Tunduma: Vurugu za kidini zaibuka upya

Tunduma: Vurugu za kidini zaibuka upya

Status
Not open for further replies.
Mamamamamama,umechomwa msikiti,kwani unahusiana nini na kuchinja?! Haya sasa,si ndo mmeanza kuchomeana nyumba za Ibada.Kanisa likichomwa mnalia sana haya sasa mlie sasa msikiti umechomwa kama hamko biased.Mbona hizi virugu kwenye waislam wengi kama Dar hatusikii?Nadhani hapa kipo kinachotafutwa,ni muhimu serikali ikatatua huu mzozo haraka iwezekanavyo.Msikiti una kosa gani kwani ndio unaochinja nyama mpaka ukachomwa.Huku ni kuchezea moto jamani.
 
Natamani nchi yangu ya zamani ambapo sikumtambua mtanzania mwenzangu kwa jina,wala nyama,wala rangi,wala alikotoka ,Mungu wangu simamia nchi hii tuna kiongozi mwenye mapepo hasikii wala hambiriki ,tatizo linasambaa yeye anaangalia tu
 
Na kule wanakokula mbwa? Huwa wanachinjiwa na nani?? Na wale wanakula samakinchanga wanachinjiwa na nani??
Mtu kafuga ng'ombe wake miaka nenda rudi kasukumana naye toka shinyanga mpaka tunduma leo umpangie achinje nani??
Pambaneni haki haiombwi inatafutwa!!
Mtu asikwambie tukae kikao "chanini" habari ya kula chakula kinaingia tumboni mwako wengine wakukalie kikao?? Tunakua kwa imani? Na pasipo imani tumbo laweza kuuma! Ukapata msokoto wa tumbo- ukaendesha.
 
Muda huu kuna vurugu kubwa inaendelea maeneo ya Tunduma baina ya Wakristo na Waislam..chanzo ikiwa ni suala la kuchinja...Mpaka muda huu magari 8 wamechomwa moto na Msikiti mmoja umeshachomwa moto

du kikwete tizama hi mambo mkuu
 
Kuchinja kuchinja Ngombe,Nguruwe,Fisi,punda N.k.Hivi kama kuchinja ni imani fulani ya dini na inalazimisha mnyama halali kulingana na Dini jee wale wanaotaka kujichinjia hovyo hovyo tu kwa kisingizio cha kitoweo chao tunauhakika gani kuwa hawatolisha watu wengine nyama isio halali kwao,kwa mfano,nguruwe,fisi,punda na wengineo.Pili jamii hii mchanganyiko ilioishi pamoja kwa zaidi ya miaka 50 sasa bila kujali mchinjaji jee pale watakapo ruhusika watu ambao wakichinja wengine hawali.Jee mnataka kutuambia kuanzia sasa shughuli za arusi misiba na mengineo zenye karamu hazito jumuisha watu wa dini tofauti.Kama zitashirikisha lakini wengine wakakataa kula chakula kiliopikwa tutajisikiaje.Mnataka kutupeleka pabaya kwa maslahi yenu binafsi na wala sio dini.
 
Muda huu kuna vurugu kubwa inaendelea maeneo ya Tunduma baina ya Wakristo na Waislam..chanzo ikiwa ni suala la kuchinja...Mpaka muda huu magari 8 wamechomwa moto na Msikiti mmoja umeshachomwa moto

Sasa hii imesha kuwa soo.
 
Chanzo ni Makanisa kuchomwa Zanzibar na wakristo kuwaona waislam kama si ndugu zao tena.

Walioshitakiwa wahukumiwe ili iwe fundisho sio kuwaweka tu mpaka upepo upoe waachiwe huru
 
Hao wanao fanya fujo,dawa ni moja tu, peleka polisi piga risasi kama watano halafu ndio watakaa sawa.hakuna cha muislamu wala mkristo,changanya wote.
Kwenu nyie kupiga risasi ndio ufumbuzi wa matatizo? Kweli tabia haina dawa.
 
Hongera ccm ile mbegu mliyoipanda sasa mnaanza kuvuna
NAWATAKIA MAVUNO MEMA
 
ndio zenu utumbo mtupu mnataka kuitia nchii kwenye vurugu njama zenu za kuigawa nchi hazitafanikiwa nani asiejua kuwa ninyi ni vibaraka wa mabeberu

Pole mkuu saa nyingine ni bora kukuonea huruma tu
 
Inamana viongozi woote wa ccm hasa wasomi tulionao akina sitta, mwakiembe, membe, lowasa, nundu, januari makamba, mwigulu nchanga hawamshauri mheshimiwa rais kuhusu hili suala la udini?
 
Kumaliza mgogoro, ziwepo bucha za Wakristu peke yao na waslamu wawe na bucha zao.

Katika mkoa wenye idadi kubwa ya Wakristu kama Mbeya, haiwezekani waslamu walazimishe kuwachinjia nyama Wakristu. Halfu kuchinja kwenyewe ni ibada yao. Yaani akina Mwalaleli ambao kila baada ya nyumba Kanisa washiriki ibada ya mapepo? Haiwezekani asilani.

Nlikuheshimu sana Mkeshaji ! Nimeziona busara zako na nimeondoa shilingi yangu kwenye heshima nliyokuwa nakupatia !

Kwahiyo Waislamu wao kuchinja ni ibada na ni ibada ya mapepo sio ? Hujaondoa tatizo ila umekoleza moto yaani wewe huna tofauti na hao wazee wa CCM -Lumumba wakina nani hiii, hawana suluhisho !

Kwani miaka 50 iliyopita tamaduni hii ya kuchinja ili mule woote ilifanyika kwa watu wa dini gani ? Kwanini haikuwa ni Ibada ya mapepo ila iwe leo ?

Yale yale " Tutahakikisha nchi hii haitawaliki " !
 
Jamii ni wakristu na waislam! Labda kama unaweza kuja na ushahid wa makubaliano ya wakristo na waislam kuhusu nan achinje! We took it naturally, with respect of others bliefs but inapotokea heshma mtu anaigeuza kuwa amri ndo tatzo linapoanzia! Hatupendi yatokee thats why tunaomba tupate suluhu
 
Kwa Tunduma ninavyopajua yanaweza kutokea makubwa zaidi ya haya. Haya yote ni matunda ya propaganda za CCM, Cuf ni waislamu, CHADEMA ni wakatoliki, sasa haya ndiyo matokeo. Na hili linaweza kuwa tatizo la uamuzi wa kijinga uliotolea na DC, anayetANGUliza ukada mbele kuliko maslahi makubwa ya taifa.
Chondechonde kama kweli kuna msikiti umechomwa hili jambo si zuri, nyumba za ibada hazina budi kuheshimiwa
 
Nadhani watanzania wana hamu ya kuchinjana na si kuchinja!
 
Baada ya maandamano ya kisiasa kushindwa, sasa ni mwendo wa uchochezi wa kidini! Ilimradi NCHI ISITAWALIKE!


Why are you so blind my dear?
Huwezi kuona namna jk alivyoasisi udini.

Unashindwa kulivalia njuga suala la udini lililowazi badala yake unataka kuelekezea lawama kwa CDM?

Kwa hiyo wale maaskofu 177 walioliona na kkuliweka bayana suala la udini nao walitumwa na CdM? CDM wamenyamaza unadhani ni vibonde?

Tumia akili yako vizuri.

Akili kama zako zinatudharirisha sana Watz. Kama huna hoja afadhali unyamaze kimya utaonekana una hekima hata kama hauna.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom