Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Umeongea kitu cha maana sana The Boss.
Kosa la ukawa ndilo hilo,ccm wanaweza kukubali tume huru na vitu vingine lakini siyo kukubali serikali tatu,ukawa walikuwa na nafasi kubwa kutengeneza mazingira mazuri ya wao kufanya kazi kupitia bunge la katiba.

Halafu UKAWA walibembelezwa kurudi
hivyo walikuwa na nafasi ya kuweka condition ya kurudi nikupitisha tume huru ya uchaguzi
halafu wao wakubali kuacha ishu ya Tanganyika
ingekuwa better kwao
 
Hoja za tume huru ya uchaguzi haikufika
walitoka kabla....
Wangebaki ingekuwaje, mbona unakuwa kama vile ulikuwa huelewi kilichokuwa kikiendelea? CCM walikuwa wamejipanga kukwamisha hata hilo unalolisema. Hivi unakumbuka jamaa waliamua kufufua marehemu apige kura?
 
Bado katiba hii yenye viraka chungu nzima pamoja na ubaya wake inaruhusu maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani ambayo hakuna yoyote mwenye ruhusa ya kuwaamulia wapinzani nini kuzungumza kwenye mikutano yao na wapi pa kufanyia mikutano yao bila kujali kama wana mbunge kwenye jimbo husika au la. Na yeyote anayewazuia wapinzani kufanya hivyo anakiuka katiba ya nchi.

Ili mradi Rais ndo anamteua IGP basi polisi wataendelea tu kunyanyasa wapinzani
 
Katika maisha siku zote ni muhimu kukumbuka makosa tunayoyafanya
mara chache sana sisi binadamu tunakumbuka na kukubali makosa
ambayo tumeyafanya zamani na yanakuja kutuumiza leo....

Kama ndugu Tundu Lissu atapitia hapa ni vizuri akakumbuka kitu....

'Bunge la Katiba'.....

Hakuna mtu katika bunge lile la katiba aliekuwa na nguvu kama Tundu Lissu
yeye alikuwa ndo 'roho' ya kila mtu alietaka 'Rasimu ya Warioba'

hata UKAWA ni kama alianzisha yeye....na wengine wakamuunga mkono...

Itoshe kusema kuwa kama Tundu Lissu angeweza kuwashawishi wenzie wabaki kwenye bunge
la katiba kwa 'faida' zingine...hilo lingewezekana

Tusisahau original wanaUKAWA walikuwepo hadi wana CCM....ambao walikuwa
wanataka 'Rasimu ya Warioba' iheshimiwe.....

lakini kosa kubwa kabisa la wanaUKAWA ni 'kubeba hoja za Tanganyika' mbele ya hoja zoote
muhimu za Rasimu ya Warioba.....

Rasimu ya Warioba ilikuwa ina faida nyingi zaidi

1.Tume huru ya uchaguzi
2.Kufuta wakuu wa wilaya
3.kupunguza madaraka ya Rais... na kadhalika na kadhalika

Leo Tundu Lissu anakamatwa na polisi kwa 'amri za wanasiasa'
Bunge la katiba lilikuwa na nafasi ya kupiga marufuku polisi kupewa amri ya kumkamata mtu...

Hata Kenya now wametuacha.....Rais wa Kenya hawezi kuitumia polisi kukamata wapinzani wake
washalimaliza hilo kwa kupitia katiba.....

Leo Rais anateua makada kuwa wakuu wa wilaya na ma DAS...
Katiba hii iliyopo ambayo Magufuli anaitumia ni mbovu kuliko ile ya Samuel Sitta

Laiti kama Tundu Lissu angetumia ushawishi wake japo kupata 'katiba nafuu'
kuliko hii anayoitumia Magufuli now...huenda leo wapinzani wasingekuwa 'wanalia kupigwa marufuku siasa'.....

Leo Magufuli angelazimika tu kuheshimu na kufuata baadhi ya vitu
Polisi wasingepokea amri ....
wakuu wa mikoa na wilaya labda wasingekuwepo hawa waliopo na kadhalika.....

Tukubali tu kwa Wana UKAWA then kususa kushiriki katika bunge la katiba na kuipinga Katiba
ya Sitta ambayo laiti wangeshiriki ingekuwa better kuliko hii....ilikuwa a big mistake....

sasa haya ndo mavuno.........tumerudi nyuma miaka 50.......
some opportunities never comes twice....
Mr, nithubutu kusema Mara nyingi wewe huongea kwa kifupi, huchangia kifupi.
Lakini thread hii kwangu mimi ni katika thread bora jukwaani.

