Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Na aliehamasisha watoke nje siku ile ni Lipumba
leo Lipumba yuko wapi?

Mkuu the boss tunarudi kulekule nilikokuambia hata kama rasimu ya Warioba ingepita bado kwenye kutekeleza ingetegemea utashi wa kiongozi wa kisiasa aliyeko madarakani. Nina mifano hapa chini kukuonyesha ninachoamini kuhusu wanasiasa kutelekeleza ama kutotekeleza kile wanachosema ama kilichopo,
  1. Ulisikia maneno ya JK baada ya kupokea rasimu ya Warioba na maneno aliyozungumza baada ya wanaccm wenzake walichofanya kwenye katiba pendekezwa?
  2. Ulikuwa unasikia zile lugha za kejeli walizokuwa wanatoa wanaccm kwa tume ya Jaji Warioba ambayo H.Polepole alikuwa mjumbe? H.Polepole huyuhuyu aliyekuwa hakubaliani kabisa na cheo cha mkuu wa wilaya leo ni nani?
  3. Huyo Lipumba leo unaweza kujua anasimamia nini mpaka uweze kuwa na imani kwamba hata kama katiba ile ingepita ingetekelezwa na wanasiasa. Huku africa hakuna kutekeleza katiba kama inavyosema bali ni hila tu ndio zinaamua katiba ifuatwe vipi.
 
Mahali ambapo akili za hali ya juu ingetumika UKAWA wafanya mambo ya kijinga kuandamana na kususia vikao halali na vilivyo kaa kisheria.
Wamesusia bunge la katiba, wamesusia bunga, total work done ni zero.

Tupe mafanikio ya waliobaki bila kususia.
 
Mkuu the boss tunarudi kulekule nilikokuambia hata kama rasimu ya Warioba ingepita bado kwenye kutekeleza ingetegemea utashi wa kiongozi wa kisiasa aliyeko madarakani. Nina mifano hapa chini kukuonyesha ninachoamini kuhusu wanasiasa kutelekeleza ama kutotekeleza kile wanachosema ama kilichopo,
  1. Ulisikia maneno ya JK baada ya kupokea rasimu ya Warioba na maneno aliyozungumza baada ya wanaccm wenzake walichofanya kwenye katiba pendekezwa?
  2. Ulikuwa unasikia zile lugha za kejeli walizokuwa wanatoa wanaccm kwa tume ya Jaji Warioba ambayo H.Polepole alikuwa mjumbe? H.Polepole huyuhuyu aliyekuwa hakubaliani kabisa na cheo cha mkuu wa wilaya leo ni nani?
  3. Huyo Lipumba leo unaweza kujua anasimamia nini mpaka uweze kuwa na imani kwamba hata kama katiba ile ingepita ingetekelezwa na wanasiasa. Huku africa hakuna kutekeleza katiba kama inavyosema bali ni hila tu ndio zinaamua katiba ifuatwe vipi.

Hata JK kuna mambo yalikwenda kinyume na utashi wake
mfano ni nani kuwa Rais

so utashi wa Rais sio final.....anaweza kushindwa pia akipata upinzani mkubwa
 
CCM walienda kwenye Bunge la Katiba wakiwa na msimamo wao,na hata wale wengine walioteuliwa kwa "maelezo maalum" ambao walikuwa ndio tegemeo la wananchi kuwa akidi yaweza kutimia kwa kuunga mkono rasimu ya Warioba,nao walikuwa na "kaukasi" yao ambayo isingewezekana kwa vyovyote vile hoja yoyote kinzani na maslahi ya CCM kupita.
Rejea upigaji wa kura.

Joel wewe unazungumza uhalisia kabisa. The boss ameamua kuonyesha hisia zake ambao kimsingi hatuzipingi lakini nadhani picha hii halisi inakuwa kama haikuiona vizuri. Kilichokuwa kinaendelea kwenye bunge la katiba hakuna tofauti na kikao cha ccm kinapopanga maslahi yake.
 
Huku kutumia polisiccm ili kuwanyima haki yao wapinzani ndiyo udikteta uchwara wenyewe huo. Afute katiba na kufuta vyama vya upinzani ili turudi mwaka 47 wa mfumo wa chama kimoja. Anavyofanya si sawa na kunaweza kabisa kukaleta machafuko makubwa nchini.

Ili mradi Rais ndo anamteua IGP basi polisi wataendelea tu kunyanyasa wapinzani
 
Kwa katiba iliyopo sasa ni kipengele kipi kinaruhusu raisi kufanya anayo fanya Sasa,? Ile katiba ya BUNGE MAALUM iko wap kwa Sasa? Hizo hoja zako Hapo juu ningeziona za maana kama katiba ya sasa ingekuwa inaheshimiwa au ile ya BUNGE MAALUM ingekuwa imepitishwa.
 
Hata JK kuna mambo yalikwenda kinyume na utashi wake
mfano ni nani kuwa Rais

so utashi wa Rais sio final.....anaweza kushindwa pia akipata upinzani mkubwa

Mkuu ningetegemea upinzani kutoka kwa wajumbe wenye mawazo huru sio hao waliokuwa wanaingizwa kwenye party caucas. Mtazamo wako nakubaliana nao sana, je uhalisia ulikuwaje? Kumbuka hata bunge lile lilikuja kwenye wakati mbaya sana tena kuelekea uchaguzi mkuu. Katika mazingira yale haikuwa katiba inajadiliwa bali kampeni kuanzia huyo Magufuli mpaka kina Tindu Lissu.
 
