Tuongee asubuhi na Albert Msando! Mada: Hama hama ndani ya vyama vya Siasa. Je, ni kukua kwa demokrasia au ni rushwa?

Sasa akisema Amerika haina shule nzuri wewe unawaza nini, kwamba wana shule kama zile za kata.

Anazungumzia level ya marekani sio ya Tanzania.

Tanzania hii ambayo hapa nilipo hakuna umeme, umekatika; nawaona akina mama na watoto mgongoni wana ndoo kichwani wanaenda kwenye madimbwi kuchota maji wanayoshare na ng'ombe na mbuzi, leo kusiwe na upinzani! Kidding?
kuwepo kwa upinzani si matakwa yetu ingawa inatusaidia kupata misaada ya wakubwa
 
Zinapambana na masuala mengine kama vile ugunduzi zaidi katika sayansi, teknolojia, astronomia n.k., lakini siyo kwenye huduma za msingi kama maji, umeme, elimu, afya n.k. Sisi miaka 56 ya Uhuru, lakini hadi leo electricity access hata asilimia 40 haijafika! Maji hadi kesho DSM kuna watu hawana access. Hospitalini bado watu wanalala kwa kulundikana kwenye kitanda kimoja. Shuleni bado watu wanakaa chini ya miti, huku shule ikiwa na mwalimu mmoja anayefundisha masomo yote!

Nchi yetu haihitaji kutumia miaka mingi kuendelea na kuwa na huduma bora za jamii kama OECD countries zilivyofanya. Kwani wakati zinaanza kuendelea enabling environment haikuwa bora na rahisi kama ilivyo sasa. Hivi unajua wazungu walikufa sana kwa magonjwa kama mafua tu? Leo, tumerahisishiwa mazingira ya kuendelea kuanzia kwenye kiwango cha elimu na uelewa, ICT, kinga dhidi ya magonjwa n.k.

Singapore, South Korea, China, Taiwan, Malaysia na Hong Kong zilikuwa maskini kama Tanzania. Tena South Korea hadi miaka ya 1980 tu pale. Leo nchi hizi zinaipa misaada Tanzania!

Miaka 56 ya nchi huru, kwa maliasili na potentials zilizopo Tanzania, hatukupaswa kuwa maskini kama tulivyo leo. Lakini thanks to CCM and its crooks, we are doomed and fckdup!
Unapolinganisha miaka ya mkoloni hapa Tanzania (zaidi ya 75) na CCM (miaka 56) huoni tofauti?
Je sisi wananchi tunajiuliza ni nini tunachoweza kuifanyia Tanzania au tunajiuliza ni nini serikali imetufanyia?
Je, sisi wananchi tunatumiaje mazingira mazuri yaliyopo Tanzania kusukuma maendeleo mbele au tumekaa kuvizia dili? Tunaendanaje na sera za uzazi wa mpango ili kuleta uwiano kati ya huduma za jamii kutoka serikalini na idadi ya watu? Je, vyama vya siasa vinatumiaje uwepo wao kusimamia kile vinachokiamini (kuwa na watu makini na wasiokuwa na tuhuma) au wanabaki kujadili watu badala ya maendeleo na kuwa na watu walewale wenye tuhuma katika mzunguko wa uhamahamaji?
Naheshimu sana ulichokisema lakini ni vyema bado tukaona, kwa jicho la tatu, hatua tulizopiga za maendeleo. Najua wengi wangependa nchi yetu iwe kama Ulaya kwa hiyo miaka 56 baada ya uhuru! Lakini tukubaliane kwamba maendeleo ni safari ndefu na ngumu na yenye kuhitaji mshikamano. Changamoto zinazojitokeza katika kutukawiza kufika huko tunakotamani, nazo ni fursa! Tupambane nazo ili kuwa na Taifa lenye nguvu!
Tujitafakari!
 
Namsikiliza, kiukweli huyu jamaa yuko vizuri, anazungumzia udhaifu mkubwa wa vyama vya upinzani nchini, ni kuitumia CCM kama role model ya chama tawala, hivyo concentration ya upinzani ni kutumia udhaifu wa CCM. This is very valid argument.

