Tungekuwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kama marehemu Lyatonga Mrema wakazi wa Dar wasingesumbuliwa na wahalifu kama panya road

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alitumia mbinu za kishushu kupambana na uhalifu wa kila namna.

Alikuwa akitoa siku saba majambazi kusalimisha silaha na walisalimisha.

Kura za siri zilitumika kufichua uhalifu wa wahalifu wa kila namna.

Nashangaa huyu waziri wa sasa anaongea kama vile anabembeleza wahalifu waache uhalifu.

Rip shushushu mbobezi Lyatonga Mrema.
20220916_201032.jpg
 
Wakazi wa Dar kwa uzembe wenu huo mtakoma. Kama Panya-road wanawasotesha vipi wakianza PAKA-road??
 
Alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alitumia mbinu za kishushu kupambana na uhalifu wa kila namna.

Alikuwa akitoa siku saba majambazi kusalimisha silaha na walisalimisha.

Kura za siri zilitumika kufichua uhalifu wa wahalifu wa kila namna.

Nashangaa huyu waziri wa sasa anaongea kama vile anabembeleza wahalifu waache uhalifu.

Rip shushu mbobezi Lyatonga Mrema.
View attachment 2358973
Kuropoka ni rahisi sana ila mnashindwa kufahamu kwamba ongezeko la watu linakuja na changamoto nyingi..

Miaka ya kina mrema watu walikuwa wachache kuliko Leo na changamoto za maisha zilikuwa nafuu kuliko saizi..
 
Acha upotoshaji...watu walilala milango wazi usiku kipindi cha joto.
 
pamoja na yote tambua Wamepita Mawaziri wa mambo ya ndani wengi sana lakini hakuna anaetambulika kwa utendaji bora kama Lyatonga

Nchi ina kitengo cha upelelezi, ina idara ya usalama wa Taifa yenye Maafisa kila eneo iweje ishindwe kuwatokomeza badala ya kusubiri waibuke then unaitisha press conference kutisha

au ni mchezo wa kuigiza kwa lengo fulani?

unasema zamani changamoto hizi hazikuwepo ?

wakati wa Black Mamba Dsm miaka ya mwisho ya 80 na mwanzo ya 90 ulikuwa hujazaliwa, mdogo sana au umesahau ?

ni Lyatonga ndio aliwasambaratisha hadi kizazi cha sasa kimekuwa hakina habari zao

kwa kifupi watu wa siku hizi kuanzia Vibaka, watawala, waandishi, wapinzani wamekuwa soft sana kiakili, kimwili n.k
Kuropoka ni rahisi sana ila mnashindwa kufahamu kwamba ongezeko la watu linakuja na changamoto nyingi..

Miaka ya kina mrema watu walikuwa wachache kuliko Leo na changamoto za maisha zilikuwa nafuu kuliko saizi..
 
Inasikitisha mno kuona namna tunavyopwaya kila mahali.

Incompetence is everywhere.
 
Back
Top Bottom