Hakika ni funzo kwa walioambiwa ujumbe huu.
Yasijiludie tena huko mbele.

"Think twice before you act"
 
Wangebaki ingekuwaje, mbona unakuwa kama vile ulikuwa huelewi kilichokuwa kikiendelea? CCM walikuwa wamejipanga kukwamisha hata hilo unalolisema. Hivi unakumbuka jamaa waliamua kufufua marehemu apige kura?

Ugomvi mkubwa wa CCM ulikuwa ni Tanganyika
tume huru hakuna haikujadiliwa kabisa
 
Katika maisha siku zote ni muhimu kukumbuka makosa tunayoyafanya
mara chache sana sisi binadamu tunakumbuka na kukubali makosa
ambayo tumeyafanya zamani na yanakuja kutuumiza leo....

Kama ndugu Tundu Lissu atapitia hapa ni vizuri akakumbuka kitu....

'Bunge la Katiba'.....

Hakuna mtu katika bunge lile la katiba aliekuwa na nguvu kama Tundu Lissu
yeye alikuwa ndo 'roho' ya kila mtu alietaka 'Rasimu ya Warioba'

hata UKAWA ni kama alianzisha yeye....na wengine wakamuunga mkono...

Itoshe kusema kuwa kama Tundu Lissu angeweza kuwashawishi wenzie wabaki kwenye bunge
la katiba kwa 'faida' zingine...hilo lingewezekana

Tusisahau original wanaUKAWA walikuwepo hadi wana CCM....ambao walikuwa
wanataka 'Rasimu ya Warioba' iheshimiwe.....

lakini kosa kubwa kabisa la wanaUKAWA ni 'kubeba hoja za Tanganyika' mbele ya hoja zoote
muhimu za Rasimu ya Warioba.....

Rasimu ya Warioba ilikuwa ina faida nyingi zaidi

1.Tume huru ya uchaguzi
2.Kufuta wakuu wa wilaya
3.kupunguza madaraka ya Rais... na kadhalika na kadhalika

Leo Tundu Lissu anakamatwa na polisi kwa 'amri za wanasiasa'
Bunge la katiba lilikuwa na nafasi ya kupiga marufuku polisi kupewa amri ya kumkamata mtu...

Hata Kenya now wametuacha.....Rais wa Kenya hawezi kuitumia polisi kukamata wapinzani wake
washalimaliza hilo kwa kupitia katiba.....

Leo Rais anateua makada kuwa wakuu wa wilaya na ma DAS...
Katiba hii iliyopo ambayo Magufuli anaitumia ni mbovu kuliko ile ya Samuel Sitta

Laiti kama Tundu Lissu angetumia ushawishi wake japo kupata 'katiba nafuu'
kuliko hii anayoitumia Magufuli now...huenda leo wapinzani wasingekuwa 'wanalia kupigwa marufuku siasa'.....

Leo Magufuli angelazimika tu kuheshimu na kufuata baadhi ya vitu
Polisi wasingepokea amri ....
wakuu wa mikoa na wilaya labda wasingekuwepo hawa waliopo na kadhalika.....

Tukubali tu kwa Wana UKAWA then kususa kushiriki katika bunge la katiba na kuipinga Katiba
ya Sitta ambayo laiti wangeshiriki ingekuwa better kuliko hii....ilikuwa a big mistake....

sasa haya ndo mavuno.........tumerudi nyuma miaka 50.......
some opportunities never comes twice....

Hiyo katiba ya warioba haijaanza kufanya kazi hata kama wangekuwepo wakaipigania isingekuwa sulihisho la leo ingefanyiwa mizengwe tu

Pili kama Rais anatumia katiba ye sasa kutuma polisi wakamate wapinzani katiba hiyo pia inatoa uhuru wa wapinzani kufanya mikutano na maandamano..sasa aitumie kama inavyotakiwa na vifungu vyote
 
Jikite kwenye mada
Sidhani kama umeelewa maudhui ya mada.
Nilichosema ni wazi, jazba zisizo na mantiki ndizo zimeifikisha UKAWA hapo ilipo, kuwa na ligi zisizoisha kupambana na dola, badala ya kuweka mikakati endelevu ya jinsi ya kufikia katika Katiba inayohitajika na wananchi.
Ujinga uliopo ni kufikiria ni UKAWA tu inahitsji katiba mpya, ni wananchi wengi tu wangependa katiba bora.
 