Niliwahi kusisitiza humu kuwa
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike
CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!

Paskali
Bro uko sawa. Kitambo sana nadhani tokea uko kipindi chako cha kitimoto kama sijakosea nakufatiliaga tu. Uko vizuri Sana. Ila kuhusu Masha naomba nikukumbushe kuwa hata baba yake siasa za tamaa na ubinafsi ndio zilimfanya aonekane kituko. Masha anataka akute chakula anawe na Kula tu. Hataki kwenda shamba hata siku moja. Na nakwambia amshukuru sana kikwete.... Masha very genius, bright but he looks like Hyena at the middle of the forest. Very stupid boy. Namfananisha na kijana anayeongoza mitihani darasani Ila mitihani ya kitaifa anafail.
 
Mkuu Dabaga, asante na naheshimu mawazo yako.

P.
 
Unapolinganisha miaka ya mkoloni hapa Tanzania (zaidi ya 75) na CCM (miaka 56) huoni tofauti?

Wapi nimefanya ulinganishi huo? Ninachokisema ni kwamba iweje miaka 56 ya Uhuru nchi ishindwe hata kuwa imekamilisha hata jambo moja kwa asilimia 100?

Je sisi wananchi tuna jiulize ni nini tunachoweza kuifanyia Tanzania au tunajiuliza ni nini serikali imetufanyia?

Wananchi jukumu letu kubwa ni kuchangia mfuko wa serikali kupitia kodi na uwajibikaji. Haya yote serikali ina jukumu la kuweka mazingira ya watu kulipa kodi na kuwajibika.

Serikali inapoomba kura, uomba kupewa nafasi ya kutumia kodi zetu ili kuweka mazingira ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupata maendeleo.

Sasa sijui unataka wananchi tufanye zaidi ya haya?

Je, sisi wananchi tunatumiaje mazingira mazuri yaliyopo Tanzania kusukuma maendeleo mbele au tumekaa kuvizia dili?

Kama nilivyosema hapo juu, serikali inapaswa kuweka mazingira ya uwajibikaji. Ukiona wapiga dili wanasumbua, hiyo ni dalili ya serikali dhaifu. Morals lazima zijengwe kwa uwepo na enforcement ya sheria. Sheria tunazo, lazima serikali kupitia viongozi wake ndiyo wavunjaji wakubwa!

Uwa napenda kutumia mfano wa sekta ya kilimo. Sekta hiii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya watanzania. Lakini serikali imeitupa sekta hii; serikali imeshindwa kutenga asilimia 10 ya bajeti kwenye sekta kama ilivyokubaliwa kupitia Azimio la Maputo la mwaka 2003.

Kwa ujumla, Tanzania hakuna mazingira mazuri kwa watu maskini kuendelea. Wataendeleaje kama serikali haiweki nguvu kubwa kwenye kundi lililo kubwa zaidi?

Tunaendanaje na sera za uzazi wa mpango ili kuleta uwiano kati ya huduma za jamii kutoka serikalini na idadi ya watu?

Kwa hiyo unataka kusingizia ongezeko la watu kuwa ndiyo sababu ya Tanzania kuwa maskini? Sasa projections zinazofanywa na population censuses uwa ni za kazi gani? Na China au India watasemaje sasa? China wapo 1/3 ya word population, lakini wanazidi kusonga mbele tu! Wanatumia idadi yao kubwa kujiendeleza zaidi. Sisi tupo milioni 50 tu, kwenye nchi yenye ukubwa wa ardhi wa 945,087 Km², halafu unaongelea uwiano wa watu na huduma za jamii!

Je, vyama vya siasa vinatumiaje uwepo wao kusimamia kile vinachokiamini (kuwa na watu makini na wasiokuwa na tuhuma) au wanabaki kujadili watu badala ya maendeleo na kuwa na watu walewale wenye tuhuma katika mzunguko wa uhamahamaji?

