Mikutano ya hadhara na Maandamano ni haki ya msingi ya Vyama Vya siasa kwa mujibu wa Sheria

Gini

JF-Expert Member
Oct 11, 2018
398
385
MIKUTANO YA HADHARA

Na George Sylvester Wambura,

Mikutano ya hadhara na Maandamano ni haki ya msingi ya Vyama Vya siasa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa sura ya 258. Ukisoma kwenye haki za vyama vya siasa utaona haki zilizoainishwa katika Sheria hiyo ni pamoja na,
1. (e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Rais Samia kuondoa zuio hilo lililowekwa na Hayati John Pombe Magufuli mnamo 2015 ni sahihi kabisa kwa kuwa mtaji wa mwana siasa ni watu katika misingi ya kuuza sera.

Unapozuia Wanasiasa kufanya Mikutano ambayo kimsingi kwa muktadha wa Nchi Yetu ndiyo inayowaleta watu pamoja kwa kuwa Teknolojia haijafika kote nchini ni kuwanyima haki. Jambo la msingi kama Sheria inavyotamka ni kufanya kwa kuzingatia tamaduni za watu, kanuni na sheria za nchi.

LAKINI, mikutano hii inapoenda kuanza lazima ifahamike kuwa hakuna mwanasiasa hasa wa upinzani atafanya mikutano ya hadhara bila kuinanga Serikali na Viongozi wake, kwa kufanya hivyo isitafsirike kuikosea Serikali bali kuwakumbusha wajibu wao. Na hapa ndipo ninapoiona shida. Siamini kama Ccm wa/tumejiandaa na hili. Ni wazi kuwa Watanzania watawaunga mkono Wapinzani kwa kuwa watajikita kuongelea ugumu wa maisha unavyowatesa Watanzania. Leo mchele bila Tzs 3,500+ hupati kula UBWECHE (wali) kwa vijana wa mjini wanavyouita.

Wataongelea mikopo mingi inayokopwa na Serikali ili kutekeleza mipango ya Maendeleo, watajikita kuonesha namna mikopo hiyo imekuwa mwiba kwa Taifa, watagusia TOZO za Kielektroniki kama Miamala ya Simu, Benki, Tozo za Umeme n.k. Wataongelea haya kwa uchungu mkubwa sana na Wananchi wataona kuwa hawa pengine ndiyo watetedi wetu.

Wataongea juu ya Umasikini wa Watanzania wakilinganisha na Viongozi wanaonufaika na mifumo ya Uongozi, MLO MMOJA Vs MA VIETE ya TZS 500M kila mwaka, wataongelea Changamoto ya Ajira ambayo kwa miaka sasa imekuwa tatizo sugu kama sio bomu. Wataongelea udhaifu wa Serikali yote.
Freeman Aikaeli Mbowe, Tundu Antipas Mugway Lissu, Mchungaji Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu) , John Heche kwa kutaja wachache wana nguvu za ushawishi, kujenga hoja na hilo kila mtu anajua.

Changamoto zote hizo zinahitaji majawabu, kwa nini tumefika hapa, tunatokaje hapa n.k HOFU yangu ni moja tu, Ccm watahimili vishindo hivi, au tutarudi kulekule alipotupeleka JPM ambako ametutoa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

CHAWA wataweza kustahimili hayo, je, wataona kama ni kuinanga Serikali au kuiwajibisha na kuikumbusha Serikali kutimiza wajibu wake?
Je, vyombo vya habari vimejipanga kuripoti taarifa za wapinzani kwa mizania sawa na Ccm au nyuma ya pazia watanyooshewa vidole na kuonywa kurusha taarifa za Wapinzani? TBC kama Shirika la Umma la Utangazaji, limejipanga kutoa haki sawia kwa kila Chama cha Siasa au itafika mahala waamue kuendelea na Biashara zao kama kawa, biashara ya kupendelea upande au taarifa za upinzani zitatolewa bila matamshi ama wataushia uchochoroni?

