Tundu Lissu: Nitarejea Tanzania iwapo nitaruhusiwa kuanika ‘Maovu’ ya Utawala wa Magufuli

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,551
2,000
Tundu Lissu Asema Atarejea Tanzania Iwapo Ataruhusiwa Kuanika ‘Maovu’ Ya Utawala Wa Magufuli

NA WANGU KANURI

MwanasiasaA mtajika wa Tanzania na mpinzani wa chama cha CHADEMA, Bw Tundu Antiphas Mughwai Lissu hivi sasa amesema kuwa yupo tayari kurejea nchini Tanzania lakini kwa sharti moja kuwa, kurejea kwake kutalingana na kama serikali ya Tanzania ipo tayari kuyaorodhesha ‘maovu’ yaliyofanywa chini ya uongozi wa marehemu John Pombe Magufuli.

Mpinzani huyu yupo katika nchi ya Ubelgiji ambako alihamia baada ya kupinga matokeo ya kura ya uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo alisema yalikuwa ghushi na yalikiuka demokrasia.

Bw Lissu alisafirishwa hadi kituo cha ndege na ubalozi wa Amerika, Ujerumani na hatimaye kufika Ubelgiji mafichoni. Itakumbukwa kuwa Bw Lissu aliponea mauaji ya mwaka 2017 na akarejea nchini Tanzania mwaka jana ili kutilia shaka na kukataa ushindi wa mara ya pili wa rais John Magufuli.

“Nimezipokea habari kuhusu kifo cha rais Magufuli lakini hazijanitamausha kwani nilitarajia kifo chake baada ya kuandika kwenye ukurasa wangu wa Twitter nikiuliza yuko wapi rais Magufuli na hali yake ya afya iko vipi, tarehe 7 mwezi Machi, 2021? Wakati huo ambao niliuliza, nilikuwa nimepokea ujumbe kuhusiana na hali yake ya afya huku nikielezwa kuwa alikuwa ameupata ugonjwa wa Covid-19 na alikuwa mgonjwa sana.

“Kwa hivyo, habari za leo hazijanijia kwa mshtuko ila jambo ambalo linanishangaza ni kuwa serikali ya Tanzania inazidi kudanganya hata sasa akiwa amefariki. Magufuli amefariki kwa sababu ya corona. Pili, Magufuli hajaaga jana usiku lakini aliaga Jumatano ya wiki jana. Isitoshe, kifo chake kinakuja baada ya mapuuza yake ya ugonjwa wa Covid-19 na kutovaa maski huku akiamini dawa za miti shamba na kutupilia mbali ripoti za kisayansi kuhusiana na ugonjwa huu,” akasema Tundu Lissu.

Ujumbe wake kwa Watanzania ulionyesha maono mapya haswa sasa ambapo rais Magufuli amefariki.

“Ni fursa ya kufungua ukurasa upya katika nchi ya Tanzania. Tunahitaji mwanzo mpya. Tunahitaji kujenga nchi yenye udemokrasia, nchi inayoheshimu haki za kimsingi za binadamu na utawala wa sheria.

“Tunahitaji kujenga mfumo wa kisiasa ambao unawashutumu viongozi wasiowajibika kwani hatujakuwa na fursa hii kwa miaka tano iliyopita chini ya uongozi wa rais Magufuli. Hivi sasa sababu amefariki, ni wakati wa Tanzania kuurejesha urazini wake na kuchukua fursa hii kwa moyo mkunjufu,” akaongezea Bw Lissu.

Isitoshe, alisema kuwa Bi Samia Suluhu ataweza kumudu Tanzania kwani alipokuwa akifanya kazi na makamu huyu wa rais, Bi Suluhu alikuwa mtu tofauti sana na rais Magufuli.

Alieleza kuwa japo Bi Suluhu alisikiza na kupokea ukosoaji kwa njia nzuri, marehemu rais Magufuli aliyachukulia makosaji haya kibinafsi na kamwe hakuyavumilia.