Unaongelea vyama vya upinzani? CCM hawajawahi kusikiliza vile vyama vya upinzani vinavyoshauri. Madhara yake tumeyaona kwenye sekta ya madini, ufisadi uliokithiri serikalini n.k.

Unasema watu makini wasiokuwa na tuhuma kwenye vyama!! Hushangai tuna mtu aliyefanya ufisadi ulioripotiwa na CAG Ikulu?

Naheshimu sana ulichokisema lakini ni vyema bado tukaona, kwa jicho la tatu, hatua tulizopiga za maendeleo. Najua wengi wangependa nchi yetu iwe kama Ulaya kwa hiyo miaka 56 baada ya uhuru!

Hatua zipi tulizopiga? Hatua tulizopiga ukilinganisha na rasilimali tulizo nazo na fedha ambazo serikali za CCM imezifisidi, ni kazi bure kabisa!

Ndiyo inawezekana kabisa. Dunia ya leo iliyoendelea katika enabling conditions za maendeleo, Tanzania haihitaji kuchukua muda mrefu kama vile nchi za Ulaya zilivyochukua? Mbona Singapore (iliyokuwa maskini hadi miaka ya 1980), China, South Korea, Malaysia, Taiwan, na Hong Kong hazijachukua miaka mingi? Brazil na India sasa ni middle income nations!

Lakini tukubaliane kwamba maendeleo ni safari ndefu na ngumu na yenye kuhitaji mshikamano. Changamoto zinazojitokeza katika kutukawiza kufika huko tunakotamani, nazo ni fursa!

Hii ni dhana potofu sana. Hapo juu nimeelezea kwanini ni dhana potofu; kwani kuna mataifa ambayo hayajachukua hiyo safari ndefu ya zaidi ya miaka 50 ya kujitegemea!

Tupambane nazo ili kuwa na Taifa lenye nguvu!
Tujitafakari!

Taifa la CCM!!!
 
Wapi nimefanya ulinganishi huo? Ninachokisema ni kwamba iweje miaka 56 ya Uhuru nchi ishindwe hata kuwa imekamilisha hata jambo moja kwa asilimia 100?

Wananchi jukumu letu kubwa ni kuchangia mfuko wa serikali kupitia kodi na uwajibikaji. Haya yote serikali ina jukumu la kuweka mazingira ya watu kulipa kodi na kuwajibika.

Serikali inapoomba kura, uomba kupewa nafasi ya kutumia kodi zetu ili kuweka mazingira ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupata maendeleo.

Sasa sijui unataka wananchi tufanye zaidi ya haya?

Kama nilivyosema hapo juu, serikali inapaswa kuweka mazingira ya uwajibikaji. Ukiona wapiga dili wanasumbua, hiyo ni dalili ya serikali dhaifu. Morals lazima zijengwe kwa uwepo na enforcement ya sheria. Sheria tunazo, lazima serikali kupitia viongozi wake ndiyo wavunjaji wakubwa!

Uwa napenda kutumia mfano wa sekta ya kilimo. Sekta hiii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya watanzania. Lakini serikali imeitupa sekta hii; serikali imeshindwa kutenga asilimia 10 ya bajeti kwenye sekta kama ilivyokubaliwa kupitia Azimio la Maputo la mwaka 2003.

Kwa ujumla, Tanzania hakuna mazingira mazuri kwa watu maskini kuendelea. Wataendeleaje kama serikali haiweki nguvu kubwa kwenye kundi lililo kubwa zaidi?

Kwa hiyo unataka kusingizia ongezeko la watu kuwa ndiyo sababu ya Tanzania kuwa maskini? Sasa projections zinazofanywa na population censuses uwa ni za kazi gani? Na China au India watasemaje sasa? China wapo 1/3 ya word population, lakini wanazidi kusonga mbele tu! Wanatumia idadi yao kubwa kujiendeleza zaidi. Sisi tupo milioni 50 tu, kwenye nchi yenye ukubwa wa ardhi wa 945,087 Km², halafu unaongelea uwiano wa watu na huduma za jamii!

