Tuongee asubuhi na Albert Msando! Mada: Hama hama ndani ya vyama vya Siasa. Je, ni kukua kwa demokrasia au ni rushwa?

Hakuna nchi hata moja humu ulimwenguni ambayo imaekamilisha jambo hata moja. Ndio maana mapambano ya maendeleo hayaishi (kwa serikalini na watu) kwa sababu hayana mwisho! Aidha, si kweli kwamba hakuna mazingira mazuri ya kujiendeleza. Naamini kwamba yapo ya kutosha na ndio maana katika nchi hii kuna watu ambao bidii na maarifa yao vimewatoa baada ya kubaini fursa lukuki zilizopo.
Naomba uvute subira, kama matamanio yako ni kuiona Tanzania iking'ara kimaendeleo, kwani muda si mrefu utaona Taifa jipya na CCM mpya isiyokuwa na akina Lowasa, Sumaye, Mtei, Nyalandu, Kingunge, Mgeja, Mahanga, nk nk!
Huu ndo udhaifu uliotufikisha hapa,badala ya kujadili tunajadili watu...!!!shame!!!
Wazee wa vijisenti,hela ya mboga,wenye kashfa lukuki za escrow,meremeta,uuzaji wa nyumba za serikal huwaoni
 
Serikali sikivu? Bro, Maputo Declaration ni ya mwaka 2003! For 14 years, serikali za CCM hazijawahi hata kutenga asilimia 5 ya bajeti yake kwenye kilimo.

Are you a robot? Nimekwambia, this time serikali imetenga bilioni 24 kwenye kilimo, huku ikitenga bilioni 500 kununua ndege! Halafu unasema serikali sikivu!!



Nimekupa mifano ya Tiger economies. Hizi si nchi za Ulaya. Nimekwambia Tanzania ilikuwa na kiwango kwenye miaka ya 1960. Hapa naongelea nchi kama South Korea, Taiwan, Singapore na Hong Kong. Leo nchi hizi zinatoa misaada kwa Tanzania. Nchi hizi hazikutoa visingizio kama unavyotoa. South Korea leo ni leading hub ya manufacturing na innovation ya electronic equipment.




Sasa kwani IMF na WB ziliilazimisha Tanzania kufuata sera zao? Zile Four Asian tigers wala hazikufuata sera za IMF/WB. Ni sawa na mnavyolialia ‘kuibiwa’ kwenye madini as if wawekezaji waliwashikia bunduki wakati wa kusaini mikataba!! Kufuata sera za IMF/WB ni kutokana na serikali za CCM, haswa post-Nyerere kutokuwa bunifu, na kujawa na vitendo vya rushwa na ufisadi, kulikopelekea kile alichokianzisha Nyerere kupotea. Nyerere was visionary kwa import substitution policy! Kungekuwepo na usimamizi wa kutosha, leo hii Tanzania ingekuwa miongoni mwa ‘lion economies’.




Hakuna Tanzania mpya kama bado kilimo hakipewi kipaumbele chifu. Stop this silly talk! Tanzania gani mpya kwa serikali kutenga bilioni 24 kwenye kilimo (15B zikiwa ni misaada na 9B ni fedha za ndani), huku ikitenga 500B kununua ndege kwenye taifa ambalo takribani asilimia 70 ya wananchi wake ni peasants wanaotegemea subsistence agriculture?

It would have made a difference kama kungekuwa na trickle down economies. Lakini serikali iliyojawa na rushwa, inazuia hilo kutokea. Kuwa na Rais ambaye anajichotea tu mapesa Hazina bila ya idhini ya Bunge, nako hakusaidii! Ama kweli ni Tanzania mpya! Maana we have never had such a practice: kwa Rais kujichotea tu mapesa Hazina bila ya Bunge kupanga!!



Rais Magufuli alishasema yeye hashauriki! Maana hakuna aliyempangia kugombea urais. Alichukua mwenye fomu! Sasa unataka tutoe ushauri upi?

Btw, hakuna jipya katika ninayozungumza. Kama suala la kukipa kilimo kipaumbele ni jambo ambalo lipo at least kutokea mwaka 2003. Serikali ilikuja na CAADP, ASDP, DADPs, Kilimo Kwanza, Big Result Now n.k. Leo yote hayo yamewekwa kando ili tununue ndege kwa bilioni 500 na kujenga uwanja ndege kwa bilioni 39 kwenye eneo ambalo halina trickle down effect kwenye uchumi!!
Je, tulie na kujigaragaza chini huku tukijitiririshia kamasi? Je, tunune? Je, ulitaka Precision Air (ambayo tetesi zinasema inatokana na kuungua kwa Benki Kuu wakati wa Mtei) itamalaki na Air Tanzania ijifie kifo cha mende? Je, unajua vyema geographical and economical position ya huko unakosema uwanja wa ndege umejengwa bila kuwepo na multiplier effect?
Narudia kukuuliza, je, kama Tanzania ilikuwa inafuata ushauri wa IMF na WB ambazo unakiri kwamba huwa haziwi catalyst kwenye maendeleo, ulitarajiaje mabadiliko / maendeleo?
Kwa kifupi, narudia kwa msisitizo kwamba ni mpaka pale wewe, mimi na wale tutakapojitambua, ndipo nchi hii itasimama. Na naamini muda si nrefu wenye kukejeli na kukebehi kinachofanyika kwa sasa, watatahayari! Take it from me, rafiki!
 
Je, tulie na kujigaragaza chini huku tukijitiririshia kamasi? Je, tunune? Je, ulitaka Precision Air (ambayo tetesi zinasema inatokana na kuungua kwa Benki Kuu wakati wa Mtei) itamalaki na Air Tanzania ijifie kifo cha mende?

Kwahiyo Precision Air kuhusishwa na Mtei na kuzuia Air Tanzania isijifie ndiyo justifications za nchi yenye asilimia 70 ya peasants kutumia 500B kununua ndege?

Hakika, ulichokiandika proves my points!!

Je, unajua vyema geographical and economical position ya huko unakosema uwanja wa ndege umejengwa bila kuwepo na multiplier effect?

Sijui! Ebu ni-enlighten ndugu. Pengine kuna economic justifications za kutumia 39B kujenga International Airport kijijini Chato.

Ukishanieleza, halafu nieleweshe inakuaje fedha za ujenzi hazikupitishwa na Bunge. Yaani Magufuli alijichotea tu hizo fedha Hazina. Ni kwa namna gani zitakuwa accounted? Ni kwa namna gani zitakuwa monitored kuzuia kuliwa na Magufuli na kampuni inayojengwa ambayo Magufuli ana conflict of interest nayo?

Narudia kukuuliza, je, kama Tanzania ilikuwa inafuata ushauri wa IMF na WB ambazo unakiri kwamba huwa haziwi catalyst kwenye maendeleo, ulitarajiaje mabadiliko / maendeleo?

Nilikuuliza wewe ni robot? Maana majibu yako ni kama vile upo programmed!

Mbona nimefafanua mara mbili juu ya hiki unachokiuliza!! Nilikwambia kwamba, was Tanzania held at gun point kukubali sera za IMF/WB? Nikakupa mifano ya nchi ambazo ziligomea sera hizo, na sasa zimeendelea kiasi cha kuipa Tanzania misaada wakati zilikuwa maskini kama Tanzania miaka ya 1960 tu!!

Miaka 30+ ya sera za WB/IMF, tafiti zimeonyesha jinsi sera hizo zilivyoshindwa, lakini serikali ya CCM bado inazikumbatia. Pale BoT kuna Washington economists walio washauri wa sera za kifedha na kiuchumi!! Unfortunately, Magufuli is gutless katika kuwafukuza hao washauri na clueless juu ya nini cha kufanya.

Kwa kifupi, narudia kwa msisitizo kwamba ni mpaka pale wewe, mimi na wale tutakapojitambua, ndipo nchi hii itasimama.

Mimi najitambua sana, namshukuru Mungu kwa hili. Na ndiyo maana nakwambia chini ya CCM, taifa hili halitoendelea kamwe. Sababu kubwa ni serikali za CCM, post-Nyerere kuitupa sekta ya kilimo. Na pia CCM na rushwa/upiga deals/ufisadi kuwa sawa na samaki na maji.

Na naamini muda si nrefu wenye kukejeli na kukebehi kinachofanyika kwa sasa, watatahayari! Take it from me, rafiki!

Maendeleo siyo imani ndugu! Kama wewe ni mmoja wa watu vigogo huko serikalini na ndivyo unafikiri hivyo, hakika si ajabu nchi hii bado ni maskini.

Maendeleo ni vitendo vinavyowezeshwa kwa sera na mipango na utekelezaji wake, unaozingatia uzingatiaji wa sheria, nidhamu ya fedha, uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa umma kwa wananchi.
 
Yaaani hili jamaa hewa kabisa alafu kuna watu wanamtegemea kwny kesi zao, duuuh hatar sn
 
Niombe niseme machache wana body.
Nikweli siasa ni biashara ya ushindani sikatai mara nyingi ni mahesabu mkiyapiga vizuri mnatoboa na mkiyapiga vibaya mnakalishwa!.
Nianze na hili la Kasi ya Madiwani na Wabunge wa Chadema wanaojivua uongozi kwa madai kuwa wanaunga Juhudi za Rais wetu John P Magufuli,sipingi kwa hilo!
Ninacho kiona hapa timing iliyotumika haikuwa muafaka!.
Naweza kusema wanaujengea upinzani nguzo imara! Kwanza kipindi hiki ni kigumu kwa kila mwananchi!2020 watanzania wanajua pumba na mchele kosa nikuona viongozi wa chama tawala wakijinadi kuwa watawang'oa hatawale viongozi wakuu hapo sasa ndo inatia shaka kuwa wananua madiwani!Watu wanauone huruma sasa hivi upinzani kwa sababu mbili kuu moja kutokuwa na jukwaa sawa na wapinzani wao pili kuonewa mchana kweupe hii wananchi wanaumia na hili la madiwani ndiyo kabisa 2020 msishangae pia hawa madiwani ni malofa kwani kule hawatapata tena nafasi hiyo kwani Mwenyekiti alishawapa neno Ng'ombe aliyekatika mkia akirudi kundini wenzake umshangaa Itimisho.
 
wadau, siku za karibuni kumekuwa na taarifa nyingi na ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari kuhusiana na wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.
kwa bahati mbaya taarifa hizo zimekuwa zikipata publicity kubwa sana kwenye media zetu. tumesahau kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili watanzania ambazo zinahitajika zipate highlights kubwa kuliko kitendo cha mtu kutoka kwenye siasa za upande mmoja kwenda mwingine.
pia nilitarajia kuwa ccm kama chama tawala na kikongwe kisingejiingiza kwenye mkumbo wa kushadidia sana suala hill kiasi cha kutumia rasilimali na muda wake mwingine kusherehekea mwanasiasa anapotoka upinzani kujiunga nacho.imekuwa kama ni sera ya nyuma ya pazia ya chama.
after all bwana Polepole leo amejinasibu kuwa ccm imepata wanachama kiasi milioni 2 tangu awamu hii ya tano. kama ndivyo, ya nini mbwembwe zote za Leo na kufanya press coverage kubwa kwa ajili ya mwanasiasa mmoja tu hadi kuhusisha uongozi wa juu wa chama?
in kweli hicho ndicho kinachowahangaisha watanzania kwa sasa? ndicho kitakachomletea mtanzania mnyonge ufumbuzi wa changamoto zinazomkabili?
kama tumeambiwa siasa hadi 2020, hiki tunachoshuhudia ni
nini?
ccm kinatakiwa kijitambue wajibu wake kama chama tawala. hakitakiwi kuwa na poor politics za kunyang'anyana wanasiasa.
 
Kumekuwepo na hamahama ya wanachama wa vyama vya upinzani kuhamia chama tawala kwa hoja kuwa wanaunga mkono jitihada za Rais namna anavyoongoza nchi.Je ipo sababu ya kuwa na vyama vya upinzani ikiwa wapinzani wenyewe wanaunga mkono jitihada za chama tawala?
 
Kumekuwepo na hamahama ya wanachama wa vyama vya upinzani kuhamia chama tawala kwa hoja kuwa wanaunga mkono jitihada za Rais namna anavyoongoza nchi.Je ipo sababu ya kuwa na vyama vya upinzani ikiwa wapinzani wenyewe wanaunga mkono jitihada za chama tawala?
Wewe unaonaje?
 
Tuseme wewe hujui kuwa mtu hupewa neno la kusema ka unataka kuonekana mtiifu?? Swali ni Je! Wanayapata wanayoyatamani?
 
Hapo ni pesa wala hakuna la maana
Ni kweli ni pesa hakuna mtu wa kujitupia kwenye siasa kwa ajili ya wengine kabla ya yeye kushiba ukiona kakimbia huku kaenda kule lengo ni kujiongezea shibe siasa ni maslahi binafsi kwanza
Siasa ni mchezo wa karata 3 wizi mtupu wa kuhadaa watu
 
Ni kweli ni pesa hakuna mtu wa kujitupia kwenye siasa kwa ajili ya wengine kabla ya yeye kushiba ukiona kakimbia huku kaenda kule lengo ni kujiongezea shibe siasa ni maslahi binafsi kwanza
Siasa ni mchezo wa karata 3 wizi mtupu wa kuhadaa watu
Kula tano mkuu
 
Kufuatia wimbi la madiwani na baadhi ya waliokuwa wagombea ubunge wa cdm kuhamia ccm,hayo ni mapito tu na misukosuko ya kisiasa hivyo kwa mwana Cdm wa kweli tuendelee kushikamana ili kukijenga chama chetu na hao wanao zoa makapi waacheni wazoe makapi yao na waendelee kuwahadaa watanzania kuwa wanapendwa
 
Kufuatia wimbi la madiwani na baadhi ya waliokuwa wagombea ubunge wa cdm kuhamia ccm,hayo ni mapito tu na misukosuko ya kisiasa hivyo kwa mwana Cdm wa kweli tuendelee kushikamana ili kukijenga chama chetu na hao wanao zoa makapi waacheni wazoe makapi yao na waendelee kuwahadaa watanzania kuwa wanapendwa
Kwa huu uharibifu wa kodi zetu wanaoufanya sasa hivi nalipa kodi ambazo hazikwepeki tu za PAYE na za gari, lakini za Spea za gari na zingine zote hawatapata hata senti kumi
 
Kiukweli no kutaka kuwahadaa watanzania na matumizi mabaya ya madaraka katika nchi maskini unashindwa kulipa Madeni ya walimu na wazabuni Wa ndani ili uchumi wao ukue kutwa kununua madiwani na wabunge kutumia pesa kijinga
 
Back
Top Bottom