Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,588
- 123,080
Kwa sababu katiba iliyopo inampa Rais nguvu ya kutoa amri kwa jeshi la polisi
ingekuwa hana nguvu hiyo hata amri za kupiga marufuku asingeweza kutoa
Mkuu inakuwa kama bado hujanipata kidogo japo nakubalina na maoni yako kwa sehemu kubwa. Ngoja nikupe mfano mrahisi zaidi, leo hii polisi wamejipa mamlaka ya kutoa vibali, je sheria inasema polisi watoe vibali ili watu kukusanyika ama sheria inataka watoe ulinzi? Je hili linatekelezwa? Na kama halitekelezwi ni kipi kinachokupa imani kwenye katiba hiyo mpya wangeiheshimu? Hiyo katiba yangetekelezwa yale tu yasiyowabana watawala kwani ingechukua muda mrefu kubadili mindset za watawala.