Unaongelea vyama vya upinzani? CCM hawajawahi kusikiliza vile vyama vya upinzani vinavyoshauri. Madhara yake tumeyaona kwenye sekta ya madini, ufisadi uliokithiri serikalini n.k.

Unasema watu makini wasiokuwa na tuhuma kwenye vyama!! Hushangai tuna mtu aliyefanya ufisadi ulioripotiwa na CAG Ikulu?

Hatua zipi tulizopiga? Hatua tulizopiga ukilinganisha na rasilimali tulizo nazo na fedha ambazo serikali za CCM imezifisidi, ni kazi bure kabisa!

Ndiyo inawezekana kabisa. Dunia ya leo iliyoendelea katika enabling conditions za maendeleo, Tanzania haihitaji kuchukua muda mrefu kama vile nchi za Ulaya zilivyochukua? Mbona Singapore (iliyokuwa maskini hadi miaka ya 1980), China, South Korea, Malaysia, Taiwan, na Hong Kong hazijachukua miaka mingi? Brazil na India sasa ni middle income nations!

Hii ni dhana potofu sana. Hapo juu nimeelezea kwanini ni dhana potofu; kwani kuna mataifa ambayo hayajachukua hiyo safari ndefu ya zaidi ya miaka 50 ya kujitegemea!

Taifa la CCM!!!
Hakuna nchi hata moja humu ulimwenguni ambayo imaekamilisha jambo hata moja. Ndio maana mapambano ya maendeleo hayaishi (kwa serikalini na watu) kwa sababu hayana mwisho! Aidha, si kweli kwamba hakuna mazingira mazuri ya kujiendeleza. Naamini kwamba yapo ya kutosha na ndio maana katika nchi hii kuna watu ambao bidii na maarifa yao vimewatoa baada ya kubaini fursa lukuki zilizopo.
Naomba uvute subira, kama matamanio yako ni kuiona Tanzania iking'ara kimaendeleo, kwani muda si mrefu utaona Taifa jipya na CCM mpya isiyokuwa na akina Lowasa, Sumaye, Mtei, Nyalandu, Kingunge, Mgeja, Mahanga, nk nk!
 
Hakuna nchi hata moja humu ulimwenguni ambayo imaekamilisha jambo hata moja. !

Ndivyo unavyojidanganya!!

Unafikiri Uswisi, Ujerumani, Uholanzi, Denmark, Norway, Sweden, na Finland, wana shida za huduma za kijamii kama maji, umeme, elimu, afya, na barabara? Uswisi maji ya kunywa yapo kila sehemu, na ni bure!! Scandinavia elimu ni bure hadi chuo kikuu kama ilivyo Ujerumani. Na siyo bora elimu, ni elimu bora, serikali zinatoa world class education kwenye taasisi zake za elimu!!

Unafikiri kwanini nchi hizo zina luxury hadi ya kutoa misaada kwa Tanzania? Zingekuwa hazijakamilisha hata jambo moja unafikiri wananchi wake wangekubali serikali zao kutoa misaada??

Tanzania chini ya CCM, imeshindwa kukamilisha hata jambo moja tu kwa miaka yote 56!!! Halafu, viongozi wanaendelea kuishi kifahari kabisa! No wonder waziri wa uchukuzi alitetea matumizi ya mashangingi ati yanatoa comfort na safety kwa viongozi!!

Aidha, si kweli kwamba hakuna mazingira mazuri ya kujiendeleza. Naamini kwamba yapo ya kutosha na ndio maana katika nchi hii kuna watu ambao bidii na maarifa yao vimewatoa baada ya kubaini fursa lukuki zilizopo.!

Kungekuwa na mazingira ya kujiendeleza, ukuaji wa uchumi wa asilimia 7 kwa zaidi ya miaka 10+ ungekuwa ume-trickle down kwa watu maskini kabisa. Lakini kinyume chake ni kuwa na ukuaji huo wa uchumi, huku watu wakizidi kuwa maskini.

