Kuna vyanzo mbalimbali vikielezea wapi chanzo kikuu cha Mto Nile. Lakini vyanzo hivyo vinakuwa vikipingana mara kwa mara juu ya utata huu.
Kwa chanzo chetu watanzania tulichoaminishwa kutokana na elimu yetu ni kwamba chanzo ni Ziwa Victoria.
Vyanzo vya Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Victoria Nyanza katika nchi za
Tanzania,
Burundi,
Rwanda,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Uganda na
Kenya.
Lakini watafiti wengine wanaeleza kuwa c
hanzo cha mbali kabisa ni Mto wa
Luvironza huko Burundi unaoingia katika
Mto Kagera na kufika
Ziwa Victoria Nyanza.
Kwa upande mwingine wa Nile unaanza
Ethiopia ukiitwa
Abbai au
Nile ya Buluu unatoka katika
Ziwa Tana.
Hakuna mapatano kabisa Nile inaanzia wapi. Kawaida ya
waandishi Waingerezani kuhesabu kuanzia Ziwa Victoria, waandishi wa
mataifa mengine huwa wanaweza wakaita tayari Mto Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".