Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,588
- 123,081
Umeongea kitu cha maana sana The Boss.
Kosa la ukawa ndilo hilo,ccm wanaweza kukubali tume huru na vitu vingine lakini siyo kukubali serikali tatu,ukawa walikuwa na nafasi kubwa kutengeneza mazingira mazuri ya wao kufanya kazi kupitia bunge la katiba.
Mkuu kama ni kweli hicho unachosema ni kipi kilisababisha kila siku kanuni zikawa zinabadilishwa wakati wa bunge lile? Mbona kuna wajumbe walionyesha kupinga mambo mbali mbali na wakaishiwa kutishiwa maisha? Mkuu kwa ujumla bunge lile halikuwa linataka kuleta katiba ya wananchi bali bunge lile lilitawaliwa na itikadi za kisiasa. Wazo lilikuwa linapita kwa kuangalia ni chama kipi kimesimamia hoja fulani.
Kwa mtazamo wangu kama tulitaka bunge la katiba liweze kufanya kazi kwa maslahi ya taifa, idadi ya wanasiasa haikutakiwa kuzidi makundi mengine. Kwa kitendo kile cha kujaza wanasiasa ndio kulikopelekea bunge lile kuendeshwa kwa hila, fitina na hisia za kiitikadi. Kwa ujumla wajumbe wa bunge lile zaidi ya asilimia 80 walikuwa hawajui wajibu wao ni kama walibebesha mzigo mzito kuliko uwezo wao wa kupambanua.