Bila sekta ya kilimo kupewa kipaumbele namba moja, taifa litaendelea kuwa na watu walio kwenye dimbwi la umaskini. Yaani nchi yetu bado ina asilimia kubwa ya peasants i.e. bado tuna agrarian societies! Hakuna muujiza zaidi ya kilimo kupewa kipaumbele namba moja. Kisha elimu ifuate, ambayo itakuza pia teknolojia na ugunduzi. Hivi ndivyo ‘Asian Tiger economies’ zilivyofanya.

Na mwisho, kama bado Washington (WB na IMF) ndiyo inapanga sera zetu za kiuchumi, tusahau kabisa kuendelea! Hizi taasisi hazijawahi kufanikiwa sehemu yoyote post WWII!

Naomba uvute subira, kama matamanio yako ni kuiona Tanzania iking'ara kimaendeleo, kwani muda si mrefu utaona Taifa jipya na !

CCM imekuwa ikisema hivyo kwa miaka 56 sasa! And it has been extremely disappointing!! Tanzania mpya ambayo Rais anajichotea tu mapesa bila kuidhinishwa na Bunge? Tanzania mpya ambayo 70% ya wananchi wanategemea kilimo (ukulima na ufugaji), lakini serikali inatenga bilioni 24 kwenye kilimo huku ikitenga bilioni 500 kununua ndege!! Hii ndiyo Tanzania mpya kweli!!

Under CCM, taifa hili halitoendelea kamwe! CCM ndiyo chanzo cha hali tuliyonayo kama taifa. Wizi, ufisadi, ufujaji wa pesa za umma, mikataba mibovu ya maliasili n.k., yote yamesababishwa na CCM, ambayo Magufuli amekuwa mwanachama na kiongozi mwandamizi wa serikali kwa miaka 20!

CCM mpya isiyokuwa na akina Lowasa, Sumaye, Mtei, Nyalandu, Kingunge, Mgeja, Mahanga, nk nk!

Ndivyo unavyojidanganya hivyo!! Hoja nyepesi kwa suala zito! Kwahiyo unataka kusema hao uliowataja ndiyo walikuwa kikwazo cha kuwa na CCM mpya na taifa lenye maendeleo?!?! Sasa with all the power, mbona serikali haiwafikishi Mahakamani watu hao?!?

Kila siku nasema humu, Magufuli na most CCM crooks walipaswa kuwa jela!

Vipi kuhusu Chenge, Ngeleja, Tibaijuka n.k.

Ati CCM mpya! Ina upya gani? Magufuli has been a CCM cadre and crook for over 20 years. Ukienda jimboni kwake Chato, utaona jinsi CCM isivyokuwa na maana! Mangula has been a CCM cadre for ages! Kinana has been a CCM cadre and crook for ages. Au unajisahaulisha kwamba meli ya kampuni ya Kinana ilikutwa na ivory?!!?
 
Nina hamu na WAPINZANI NDANI YA CCM. SIJUI LINI WATAANZA MAKEKE YAO. AU SIJUI WATAKUA "NDIO MZEE?"
 
Ndivyo unavyojidanganya!!

Unafikiri Uswisi, Ujerumani, Uholanzi, Denmark, Norway, Sweden, na Finland, wana shida za huduma za kijamii kama maji, umeme, elimu, afya, na barabara? Uswisi maji ya kunywa yapo kila sehemu, na ni bure!! Scandinavia elimu ni bure hadi chuo kikuu kama ilivyo Ujerumani. Na siyo bora elimu, ni elimu bora, serikali zinatoa world class education kwenye taasisi zake za elimu!!

Unafikiri kwanini nchi hizo zina luxury hadi ya kutoa misaada kwa Tanzania? Zingekuwa hazijakamilisha hata jambo moja unafikiri wananchi wake wangekubali serikali zao kutoa misaada??

Tanzania chini ya CCM, imeshindwa kukamilisha hata jambo moja tu kwa miaka yote 56!!! Halafu, viongozi wanaendelea kuishi kifahari kabisa! No wonder waziri wa uchukuzi alitetea matumizi ya mashangingi ati yanatoa comfort na safety kwa viongozi!!