Hiyo katiba ya warioba haijaanza kufanya kazi hata kama wangekuwepo wakaipigania isingekuwa sulihisho la leo ingefanyiwa mizengwe tu

Pili kama Rais anatumia katiba ye sasa kutuma polisi wakamate wapinzani katiba hiyo pia inatoa uhuru wa wapinzani kufanya mikutano na maandamano..sasa aitumie kama inavyotakiwa na vifungu vyote

Wangeshiriki hakuna anaejua wangepata nini
si wapinzani hawa hawa walijadili Escrow?
na watu wakajiuzulu?
wangeshindwa nini kupata mengine hata la kuzuia tu Rais kuamuru jeshi la polisi?
 
Bado katiba hii yenye viraka chungu nzima pamoja na ubaya wake inaruhusu maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani ambayo hakuna yoyote mwenye ruhusa ya kuwaamulia wapinzani nini kuzungumza kwenye mikutano yao na wapi pa kufanyia mikutano yao bila kujali kama wana mbunge kwenye jimbo husika au la. Na yeyote anayewazuia wapinzani kufanya hivyo anakiuka katiba ya nchi.

Very good
upo sahihi
 
Mkuu The Boss, hebu tukumbushe ni nini hasa kilichowafanya Ukawa watoke nje kwenye Bunge la Katiba?

Rasimu ilitaja serikali tatu
CCM walipinga hilo.....hiko ndo kilikuwa kipengele cha mwanzo
wapinzani wakatoka nje hata kipengele cha tume huru ya uchaguzi hakijafikiwa
matokeo yake ndo haya Tume ya Lubuva....
 
Ile rasimu ya warioba ilikua haiwezi kupita kwa jinsi ilivyokua inaweza kuleta uwiano sawa na kupunguza nguvu za madaraka ya raisi sidhani kwa uelewa wa watanzania wakubwa kuna kiongozi angeweza kuruhusu lile swala lipite pia asilimia kubwa ya wawakilishi bungeni ni wafuata mkumbo maana uelewa wao ni mdogo au hata kama mtu akiwa na uelewa mkubwa kwa ulevi wa madaraka anapotosha hata kile anachoamini rejea aliekataa thesis yake ya Phd...
 
Wangeshiriki hakuna anaejua wangepata nini
si wapinzani hawa hawa walijadili Escrow?
na watu wakajiuzulu?
wangeshindwa nini kupata mengine hata la kuzuia tu Rais kuamuru jeshi la polisi?
Escrow ilijadiliwa kwa kuwa wapo waliotaka uwaziri kwahiyo walifanya hivyo ili wenzao wajiudhulu na wao wapate
ile rasimu ilikuwa nzuri ila wasingeweza kuipitisha
 
Na hata kina Lowassa,Sitta waliutaka urais
wangeshawishiwa kuwa tume huru ya uchaguzi itawapa nguvu popote kule watakapohamia....
nani anaejua leo tungekuwa wapi?
 
Tundu Lissu aliacha hoja zote za maana akaingia kwenye ushabiki wa zanzibar na tanganyika leo ndio tunaona matokeo yake
 
Mkuu katiba unayodhani ingekuwa mkombozi ndio inasiginwa vilivyo, sheria na kanuni haziheshimiki, ni matamko na utekelezaji unafuata kwakuwa ni amri toka juu sio kufuata katiba, kwahiyo hata rasimu ya Warioba ingekuwa ndio katiba kwa leo bado ingesiginwa kama hii na mihemko ingeongoza Nchi kama kawaida. Umesahau visiwani tulishaambiwa Nchi haibadilishwi kwa vikaratasi?
 
Rasimu ilitaja serikali tatu
CCM walipinga hilo.....hiko ndo kilikuwa kipengele cha mwanzo
wapinzani wakatoka nje hata kipengele cha tume huru ya uchaguzi hakijafikiwa
matokeo yake ndo haya Tume ya Lubuva....
Ni muhimu pia utambue kwamba msingi wa katiba uko kwenye eneo hilo, kama tunataka kuwa wakweli. Lakini swali langu linaweza kuwa je, unataka kutuambia kuwa kama Ukawa wangerudi kwa sharti hilo unalolisema una uhakika kwamba zisingetafutwa kura za marehemu?
 
Kuna wakati Baba wa Taifa alinukuliwa akisema "katiba hii ni nzuri sana, lakini akijitokeza kiongozi akaifuata watu watamuita dikteta "
Ndio kinachoonekana leo.
Upande wa pili wasije jisahau maana kufuata katiba ya nchi ni kiapo kinachompa mamlaka mkuu wa nchi kufanya chochote kwani ni yeye tu aliyeko juu ya sheria.
Chochote akifanyacho kijeshi ni amri.
Hili liwe funzo kwa upande wa pili kutokupuuza mambo ya muhimu kujadili kwani baadae itakuja kuwaghalimu sana .
 
Back
Top Bottom