Je, Serikali itahimili vishindo vya Tundu Antipas Mugway Lissu akiunguruma juu ya Mikataba ambayo ataiibua kuwa feki au iliyosainiwa mikakosa?
Anyway, nimpongeze Mhe Rais Dkt. Samia kwa kuona umuhimu wa ushindanishi wa sera kama namna itakaojenga na kudumisha Demokrasia ya kweli ndani ya nchi na kujenga mshikamano. Kama alivyosema Rais Samia kuwa angependa kuona siasa zinatuleta pamoja na kuchochea Maendeleo ya nchi.

Jeshi la Polisi, ni wakati wa kukaa pembeni na kuacha kujiegemeza kwenye kuona udhaifu wa Wapinzani tu bali msinamie misingi ya sheria, kanuni, taratibu na mtambue kuwa Taifa hili linajengwa kwa misingi ya Utu wetu bila kuingiza Udini, Ukabila, Ukanda, Rangi. Siasa sio uadui.

UVCCM niwakumbushe kuwa sote tunawajibu wa kupigania maendeleo ya Taifa hili, mkumbuke kuwa mmepewa dhamana ya miaka mitano (5) na Vijana wenzenu ili kuwapigania na kusimamia masilahi yao na mkumbuke kuwa ninyi ni nguvu kazi ya Taifa ya leo na baadae, msijisahau sana maana pengine wakati ujao hamtakuwa na nafasi hizo za uongozi, mifano ipo wazi, wapo waliojiona wao ndiyo wao ila sasa wamebaki kuwa sawasawa na wanachama wa kawaida. Uongozi ni dhamana/koti la kuazima.

UVCCM, siasa ni maendeleo, mna wajibu wa kusaidia vijana walio katika limbwi la umasikini kwa kukosa fursa za ajira na hata wanapojiajiri wanakosa watu wakuwashika mikono. Mifuko mingi ya kutoa Mikopo ambao ni ya Serikali, kupata mikopo hiyo unatakiwa ujipange hasa. Masharti yao ni zaidi ya Benki, siongei kwa kubahatisha, nina mifano hata mkitaka nipo tayari.

Unajiuliza hizo pesa Serikali inatoa kusaidia Vijana, Wananchi (Wajasiriamali) zinaenda wapi, nani wanufaika nazo? Ili upate mkopo katika taasisi hizo za Serikali ambazo zipo kwa ajili ya kusaidia wajasiriamali, Vigezo vya ukopaji ni, mkopaji awe na dhamana 3, dhamana yake (ajidhamini), na awe na wadhamini wengine wawili, kitu ambacho hata Benki hakipo. Ukiwa na wadhamini wawili wenye mara 3 ya mkopo unaoomba hutapewa kwa sababu ni lazima wewe mwenyewe uwe na dhamana pia ili jumla ziwe dhamana tatu (3).

UVCCM, hayo mambo ndiyo mnatakiwa mshughulike nayo na si kupiga push ups mara tunasimama na mama, Rais wetu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshasimama tayari kwa miguu yake na anatarajia kuona mnamsaidia kuwaletea maendeleo wananchi, badala yake anawashangaa mnapogeuka kuwa Chawa na kufanya mambo ya hovyo.
Tumsaidie Rais, ukimsikiliza Rais Samia unaiona dhamira yake ya kuwaletea Wananchi Maendeleo ila anakwamishwa na Wasaidizi wake, propaganda tu ndiyo wanazojua, sio wote ila wengi ni siasa tu wanafanya.
Wapo Wasaidizi wake tumekutana na kubadilishana mawazo ya kimiradi, lakini mwisho wa siku hakuna kinachofanyika.

Tumsaidie Rais Samia kwa matendo, sio uko jukwaani unaimba Samia Oyee halafu kwa ground hufanyi. Siasa ni Maendeleo, Wananchi wanataka suluhisho la changamoto zao na sio porojo tu.
Anyway, ngoja kwa leo niishie hapa.

Mtozi, George Sylvester Wambura (Mwananchi)
 
Back
Top Bottom