Kungekuwa na mazingira ya kujiendeleza, ukuaji wa uchumi wa asilimia 7 kwa zaidi ya miaka 10+ ungekuwa ume-trickle down kwa watu maskini kabisa. Lakini kinyume chake ni kuwa na ukuaji huo wa uchumi, huku watu wakizidi kuwa maskini.

Bila sekta ya kilimo kupewa kipaumbele namba moja, taifa litaendelea kuwa na watu walio kwenye dimbwi la umaskini. Yaani nchi yetu bado ina asilimia kubwa ya peasants i.e. bado tuna agrarian societies! Hakuna muujiza zaidi ya kilimo kupewa kipaumbele namba moja. Kisha elimu ifuate, ambayo itakuza pia teknolojia na ugunduzi. Hivi ndivyo ‘Asian Tiger economies’ zilivyofanya.

Na mwisho, kama bado Washington (WB na IMF) ndiyo inapanga sera zetu za kiuchumi, tusahau kabisa kuendelea! Hizi taasisi hazijawahi kufanikiwa sehemu yoyote post WWII!

CCM imekuwa ikisema hivyo kwa miaka 56 sasa! And it has been extremely disappointing!! Tanzania mpya ambayo Rais anajichotea tu mapesa bila kuidhinishwa na Bunge? Tanzania mpya ambayo 70% ya wananchi wanategemea kilimo (ukulima na ufugaji), lakini serikali inatenga bilioni 24 kwenye kilimo huku ikitenga bilioni 500 kununua ndege!! Hii ndiyo Tanzania mpya kweli!!

Under CCM, taifa hili halitoendelea kamwe! CCM ndiyo chanzo cha hali tuliyonayo kama taifa. Wizi, ufisadi, ufujaji wa pesa za umma, mikataba mibovu ya maliasili n.k., yote yamesababishwa na CCM, ambayo Magufuli amekuwa mwanachama na kiongozi mwandamizi wa serikali kwa miaka 20!

Ndivyo unavyojidanganya hivyo!! Hoja nyepesi kwa suala zito! Kwahiyo unataka kusema hao uliowataja ndiyo walikuwa kikwazo cha kuwa na CCM mpya na taifa lenye maendeleo?!?! Sasa with all the power, mbona serikali haiwafikishi Mahakamani watu hao?!?

Kila siku nasema humu, Magufuli na most CCM crooks walipaswa kuwa jela!

Vipi kuhusu Chenge, Ngeleja, Tibaijuka n.k.

Ati CCM mpya! Ina upya gani? Magufuli has been a CCM cadre and crook for over 20 years. Ukienda jimboni kwake Chato, utaona jinsi CCM isivyokuwa na maana! Mangula has been a CCM cadre for ages! Kinana has been a CCM cadre and crook for ages. Au unajisahaulisha kwamba meli ya kampuni ya Kinana ilikutwa na ivory?!!?
Nafarijika ninapoona ukihimiza hoja ya kilimo kupewa kipaumbele na kukiwekea msukumo unaostahili! Nashukuru sana kwani Watanzania wengi wanategemea kilimo kama ajira kuu kwao. Naamini serikali iliyo sikivu itakuwa imesikia!
Jambo ambalo nashindwa kuelewa na kuamini ni dhana ya kuilinganisha Tanzania (nusu karne) na Ulaya (zaidi ya karne) kimaendeleo! Aidha, kukiri kwamba IMF na WB ndizo zimekuwa zikiiamulia Tanzania namna ya kuendesha uchumi wake huku ukitarajia mabadiliko hayo unayoyasema ni kichekesho na ni ushahidi kwamba unajua moja ya sababu ambazo zimedumaza maendeleo ya nchi hii!
Maana yangu ya kuwataja niliowataja haikuwa na maana unayoitaja. Maana yangu ilikuwa kwamba chama kikuu cha upinzani kuwa na safu ya uongozi iliyohama kutoka CCM kisitarajie kusaidia kuleta mabadiliko katika nchi hii kwani hali iliyopo nchini, wao ni miongoni mwa walioitengeneza!
Cha msingi (bottomline) ni kwamba mtu pekee ambaye haioni Tanzania mpya inayokuja atakuwa ama nafanya hivyo kwa makusudi au ana upofu au uziwi ambao utaendelea kumtesa na atakufa kama vile hakuishi kamwe (dying as if he never lived)! Na kwamba tutoe ushauri wa dhati wa namna ya kusonga mbele badala ya ama kununa au kukejeli! Isije ikawa kama yule mzee mpumbavu aliyeambiwa na mwanawe, wakati wakivuka bahari ya Mediterranean, kwamba " baba, meli inazama" naye kwa kejeli akasema "mwanangu usijali, hii meli sio yetu"!
Tujitafakari!
 
