiulize kwanini wako watu wanashangilia na kufurahi Mbowe na wenzake kuwa ndani muda wote huo???
Haki haiombwi
 
Kwetu haya hayawezekani Mkuu kama kuna picha zilitembea polisi wakishiriki kuiba kura unatarajia kuona wakitenda haki ama kuundiwa chombo cha kuwachunguza??? Pata picha ya gaidi Hamza na uchunguzi ulivyokamilika fasta na watu kupewa vyeti kisha rudi katika kesi ya tuhuma za ugaidi ya Mbowe utaona tulipo na wapi tunapelekwa.
Ni kweli wanafunika ukweli hii haikubaliki sehemu yeyote eti Jambazi anaenda kutoa ushahidi kisa ni polisi...
 
Tunaweza kuamini hivyo lakini si kwa nchi ambayo imegubikwa na vyeo vya kihisani. Tujiulize ni kwanini hadi sasa Jumanne hajafunguliwa mashtaka kesi ya kumbambikia mstaafu meno ya tembo? Tujiulize kwanini jaji anatumia nguvu kubwa kuwahami jamhuri pale walipoyapuyanga? Tujiulize kwanini wako watu wanashangilia na kufurahi Mbowe na wenzake kuwa ndani muda wote huo???
Haki haiombwi
Upo sahihi Mkuu
 
Ukiangalia aina ya mashahidi wa jamhuri kwenye hii kesi na historia zao inatosha kabisa kumuonesha mtu mwenye akili timamu ni lipi lengo la serikali kwenye hii kesi ya Mbowe, wamechagua askari wahuni wasioheshimu majukumu ya kazi zao wawe mashahidi wao ili waseme uongo bila hofu yoyote kwa Mungu kwasababu ndio tabia yao.
Wamewatafuta mashetani katika maumbo ya wanadamu wawe mashahidi, na pia wawe watoa hukumu.

Mpaka sasa, tangu kesi ianze, mashahidi na majaji, wote ni lile kundi moja.
 
Back
Top Bottom