Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
8,294
8,855
Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*

UPDATES
29/08/2017

Kwa ufupi
  • Rais wa TLS Tundu Lissu, juzi alitangaza uamuzi wa baraza hilo kupinga kushambuliwa kwa ofisi ya mawakili wa kampuni ya Immma, akiwataka mawakili wote nchini kususia kwenda mahakamani leo na kesho.
  • Alisema baraza hilo limekubaliana kuwa mawakili wote nchini wasiende mahakamani ili kuonyesha kutokubaliana na shambulio hilo lililofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye ofisi hizo Mtaa wa Charambe, Upanga jijini Dar es Salaam.
By Waandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz


Dar/mikoani. Utekelezaji wa azimio la Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwamba leo na kesho wasusie kwenda mahakamani umewaweka njia panda mawakili.

Rais wa TLS Tundu Lissu, juzi alitangaza uamuzi wa baraza hilo kupinga kushambuliwa kwa ofisi ya mawakili wa kampuni ya Immma, akiwataka mawakili wote nchini kususia kwenda mahakamani leo na kesho.

Alisema baraza hilo limekubaliana kuwa mawakili wote nchini wasiende mahakamani ili kuonyesha kutokubaliana na shambulio hilo lililofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye ofisi hizo Mtaa wa Charambe, Upanga jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa milipuko iliyotumika katika shambulio hilo imetengenezwa kienyeji.

Mawakili 360 ambao ni wanachama wa TLS mkoani Arusha wanasubiri barua rasmi ya baraza la uongozi la chama hicho ili waitaarifu Mahakama kuhusu uamuzi wa kususia.

Mwenyekiti wa TLS Arusha, Elibariki Maeda alisema jana kuwa ni vigumu kususia kuanzia leo bila kupata barua rasmi ambayo itapelekwa mahakamani.

“Ingawa tunaungana na viongozi wetu kulaani tukio la kushambuliwa ofisi za mawakili wa Immma, lakini tukigoma tu kwenda mahakamani kesho (leo) bila kupeleka barua rasmi, kuna uwezekano wa kuathiri kesi za wateja, ikiwamo kufutwa,” alisema.

Maeda alisema kwa kuzingatia kuwa mawakili wengi ni wa kujitegemea na waajiri wao ni wateja, hivyo kabla ya kugoma wanahitaji kuwa na barua rasmi ambayo ndiyo itafikishwa mahakamani.

“Tumekuwa na vikao leo (jana) na kamati ya uongozi hapa Arusha, tumekubaliana kusubiri barua ya Kamati ya Utendaji (baraza la uongozi) ili tuisambaze kwa wanachama wetu na Mahakama,” alisema.

Wakili mwingine mwanachama wa TLS aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema suala la mgomo linaweza kuwa gumu kutokana na ukweli kuwa kufanya hivyo kutawaathiri wateja wao.

“Mimi siwezi kugoma bila kushauriana na mteja wangu, mfano kesho (leo) nina kesi ina miaka tisa mahakamani sasa nisipoenda ina maana tutapoteza haki ya mteja wangu,” alisema.

Mwenyekiti wa TLS Mwanza, Lenin Njau alisema kimsingi wanaunga mkono azimio hilo, ingawa utekelezaji unasalia kuwa utashi binafsi wa wakili mmojammoja.

“Ingawa kama taasisi tunaunga mkono azimio hilo, suala la kutokwenda mahakamani linabakia kuwa utashi wa mtu mmojammoja,” alisema Njau.

Alisema baadhi ya mawakili wanalaani shambulio hilo na kutaka Serikali na vyombo vya dola kushinikizwa kuharakisha uchunguzi bila kuhusisha mgomo wa kuhudhuria mahakamani na kwenye mabaraza.

Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Dodoma, Steven Kuwayawaya alisema wataendelea na shughuli zao kama kawaida kwa sababu hadi sasa hawajapokea taarifa rasmi. “Hatujapokea official documents (nyaraka rasmi) hadi sasa, kwa hiyo kesho (leo) sisi tutaendelea na shughuli zetu,” alisema.

Ripoti ya uchunguzi wa awali

Wakati wanasheria wakiwa njiapanda, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika alizungumza na waandishi wa habari jana na kusema uchunguzi wa awali wa tukio hilo umebaini kuwa milipuko iliyotumika katika shambulizi hilo imetengenezwa kienyeji.

Alisema siku ya tukio, wataalamu walikwenda eneo hilo na walijiridhisha kuwa milipuko hiyo haikutengenezwa viwandani.

Kitalika alisema Agosti 26, jeshi hilo lilibaini kuwa kati ya saa saba na saa nane usiku, watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi, walifika ofisi za Immma Advocates wakiwa na magari mawili na walijifanya kuwa askari polisi hivyo kuwarubuni na kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari na walikutwa eneo la Kawe wakiwa hawajitambui.

Alisema kundi lililobaki liliingia ndani ya ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusababisha uharibifu wa mali, jengo la ofisi na majengo ya jirani.

“Hawa watuhumiwa walijifanya kama ni polisi, hii ilikuwa ni mbinu waliyotumia kufanya uhalifu, hivyo nawaeleza wananchi kuwa walikuwa wahalifu kama wengine si askari kama inavyodaiwa,” alisema.