Nafarijika ninapoona ukihimiza hoja ya kilimo kupewa kipaumbele na kukiwekea msukumo unaostahili! Nashukuru sana kwani Watanzania wengi wanategemea kilimo kama ajira kuu kwao. Naamini serikali iliyo sikivu itakuwa imesikia!

Serikali sikivu? Bro, Maputo Declaration ni ya mwaka 2003! For 14 years, serikali za CCM hazijawahi hata kutenga asilimia 5 ya bajeti yake kwenye kilimo.

Are you a robot? Nimekwambia, this time serikali imetenga bilioni 24 kwenye kilimo, huku ikitenga bilioni 500 kununua ndege! Halafu unasema serikali sikivu!!

Jambo ambalo nashindwa kuelewa na kuamini ni dhana ya kuilinganisha Tanzania (nusu karne) na Ulaya (zaidi ya karne) kimaendeleo!

Nimekupa mifano ya Tiger economies. Hizi si nchi za Ulaya. Nimekwambia Tanzania ilikuwa na kiwango kwenye miaka ya 1960. Hapa naongelea nchi kama South Korea, Taiwan, Singapore na Hong Kong. Leo nchi hizi zinatoa misaada kwa Tanzania. Nchi hizi hazikutoa visingizio kama unavyotoa. South Korea leo ni leading hub ya manufacturing na innovation ya electronic equipment.

Aidha, kukiri kwamba IMF na WB ndizo zimekuwa zikiiamulia Tanzania namna ya kuendesha uchumi wake huku ukitarajia mabadiliko hayo unayoyasema ni kichekesho na ni ushahidi kwamba unajua moja ya sababu ambazo zimedumaza maendeleo ya nchi hii!

Sasa kwani IMF na WB ziliilazimisha Tanzania kufuata sera zao? Zile Four Asian tigers wala hazikufuata sera za IMF/WB. Ni sawa na mnavyolialia ‘kuibiwa’ kwenye madini as if wawekezaji waliwashikia bunduki wakati wa kusaini mikataba!! Kufuata sera za IMF/WB ni kutokana na serikali za CCM, haswa post-Nyerere kutokuwa bunifu, na kujawa na vitendo vya rushwa na ufisadi, kulikopelekea kile alichokianzisha Nyerere kupotea. Nyerere was visionary kwa import substitution policy! Kungekuwepo na usimamizi wa kutosha, leo hii Tanzania ingekuwa miongoni mwa ‘lion economies’.

Cha msingi (bottomline) ni kwamba mtu pekee ambaye haioni Tanzania mpya inayokuja atakuwa ama nafanya hivyo kwa makusudi au ana upofu au uziwi ambao utaendelea kumtesa na atakufa kama vile hakuishi kamwe (dying as if he never lived)!

Hakuna Tanzania mpya kama bado kilimo hakipewi kipaumbele chifu. Stop this silly talk! Tanzania gani mpya kwa serikali kutenga bilioni 24 kwenye kilimo (15B zikiwa ni misaada na 9B ni fedha za ndani), huku ikitenga 500B kununua ndege kwenye taifa ambalo takribani asilimia 70 ya wananchi wake ni peasants wanaotegemea subsistence agriculture?

It would have made a difference kama kungekuwa na trickle down economies. Lakini serikali iliyojawa na rushwa, inazuia hilo kutokea. Kuwa na Rais ambaye anajichotea tu mapesa Hazina bila ya idhini ya Bunge, nako hakusaidii! Ama kweli ni Tanzania mpya! Maana we have never had such a practice: kwa Rais kujichotea tu mapesa Hazina bila ya Bunge kupanga!!

