Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Hata wale mawakili walio watetea ile meli ya samaki wa Magufuli walikuwa mawakili kutoka Tanzania..... Tundu Lisu kutetewa na IMMA ni ishu ya kawaida hiyo ndiyo kazi ya mawakili...


Bado sioni hiki kijipeperushi alicho kiandika Jerry Murro kina mashiko.....

NB upate kichwa kimoja cha Tundu Lissu kwa ulinganyo wa kichwa cha Jerry Murro ni sawa na vichwa 152 vya Jerry Murro kwa kichwa kimoja cha Tundu Lisu
Kweli nyie hamjielewi ni kwanin mnamkweza sana huyo lissu?
Eti lissu mmoja ni Sawa na kina muro 152...
Jasho la Dr. Slaa litawatafuna milele mpaka mtubu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wale mawakili walio watetea ile meli ya samaki wa Magufuli walikuwa mawakili kutoka Tanzania..... Tundu Lisu kutetewa na IMMA ni ishu ya kawaida hiyo ndiyo kazi ya mawakili...


Bado sioni hiki kijipeperushi alicho kiandika Jerry Murro kina mashiko.....

NB upate kichwa kimoja cha Tundu Lissu kwa ulinganyo wa kichwa cha Jerry Murro ni sawa na vichwa 152 vya Jerry Murro kwa kichwa kimoja cha Tundu Lisu

Tundu Lisu hana huo uwezo unaosema...ILA amefanikiwa kuzaliwa kwenye inchi yenye watu kama wewe na kwa jinsi hiyo anaonekana booonge la genius.
 
Tuangalie tukio lenyewe na upana wa athari zake. Uvamizi wa mabomu/mass killing ni mfumo unaotumiwa na ma terrorist. Hapa kwetu Tanganyika, tunakumbuka ubalozi wa marekani ulivyoshambuliwa kwa mabomu na tuliona jinsi serikali ilivyolishughulikia suala lile. Mh Muro, naomba utuambie kwanini serikali hasa waziri wa sheria au mambo ya ndani wameshindwa kutoa tamko lolote?

Mshakuwa addicted na matamko..kila kitu mnataka tamko hahahahaa!
 
Kwa kumbukumbu zangu na kama sikosei,Jerry Muro hata uvamizi wa Bashite clouds aliutetea hadharani.

Si hivyo tu,hata Manji alipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya alionekana kuunga mkono kukamatwa kwake pale alipohojiwa channel 10 katika kipindi cha Mada Moto.

Huyo ndio Jerry.

U-DC unatafutwa kupitia migongo ya watu.
Jikite kwenye mada, Lissu hakuwashutumu IMMMA kupora mabilioni? Lissu hakumshutumu Lowassa fisadi asiyesafishika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo letu watanzania kila kitu tunataka kujibu...JERRY MURO.. kwa madudu uliyoyaandika nina wasiwasi kam ni wew umeandika.. Maana inaonekana hata ulichokiandika hukijui.... Unaifaham katiba ya TLS? Sifa za viongozi wao.. Na ndomana Rais wa nchi kuna mda anafanya majukumu ya chama, na kuna muda anafanya majukumu ya kuongoza nchi ambayo ina watu kutoka vyama tofauti..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni upi? Ok! Let's go figure>kwenye hizo fikra za muro alizoziainisha hapo neno Lissu limejitokeza zaidi ya mara sita,huku neno 'Rais wa Tls' likionekana zaidi ya mara 16! Ambapo neno 'Rais wenu' lipo zaidi ya mara mbili!! Labda uniaminishe kuwa maneno hayo yanawalenga watu tofauti tofauti,or else how undoubtly can you(muros)jump the stunt of being coward personality attackers? Or move away stealth unseen?
Hebu soma hii jagged statement ya muro>
Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS
Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenyeIMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidina "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatuaza AWALI za kushughulikia suala hili.

Halafu niambie nani anayefanya personal attack.

Mkuu ume adress all key points personal attack za muro kwa lissu
But kama hauko kimlengo wowote wa siasa ni dhahiri shahiri TL anataka kufanya TLS kuwa ya mlengo wa kisiasa badala ya majukumu yake halisi.

Kwenye sheria jamaa yuko vizuri tena sana tu but ukisikiliza maneno ambayo huwa anayotoa kwenye medias yaan ni bora hata yule bwege wa Lindi..anatoa maneno mepesi, yaliyojaa dharau na kebehi nyingi! Au huwa anajiona yeye ndio wakili msomi kuliko wote waliopo??


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni raia pekee aliyekamatwa akimiliki pingu na kuachiwa huru , ni nyoka lakini wa bei rahisi sana .
Haka ni ka informer na bei yake ni rahisi sana, bado hakajapata ajira kule. Kanapiga kelele ili kasikike.
 
Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*
Jerry Muro anatafuta kiki kwa pikipiki ......anapigwa chini kila anapo simama masikini
 
Jerry Muro ndio yule alikamatwaga kwa kula rushwa ya 10mil. au ni mwingine? Na ambaye alikuwa msemaji wa Yanga akafukuzwa!!?

ndio huyohuyo msema hovyo kaungana na mnafiki mwenzake wa itifaki na uenezi ili kuongeza nguvu
 
We have to discuss the above topic mkuu sio personality yake, mbona tunakosa maarifa kadri siku zinavyokwenda?
Put aside our political difference!

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa hiyo tundu lissu anayejadiliwa hapa ni nyani au? kwa maana hana utu si ndio? Halafu huyo mla rushwa ya mil 10 ndo ana utu kwa hiyo asijadiliwe.... poor u

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ume adress all key points personal attack za muro kwa lissu
But kama hauko kimlengo wowote wa siasa ni dhahiri shahiri TL anataka kufanya TLS kuwa ya mlengo wa kisiasa badala ya majukumu yake halisi.
Kwenye sheria jamaa yuko vizuri tena sana tu but ukisikiliza maneno ambayo huwa anayotoa kwenye medias yaan ni bora hata yule bwege wa Lindi..anatoa maneno mepesi, yaliyojaa dharau na kebehi nyingi! A
u huwa anajiona yeye ndio wakili msomi kuliko wote waliopo??


Sent using Jamii Forums mobile app



What does it take to be "mwanasheria msomi kuliko wote?' jinsi tu unavyotamka hilo neno it vividly depicts how arrogant
you are!!
 
Lissu amebadilika sana kutoka shujaa Wa kupinga ufisadi mpaka kufikia hatua hii ?! hawa IMMMA Si alishawahi kuwatuhumu wanahusika na ufisadi?! Lowassa amembadilisha sana Lissu kuna kitu Lissu amejifunza kuhusu kuropokaropoka na kuchafua watu pasi na ushahidi...kuna baadhi hawatanielewa hapa
 
Wew unayejua ndio maana nimekuuliza
One answer yes or not[emoji2] [emoji2]
Lissu atafanya vichaa waongezeke mitaani kwa hali hii
Lissu tuliza vijana wako wengi wameshajitoa ufahamu waliokua nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama vichaa wenyewe ni wa aina yangu basi kesheni mkiomba angalau nusu ya watanzania wawe vichaa!! Hakika mtatoka hapa mlipochimbiwa na kusogea mbele.
 
Back
Top Bottom