Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Tundu Lissu aliacha hoja zote za maana akaingia kwenye ushabiki wa zanzibar na tanganyika leo ndio tunaona matokeo yake

exactly my point
kumbe wangetazama zaidi maslahi mapana kuliko haya ya Tanganyika na Zanzibar
 
haya yote yamesababishwa na tabia ya kususa...leo wanasusia hili kesho wanasusia lile....

Kwenye maisha ya kawaida, huwezi kupata kila kitu, ndio maana kuna maridhiano...

Na kwa sasa, ni ngumu kurudi kwenye mjadala wa katiba mpya.....
CCM walicheza karata yao vizuri....
 
Hoja za tume huru ya uchaguzi haikufika
walitoka kabla....

The boss unakuwa kama ni mgeni wa nchi hizi za kiafrika, kwa kiwango kikubwa katiba za nchi nyingi za kiafrika zinafuatwa kutegemeana na utashi wa kiongozi na wala sio katiba inasemaje. Katika nchi hizi za kiafrika ili mengi yaliyo kwenye katiba yafuatwe ni lazima kuwe na misuguano mikali na wakati mwingine misuguano hiyo hupelekea machafuko. Katiba hii iliyopo inaruhusu wapi rais kuzuia vyama vingine kukutana na kufanya siasa mpaka mwaka kiongozi huyo aliopanga? Kwa hiyo hata kama ingekuja katiba nzuri vipi bado isingefuatwa. Kwa maneno marahisi kabisa, hiyo rasimu ya Warioba ilikuwa ni matakwa yetu wananchi, lakini uliona bila aibu kundi la watu fulani waliondoa vifungu muhimu ambavyo vilikuwa moyo wa katiba ile kwa maslahi binafsi. Kwa hiyo hata kama ingepita kwa muujiza bado kundi lile lile lingeitekeleza kulingana na maslahi yao.
 
Mapema tu umesahau visiwani uchaguzi na mizengwe mkuu?

si kwa sababu hakuna tume huru..
tume ingekuwa huru mizengwe isingekuwepo
na huko Zanzibar mgogoro wa uchaguzi hadi Jumuia za kimataifa zimesema...
 
The boss unakuwa kama ni mgeni wa nchi hizi za kiafrika, kwa kiwango kikubwa katiba za nchi nyingi za kiafrika zinafuatwa kutegemeana na utashi wa kiongozi na wala sio katiba inasemaje. Katika nchi hizi za kiafrika ili mengi yaliyo kwenye katiba yafuatwe ni lazima kuwe na misuguano mikali na wakati mwingine misuguano hiyo hupelekea machafuko. Katiba hii iliyopo inaruhusu wapi rais kuzuia vyama vingine kukutana na kufanya siasa mpaka mwaka kiongozi huyo aliopanga? Kwa hiyo hata kama ingekuja katiba nzuri vipi bado isingefuatwa. Kwa maneno marahisi kabisa, hiyo rasimu ya Warioba ilikuwa ni matakwa yetu wananchi, lakini uliona bila aibu kundi la watu fulani waliondoa vifungu muhimu ambavyo vilikuwa moyo wa katiba ile kwa maslahi binafsi. Kwa hiyo hata kama ingepita kwa muujiza bado kundi lile lile lingeitekeleza kulingana na maslahi yao.

Kwa sababu katiba iliyopo inampa Rais nguvu ya kutoa amri kwa jeshi la polisi
ingekuwa hana nguvu hiyo hata amri za kupiga marufuku asingeweza kutoa
 
Katiba ya sasa Rais anamteua mkuu wa polisi
ni rahisi kwake kumpa amri

ingekuwa katiba hana mamlaka ya kumteua mkuu wa polisi ingekuwa rahisi kuliko sasa

Nakuelewa The Boss, ila mtu akishaamua kuvunja katiba anavunja tu
Kwa case yako, anaweza akaamua kiubabe kutumia hata Jeshi kuwadeal wapinzani wake (japo nayo ni kinyume cha sheria).
 
