JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameulizwa kama Serikali imeshakamilisha malipo ya kiinua mgogo chake alichokuwa anadai, majibu yake ni haya:
“Nilikuwa nadai kiinua mgogo cha miezi 44 niliyokuwa Bungeni, nimelipwa kiinua mgongo cha miezi 20 bado cha miezi 24.
“Nilikuwa nadai fidia ya fedha zote nilizotumia kwenye matibabu baada ya kushambuliwa Septemba 7, 2017, hizo sijalipwa. Nimezidai kwa kuwa Sheria ya uendeshaji wa Bunge inasema Mbunge akiugua akiwa kazini anapwa kulipiwa gharama ya matibabu yake, sijaomba kitu ambacho kipo nje ya sheria.
“Niambiwa niandike barua, nimefanya hivyo na nimeambatanisha na risiti zote nikizotumia kuanzia Nairobi hadi Ubelgiji.
“Katika matibabu yangu kuna fedha ambazo zililipwa na Chama, kuhusu fedha nilizochangiwa na watu mbalimbali wakati wa matibabu kama nikilipwa zitakuwa zangu kwa kuwa nazihitaji.
“Miaka takribani minne nimekaa hospitali, maumivu yote yale, ndio maana Sheria inasema niliowe hizo fedha ili ziweze kunisaidia kwa mambo mbalimbali.
“Pia hao waliochanga hawajaniambia niwarudishie, hawakunikopesha, walinisaidia kwa sababu Serikali ilitaka nife nisipate msaada.”
Chanzo: Edwin Odemba