Labda nchi ya ufipa ndio atakuwa rais Lisu.

Ila Mwenye chama lowasa ameshajitangaza ni mgombea pekee wa chadema 2020
 
Kwa katiba iliyopo sasa ni kipengele kipi kinaruhusu raisi kufanya anayo fanya Sasa,? Ile katiba ya BUNGE MAALUM iko wap kwa Sasa? Hizo hoja zako Hapo juu ningeziona za maana kama katiba ya sasa ingekuwa inaheshimiwa au ile ya BUNGE MAALUM ingekuwa imepitishwa.

Katiba ya sasa Rais anamteua IGP
hiyo inatosha kumpa nguvu ya kutoa amri
 
Kama hiki ndivyo hali halisi ilivyo ni kwa nini basi wasiruhusiwe waendelee na ujinga wao wa maandamano na mikutano ya hadhara?
Ukweli uliopo tawala wanaishiwa pumzi kila siku wamejishikiza kwenye nguvu ya serikali (majeshi)

ukiacha upinzani uendelee na spidi iliyopo ni kuimaliza pumzi kabsa sisiem na kumbuka kuna kubwa lao la mikakati ya ushindi yupo cdm, mbinu iliyobaki ni kumjazia vyeo president adhibiti upinzani kwa nguvu ya dola

ndipo unapoona kataza kataza za mikutano kuzima bunge live nk..
 
Katika maisha siku zote ni muhimu kukumbuka makosa tunayoyafanya mara chache sana sisi binadamu tunakumbuka na kukubali makosa ambayo tumeyafanya zamani na yanakuja kutuumiza leo.

Kama ndugu Tundu Lissu atapitia hapa ni vizuri akakumbuka kitu.

'Bunge la Katiba'.....

Hakuna mtu katika bunge lile la katiba aliekuwa na nguvu kama Tundu Lissu yeye alikuwa ndo 'roho' ya kila mtu alietaka 'Rasimu ya Warioba' hata UKAWA ni kama alianzisha yeye na wengine wakamuunga mkono.

Itoshe kusema kuwa kama Tundu Lissu angeweza kuwashawishi wenzie wabaki kwenye bunge la katiba kwa 'faida' zingine hilo lingewezekana

Tusisahau original wanaUKAWA walikuwepo hadi wana CCM ambao walikuwa
wanataka 'Rasimu ya Warioba' iheshimiwe.

lakini kosa kubwa kabisa la wanaUKAWA ni 'kubeba hoja za Tanganyika' mbele ya hoja zoote muhimu za Rasimu ya Warioba.

.
Kwa anaejua ......UKAWA kukomalia hii hoja faida gani ungepata Upinzani Na Taifa kwa ujumla.?

Nini hasa kilikuwa kinapiganiwa kwenye hii hoja.?
 
Kuna hili swala la katiba lakini pia kuna swala la ukosefu wa elimu kwa hawa viongozi, au kama sio elimu basi sio watu smart au waoga mno. Mfano Rais akikiuka kufata separation of power akaanza kuingilia kazi za Judiciary, ilitakiwa apewe resistance kwa kua yeye sio mkuu kule, ila in Tz they just don't care, they take his orders plain and simple without question, ukweli ni kwamba hata wakigoma nothing will happen to them coz sheria inawalinda. Its really a pitty ukiwa Tanzania neno la kiongozi yeyote yule linaweza kukurudisha kwenye umasikini, hata ambaye hajui kusoma na kuandika anamove polisi kwa mdomo tu and they don't question, wao wanafata wakisikia tu ni mtu mwenye cheo fulani.
 
Kwa anaejua ......UKAWA kukomalia hii hoja faida gani ungepata Upinzani Na Taifa kwa ujumla.?

Nini hasa kilikuwa kinapiganiwa kwenye hii hoja.?

Mahesabu ilikuwa Mungano uvunjike
ili CCM isambaratike..wapate loophole ya kushika madaraka
 
Mahesabu ilikuwa Mungano uvunjike
ili CCM isambaratike..wapate loophole ya kushika madaraka
Kwa hiyo mkuu ni kwamba hii hoja endapo ingefanikiwa ingekuwa Na manufaa zaidi kwa Upinzani kuliko Taifa.?
 
Hili ni swali zuri sana. Kwa ufupi CCM waliacha kujadili rasimu ya Warioba wakaja na msimamo wa chama, matakwa ya chama yakawa mbele zaidi ya utaifa.
Na ndio hili ambalo UKAWA walilipinga. Maana waliona pale kumbe kulikuwa na watu ambao walikuwa tayari wameamua kuwa iwe hivi,iwe mvua iwe jua,lazima iwe hivi. Sasa kama mtu mwenye akili umeshaliona hilo,kwa nini uendelee na upuuzi huo?
 
Katiba ya sasa Rais anamteua IGP
hiyo inatosha kumpa nguvu ya kutoa amri
Sasa kwa hoja Hiyo mbona sioni jipya, Maana hata kama akina Tundu lisu wangekuwepo bungeni isingezaidia kitu, sababu hiyo katiba ya BUNGE maalum sio inayotumika Kwa Sasa,!!!.
 
Back
Top Bottom