Hiyo kenya Unaoyo itolea mfano
Ndio hiyo hiyo inayo ongoza kuua kwa risasi wale wanao ipinga serikali
Sijui nini lengo la kutafuta mfano huo.
Pili huyo lisu ni kibaraka tu wa Mbowe
Hana lolote
Mla matapishi yake kila siku
Anaishi ktk siasa kwa sababu ya ninyi vibendera hamjui kusema no
Kila kitu shangwe
 
Wao walitaka kupata kila kitu
kumbe wangepata tu hata Tume huru ya uchaguzi ingewasaidia....
Isha lizungumzia hili saana
Kwa maana ingine haya anayo yapata Lissu muache yamkumbe
Ingawa katiba inamruhusu
Aliishauri vibaya UKAWA:
Kung'ang'ania serikali 3 kama ndiyo main objective yao
Aliishauri vibaya CHADEMA:
Kumtoa Dr Slaa kumuweka Lowassa
 
Katiba ya sasa Rais anamteua mkuu wa polisi
ni rahisi kwake kumpa amri

ingekuwa katiba hana mamlaka ya kumteua mkuu wa polisi ingekuwa rahisi kuliko sasa
Boss ndugu yangu, katiba ni karatasi kama karatasi nyingine yoyote! Katiba inakuwa katiba iwapo wenye nchi wameamua kuiheshimu. Nakuapia kwa hali ilivyo hata ingepita ile katiba ya Warioba (wacha ya Sitta) bado tu watawala wangetupelekesha! BTW Kenya wana katiba mpya lakini hakuna kilichobadilika. Kina Raila bado wanaendelea kupigwa mabomu tu! Na tume yao ya uchaguzi wapinzani hawana imani yao na kuitoa imekuwa issue! Halafu nikuulize... unafikiria Kenyatta alishinda ule uchaguzi uliopita kwenye round ya kwanza?
 
Kuna wakati Baba wa Taifa alinukuliwa akisema "katiba hii ni nzuri sana, lakini akijitokeza kiongozi akaifuata watu watamuita dikteta "
Ndio kinachoonekana leo.
Upande wa pili wasije jisahau maana kufuata katiba ya nchi ni kiapo kinachompa mamlaka mkuu wa nchi kufanya chochote kwani ni yeye tu aliyeko juu ya sheria.
Chochote akifanyacho kijeshi ni amri.
Hili liwe funzo kwa upande wa pili kutokupuuza mambo ya muhimu kujadili kwani baadae itakuja kuwaghalimu sana .

Umepotea njia...ni wapi kiongozi ameifuata katiba halafu watu wakamwita dikteta? kufuta mikutano ya siasa ndio kufuata katiba? acha uzushi
 
Watu wenye nia ovu huwa hawaangali sheria kwakuwa tayari nia yao inakinzana na sheria hizo mkuu.

Sasa hivi Polisi watasema tu 'wanapokea amri
lakini ingekuwa hakuna sheria ya kumpa Rais nguvu juu ya polisi
wangeogopwa pia kushitakiwa
 
Wangeshiriki hakuna anaejua wangepata nini
si wapinzani hawa hawa walijadili Escrow?
na watu wakajiuzulu?
wangeshindwa nini kupata mengine hata la kuzuia tu Rais kuamuru jeshi la polisi?
Mkuu boss hata katiba iliyopo sasa haimruhusu rais kufanya haya anayowafanyia wapinzani!
 
Isha lizungumzia hili saana
Kwa maana ingine haya anayo yapata Lissu muache yamkumbe
Ingawa katiba inamruhusu
Aliishauri vibaya UKAWA:
Kung'ang'ania serikali 3 kama ndiyo main objective yao
Aliishauri vibaya CHADEMA:
Kumtoa Dr Slaa kumuweka Lowassa

wewe unalako jambo Lissu hakamatwi kwa issues za Dr Slaa mbona unachanganya mada?
 
Boss ndugu yangu, katiba ni karatasi kama karatasi nyingine yoyote! Katika inakuwa katiba iwapo wenye nchi wameamua kuiheshimu. Nakuapia kwa hali ilivyo hata ingepita ile katiba ya Warioba (wacha ya Sitta) bado tu watawala wangetupelekesha! BTW Kenya wana katiba mpya lakini hakuna kilichobadilika. Kina Raila bado wanaendelea kupigwa mabomu tu! Na tume yao ya uchaguzi wapinzani hawana imani yao na kuitoa imekuwa issue! Halafu nikuulize... unafikiria Kenyatta alishinda ule uchaguzi uliopita kwenye round ya kwanza?

Kenya ya leo kisiasa ni nafuu kuliko Kenya ya Moi
sisi sasa ni kama tunafanana na Kenya ya Moi....
 
Sasa hivi Polisi watasema tu 'wanapokea amri
lakini ingekuwa hakuna sheria ya kumpa Rais nguvu juu ya polisi
wangeogopwa pia kushitakiwa
Lakini katiba haisemi hivyo ila polisi wanafanya hivyo kwa amri kutoka juu kumbuka.
 
Back
Top Bottom