Na kwamba tutoe ushauri wa dhati wa namna ya kusonga mbele badala ya ama kununa au kukejeli!

Rais Magufuli alishasema yeye hashauriki! Maana hakuna aliyempangia kugombea urais. Alichukua mwenye fomu! Sasa unataka tutoe ushauri upi?

Btw, hakuna jipya katika ninayozungumza. Kama suala la kukipa kilimo kipaumbele ni jambo ambalo lipo at least kutokea mwaka 2003. Serikali ilikuja na CAADP, ASDP, DADPs, Kilimo Kwanza, Big Result Now n.k. Leo yote hayo yamewekwa kando ili tununue ndege kwa bilioni 500 na kujenga uwanja ndege kwa bilioni 39 kwenye eneo ambalo halina trickle down effect kwenye uchumi!!
 
Namsikiliza, kiukweli huyu jamaa yuko vizuri, anazungumzia udhaifu mkubwa wa vyama vya upinzani nchini, ni kuitumia CCM kama role model ya chama tawala, hivyo concentration ya upinzani ni kutumia udhaifu wa CCM. This is very valid argument.

Niliwahi kusisitiza humu kuwa
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike
CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!

Paskali

Paskali

Tatizo la upinzani wa nchini mwetu ukiwaambia ukweli wewe unabandikwa uccm hata kama ulikuwa una lengo la kuwasaidia ili waweze kutoa changamoto yenye nguvu kwa chama tawala, Wee angalia hata hizi comments zao tu kwenye hii post.

Niruhusu Pia niongeze mada inayohusiana na hii

Actually me nilitegemea CHADEMA wangemuadhibu John Heche kwa kugomea kwenda kwenye kipindi hicho cha Star tv kwa kutoa sababu za kipuuzi na kijinga kabisa kuwa "Hadhi" yake kama mbunge hawezi kudiscuss hii mada na Alberto Msando. Hicho ni kichaka cha mtu asiye na hoja.

Hao ndiyo watu wanaotuomba ridhaa ya kuongoza nchi, hao ndiyo watu wanaolialia kila siku kwenye media kuwa nchii hii ni yetu sote siyo ya ccm peke yao hivyo kila mtu ana haki ya kutoa mchango wake kwa uhuru na haki.

JE? Kama John Heche amekataa kukaa na kudiscuss na Alberto Msando leo kwa kigezo cha "Hadhi"siku CDM wakipata madaraka na Heche akateuliwa kuwa PM (Ofcourse naomba Mungu isitokee) unahisi atakaa na diwani kudiscuss maswala ya maendeleo????.

Kwa itikadi hiyo ya "Hadhi" kwa mujibu wa Heche ni kwamba Mpaka sasa hatuna mtu kutoka upinzani ambaye anaweza kudiscuss kitu chochote na Waziri Mkuu Majaliwa isipokuwa Mbowe peke yake maana Mbowe ndiyo KUB ambaye ki hadhi pale bungeni ni sawa na waziri mkuu, hivyo kwa mtu yeyote kutoka upinzani akijaribu kuaddress au kuonesha kutokupendezwa na issue yoyote iliyotolewa na PM mtu huyo ni kichaa asiyejua mipaka yake (Si mimi ni John Heche).

Tukienda mbali zaidi kwakuwa CDM mpaka sasa hakuna mtu mwenye hadhi sawa na Rais wa JMT kitendo chochote cha Mbowe na wabunge wake kukaa na kujadili matamko ya Rais ni ukosefu wa nidhamu na ni upuuzi kwa kuwa hawajui level ya hadhi zao na mipaka yao ki itifaki.

Je hiki ndicho anachomaanisha John Heche??? Je CHADEMA wanakubaliana nacho???

Paskali tuwasaidie wapinzani kusimama sehemu sahihi bado tunawahitaji sana kwenye kuisimamia serikali.
 
Back
Top Bottom