Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Kuna sehem jerry umeongea kishabiki na sio kiuhalisia. Tundu lissu alisema waliovamia hapo walivalia nguo za pollice. Ww unasema alisema ni police. Huon unapotosha makusud kwa malengo yako?? Taarifa ya police wenyewe wanakili kwamba walinzi walidanganywa na waharifu hao kwa kujiita police. Je wanaweza kudanganya kujiita police bila kuwa na utambulisho wowote wa pilice? Hii ina maana police wanaungana na Tundu Lissu . Sasa ww unaandika haya ukiyatoa wap?? Kuna mengine uko sawa lakn meng zaid hujajenga hoja zenye kufikirisha
 
OK tudiscuss contents ya alichoandika muro [emoji2] [emoji2] [emoji2] hapa naweza baki mwenyewe
Maana nyie ukweli kuhusu TL huwa hampendi kuusikia!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukweli ni upi? Ok! Let's go figure>kwenye hizo fikra za muro alizoziainisha hapo neno Lissu limejitokeza zaidi ya mara sita,huku neno 'Rais wa Tls' likionekana zaidi ya mara 16! Ambapo neno 'Rais wenu' lipo zaidi ya mara mbili!! Labda uniaminishe kuwa maneno hayo yanawalenga watu tofauti tofauti,or else how undoubtly can you(muros)jump the stunt of being coward personality attackers? Or move away stealth unseen?
Hebu soma hii jagged statement ya muro>

Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS
Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.

Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenyeIMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidina "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatuaza AWALI za kushughulikia suala hili.

Halafu niambie nani anayefanya personal attack.
 
Hapa ishu iko hivo, kwa wale wazee wa ufipa (chadema) hawatakuja na arguments yenye mashiko unless they will attack muro's personality! Hii ni kuonesha hawajakomaa kisiasa na wanamsujudia huyo lissu kama ndio msomi wa kwanza kutokea ndani ya CDM..that a big shame

Sent using Jamii Forums mobile app
hivi wewe huoni yeye ndio kaanza kuattack personality ya lisu,in fact,lengo la m-ccm huyu(muro) ni kumshambulialisu huku akisahau tamko si la lisu bali la tls.
halafu huyu akili yake ni ndogo mno
 
Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*
Ukuu wa wilaya unamsumbua,,kwa maoni yangu ndugu Murro na usomaji wake wa kupiga picha si stahihi ya wakili msomi kama Lissu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna asiyekujua ww muro kwa uropokaji tena mchumia tumbo ni kweli mwandishi lkn ni mtu unayetumia karam yako visivyo, unamatatizo au mbinafisi unatisha watu ili kupata vhochote hata hapo umegeuka msemaji ili ufikiriwe sisi c wa hivyo mkuu ni mambo mangapi yanatokea ya kikatiri wanafanyiwa watanzania umeyasemea?

Kama c lile la nape ulijitokeza ili umuokoe huyo mtekaji mwenzio aliyetishia kumpiga risasi nape?watu washaanza kukuelewa kuwa ni kati ya kikosi cha utekaji au kukaa kimya unazani wote wajinga?kuna viroba vilikutwa na maiti ndani yake je hilo hukuliona hata utumwe kusema haya?

Fanya yote lkn kumbuka kuna MUNGU jitafakali kwa maisha ya baadae na kizazi chako,ww ni kati ya waandishi hatari sana mrengaji ambaye muda c mrefu majibu utayashuhudia ipende tanzania ktk haki sio kinyume chake yeyote yule afuatirie nyendo za huyu mtu hakika ukweli ataushuhufia,muro c mwema kiasi hicho kama aliweza kumpga pingu mkrugenzi ili apate pesa baahati mbaya likabuma kwann asiwe kikosi cha yule kiongozi wa watekaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la Rushwa alisafishwa Kisheria hivyo hakuhusika nalo bali lilikuwa ni la ' Kichuki ' zaidi dhidi yake kutoka katika ' Mamlaka ' fulani nchini ambayo ilichukiwa Kitendo cha Muro kuwaonyesha wakichukuwa ' rushwa '. Kuhusu Yanga ambako alikuwa ni Msemaji wake wala hajafukuzwa kama ambavyo Wewe na wenzako wengine mnasema bali mkataba wake ulifikia mwisho na wakati huo huo Jerry Muro alikuwa ameshapata ' shavu ' jingine tena la maana huko SUMATRA ambako yupo hadi sasa ' akitiririka ' na ' kuserereka ' vyake tena kwa raha zake huku akila ' bata ' ambazo pengine angeendelea kuwa Yanga hadi leo angezisikia tu ' ndotoni '.

Mwisho ushauri wangu tu mzuri Kwako ili kuonyesha kwamba kweli Wewe ni Great Thinker wa JF basi siku zingine uwe unajikita katika ' mada ' husika iliyopo na siyo ' Kushadadia ' vitu vingine ambavyo vingepaswa ' vishadadiwe ' sana na akina Dada, Mama na Bibi zetu ila bahati mbaya sana ' vinashadadiwa ' na Dume zima. Unatutia mno wasiwasi Sisi ' Wadindaji ' wenzako Mkuu kama kweli Wewe ni mwenzetu.
Hata wewe zungumzia madhara na hayo ya huyo muro wako lkn kuwa makini sana na huyo muro wako nae utamuelewa tu yuko upande gani kwa kuwa hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muro yupi aliyekua msemaji wa yanga Anataka teuzi ya UDC
 
Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*
Well said, Jerry. Labda ungeongeza IMMA zamani ilikuwa IMMMA hadi Lawrence "M"asha alipoenda siasa Mwanza kaung'ata mkono uliokiwa unamlisha, akajikuta naye yuko deep sink CHADEMA. Ila hii ya IMMA kumtetea Tundulissu au Deep Green umeteleza - sioni kama kuna ubaya wowote; Wakili yuko huru kumtetea mtu yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muro kaandika pointi sana, ila kwa sababu kuna baadhi ya watu waliorogwa na mchawi pesa, utashangaa hawatamuelewa
 
Hata wale mawakili walio watetea ile meli ya samaki wa Magufuli walikuwa mawakili kutoka Tanzania..... Tundu Lisu kutetewa na IMMA ni ishu ya kawaida hiyo ndiyo kazi ya mawakili...

Bado sioni hiki kijipeperushi alicho kiandika Jerry Murro kina mashiko.....

NB upate kichwa kimoja cha Tundu Lissu kwa ulinganyo wa kichwa cha Jerry Murro ni sawa na vichwa 152 vya Jerry Murro kwa kichwa kimoja cha Tundu Lisu
 
Kwa kumbukumbu zangu na kama sikosei,Jerry Muro hata uvamizi wa Bashite clouds aliutetea hadharani.

Si hivyo tu,hata Manji alipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya alionekana kuunga mkono kukamatwa kwake pale alipohojiwa channel 10 katika kipindi cha Mada Moto.

Huyo ndio Jerry.

U-DC unatafutwa kupitia migongo ya watu.

Huwezi kufifisha hoja kwa kufanya character assassination ya kijinga hivyo..NI VIGUMU KUITENGANISHA TLS, TunduLisu na CHADEMA....Hapo wanasheria mmechemka
 
Back
Top Bottom