Kitalika alisema wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliofanya tukio hili na kujua dhamira yao ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

Pia, aliwataka waathirika wa tukio hilo na wananchi kwa jumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi, hivyo kuwataka wenye taarifa zinazoweza kuwasaidia katika kupeleleza waziwasilishe.

Rais wa TLS, Lissu akizungumza na waandishi wa habari juzi alidai wamepata taarifa kutoka kwa uongozi wa Immma Advocates kuwa kabla ya mlipuko huo polisi wakiwa na magari walifika kwenye ofisi hizo na kuzungumza na walinzi.

Alidai polisi waliwaeleza walinzi kuwa kuna mhalifu ambaye amewatoroka na kuruka uzio ili kuingia ndani ya ofisi hizo, hivyo walikuwa wanataka kuingia ili kumtafuta. Lissu alidai walipoingia, waliwakamata walinzi hao na kuwachoma sindano na baadaye mlipuko huo ukatokea.

Tamko Tume ya Haki za Binadamu

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa tamko kulaani shambulio hilo.

Taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Mwenyekiti wake, Bahame Nyanduga imesema imesikitishwa na kitendo hicho ambacho kinaashiria uhalifu wenye nia ya kutisha wanasheria wasitekeleze majukumu yao ya kisheria ya kutetea wateja wao.

“Tume inasisitiza kuwa dhana ya utawala bora inategemea utawala wa sheria ambao utaathirika iwapo wanasheria watatishwa na matukio kama ya kupigwa mabomu au vitendo vinginevyo vitakavyowanyima uhuru wa kufanya kazi zao,” inasema taarifa ya tume. Imelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakamilisha upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya sheria.

Pia, imeutaka uongozi wa TLS kusitisha tangazo la kuwataka mawakili kususia vikao vya Mahakama na mabaraza kwa siku mbili.

Imesema mgomo huo hautakuwa na maana kwa vile vyombo vya usalama vimeshaanza kufanya uchunguzi na kwamba utawaathiri zaidi wateja wao ambao hawahusiki na tukio hilo.

Imeandikwa na Mussa Juma, Godfrey Kimani, Jonathan Musa, Sharon Sauwa, Kelvin Matandiko na Pamela Chilongola.


Leo Tena
29/8/2017

*Breaking News*
Mawakili wanaofanya kazi zao Mkoa wa Dar es Salaam, Leo Jumanne 29/08/2017 *WAMEENDELEA* na kazi zao kama kawaida, *HOJA* yao kubwa wanasema *HAWANA* mkataba wa Kazi na *TUNDU LISSU,* wana mikataba ya kazi na *WATEJA* wao.

Hii ndio Dar es Salaam ya Mawakili Wasomi, na wanaojitambua na kutambua *HESHIMA* ya taalamu zao.

Ikiwaka *MULIKA,* ikizimika *PAPASA.*

Wakili Mtarajiwa
*Jerry C. Muro*
*Ubungo, Maziwa*
*Dar es Salaam.*
*29/08/2017*
 
Nyuzi zipo nyingi mno zenye jumbe tofauti or mawazo tofauti lakini wakilenga sehemu moja.... mf. uzi wa mpenda zoe juu ya Lisu na zingine kwa wakati ule...
 
Kwa kumbukumbu zangu na kama sikosei,Jerry Muro hata uvamizi wa Bashite clouds aliutetea hadharani.

Si hivyo tu,hata Manji alipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya alionekana kuunga mkono kukamatwa kwake pale alipohojiwa channel 10 katika kipindi cha Mada Moto.

Huyo ndio Jerry.

U-DC unatafutwa kupitia migongo ya watu.
 
kila mtu anapo kuwa na mawazo yake yasijumuishwe kuwa ni mawazo ya wote... au kuya fananisha kwakuwa kila mtu kachambua kivyake... au kajieleza kivyake...

wewe ukiulizwa jina na yule hivyo hivyo... mtataja jina moja kuwa JUMA ABDUL... swali laweza kuwa moja majibu ni tofauti... na ndio maana kuna nyuzi za kilimo lakini kila mtu kaelezea yeye kwa namna yake
 
Jerry Muro hata uvamizi wa Bashite clouds aliutetea hadharani.

Si hivyo tu,hata Manji alipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya alionekana kuunga mkono kukamatwa kwake pale alipohojiwa channel 10 katika kipindi cha Mada Moto.

Huyo ndio Jerry.
Huyu ni raia pekee aliyekamatwa akimiliki pingu na kuachiwa huru , ni nyoka lakini wa bei rahisi sana .
 
Tuangalie tukio lenyewe na upana wa athari zake. Uvamizi wa mabomu/mass killing ni mfumo unaotumiwa na ma terrorist. Hapa kwetu Tanganyika, tunakumbuka ubalozi wa marekani ulivyoshambuliwa kwa mabomu na tuliona jinsi serikali ilivyolishughulikia suala lile. Mh Muro, naomba utuambie kwanini serikali hasa waziri wa sheria au mambo ya ndani wameshindwa kutoa tamko lolote?
 
Kuwa na hoja nzuri ni swala moja, ila kuiwakilisha mbele ya jamii na ikaekeweka ni swala jingine.

Naamini hii hoja ungempa akuandikie Mm Mwanakijiji au yule Malota ingekuwa yenye mvuto na mtiririko wa kuvutia....

Hata hivyo hoja yako imeeleweka.
 
Back
Top Bottom