Tuondoe utata hapa: Ni wapi haswa chanzo cha Mto Nile?

Tuondoe utata hapa: Ni wapi haswa chanzo cha Mto Nile?

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,426
Reaction score
12,161
Kuna vyanzo mbalimbali vikielezea wapi chanzo kikuu cha Mto Nile. Lakini vyanzo hivyo vinakuwa vikipingana mara kwa mara juu ya utata huu.

Kwa chanzo chetu watanzania tulichoaminishwa kutokana na elimu yetu ni kwamba chanzo ni Ziwa Victoria.

Vyanzo vya Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Victoria Nyanza katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Kenya.

Lakini watafiti wengine wanaeleza kuwa chanzo cha mbali kabisa ni Mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika Mto Kagera na kufika Ziwa Victoria Nyanza.

Kwa upande mwingine wa Nile unaanza Ethiopia ukiitwa Abbai au Nile ya Buluu unatoka katika Ziwa Tana.

Hakuna mapatano kabisa Nile inaanzia wapi. Kawaida ya waandishi Waingerezani kuhesabu kuanzia Ziwa Victoria, waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza wakaita tayari Mto Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".
 
Lakini kwa miaka mingi tumekuwa tukiaminishwa kwamba chanzo cha mto Nile ni ziwa Victoria pale Jinja, Uganda. Na ukifika pale kuna alama kabisa ya kudumu iliyowekwa ziwani kuonyesha mto unapoanzia ndani ya ziwa. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa mwingereza John Speke alioufanya katika miaka ya mwishoni mwa karne ya 19. Ukifika eneo hilo sehemu ya kuingilia kuna historia ya mvumbuzi huyo na maelezo ya mto Nile.
 
Maji yanaanzia Nyanza na kumwaga maji yake Bahari ya pasific huko masri

Masri wamehodhi huu mto kutokana na sheria mbovu za mabeberu
 
Chanzo chake ni kila penye maji yanye ladha ya maji inayoendana na ladha ya maji ya mto nile.
 
Kwamba nile ina vyanzo viwili maji meupe yanatoa victoria na maji blue yanatoka ziwa tana
 
MTO Nile umeanzia ziwa victory
Mimi bado sijaamini au niseme inanichanganya kuhusu hilo. Kwa maana mto unavujisha maji mda wote sasa ziwa lingeweza kupungua au kukauka kabisa.
 
kuna vyanzo mbalimbali vikielezea wapi chanzo kikuu cha mto nile. Lakini vyanzo hivyo vinakuwa vikipingana mara kwa mara juu ya utata huu.

Kwa chanzo chetu watanzania tulichoaminishwa kutokana na elimu yetu ni kwamba chanzo ni ziwa victoria.

Vyanzo vya Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria Nyanza katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Kenya.

Lakini watafiti wengine wanaeleza kuwa chanzo cha mbali kabisa ni mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika mto Kagera na kufika Ziwa Viktoria Nyanza.

Kwa upande mwingine wa Nile unaanza Ethiopia ukiitwa Abbai au Nile ya Buluu: unatoka katika Ziwa Tana.

Hakuna mapatano kabisa Nile inaanzia wapi. Kawaida ya waandishi Waingerezani kuhesabu kuanzia Ziwa Viktoria; waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza wakaita tayari mto Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".
chanzo ni CHASO
 
mto Nile chanzo chake ni bahari ya Meditrenia na maji yake yanamwagika ziwa Victoria
 
Haliwezi kauka maana ziwa victoria linapokea maji mengi sana yakilinganishwa na yanayotolewa na mto nile. Mto mara na mto kagera tu vinatosha kumfanya nile awepo kwa hali yake bila hata kutoa lita moja ziwani
Mimi bado sijaamini au niseme inanichanganya kuhusu hilo. Kwa maana mto unavujisha maji mda wote sasa ziwa lingeweza kupungua au kukauka kabisa.
 
Back
Top Bottom