Kwa mtazamo wake Bw Lissu, Bi Suluhu ataongoza nchi ya Tanzania kwa utofauti iwapo atasitisha sera za kupotosha na kuwagandamiza watu alizoweka rais Magufuli na kuanzia mkondo mpya kwa kuwaita wapinzani kama yeye na wale wengine waliofurushwa na kufungwa gerezani na rais Magufuli.

Vile vile Bi Samia ana kazi nyingi ya kurekebisha uovu aliofanya rais Magufuli ndani ya nchi ya Tanzania na hata katika mahusiano ya Tanzania na mataifa jirani.

Hali kadhalika, Bw Lissu alisema kuwa ataiandika barua kwa umma kuhusiana na mwelekeo wake na wa wenzake ili kutoa mwanga katika mambo ya kisiasa.

“Hatuwezi kuendelea na ‘Umagufuli’ bila Magufuli. Hii inamaanisha kuwa taifa sharti libadilike. Katiba lazima iangazwe upya kwani ilihujumiwa na rais Magufuli tangu mwaka wa 2014.

“Isitoshe, waliofungwa kwa sababu ya nafasi zao za kisiasa waachiliwe huru, waliofurushwa kutoka nchi ya Tanzania warejeshwe na tukomeshe unyanyasaji wa haki za kibinadamu ambao ulikuwa kielelezo cha uongozi wa rais Magufuli. Tuweke huru vyombo vyetu vya habari na vyama vingine vya kisiasa,” akasema Bw Lissu.

Matamshi yake Bw Lissu yaliibua hisia mseto huku akikashifiwa na kupongezwa kwa usawa.

“Hutawahi ongoza Tanzania, Bw Tundu. Kusherehekea kifo cha mtu si jambo la Kiafrika. Mbona mna tamaa ya kutufanya tuamini kuwa alifariki sababu ya Covid-19?” akauliza @aamutambara.

“Bw Lissu anazungumza kana kwamba anasherehekea kifo chake rais Magufuli. Mtu amweleze Bw Lissu kuwa tamaduni yetu haituruhusu kusherehekea kifo cha mtu,” akasema @CShitiabai.

“Utamaduni wa Kiafrika hauturuhusu kusherehekea kifo cha mmoja wetu hata ingawa yeye ni adui. Bw Tundu Lissu sharti ajue hivyo,” akaeleza @Danmusyoka7.

“Ningekuwa ninasherehekea iwapo ningekuwa Bw Tundu. Fikiria kuhusu mtu aliyeamuru ufyatuliwe risasi nyingi zinazofuatana mtawalia kana kwamba wewe si mwanadamu? Ingekuwa mimi ningekuwa napiga sherehe sasa,” akaandika @taller056.

“Ninasimama naye Bw Tundu Lissu. Ikiwa ungenifyatulia risasi milioni mwilini, ningekukujia kwa kila kitu nilicho nacho. Mtu hujichumia heshima, si kuamrisha watu wakuheshimu. Kauli hii inaandamana na kutaka neema kwa watu,” akasema @gabrieloguda.

“Ndugu yangu Bw Tundu Lissu, risasi 16 hazingekuua sababu Mungu alitaka ujionee kifo cha mtu ambaye alitaka kukuua. Hatusherehekei kifo chake, lakini kwa kila jambo unalolifanya kuna matokeo. Ukimtamkia mwenzako mabaya, yatakupata wewe,” akahitimisha @TonyMureithi

“Bw Tundu Lissu alikuwa na uhakika kuwa rais Magufuli hayupo tena. Alipokuwa akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter alifanya hivyo akiwa amejiamini sana. Kile tu alitaka ni hakikisho kupitia tangazo rasmi,” akaandika @iamjoseh_
Habari Zinazohusiana Na Hii
 

kimbendengu

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,483
2,000
CCM wote ni wanafiki amekufa Mzee Nyerere waliomboleza mwezi mzima lakini kilichofuatia ni kuiba juu ya kuiba, ufisadi juu ya ufisadi huko Butiama ukiondoa kaburi la Nyerere kitu gani kimeendelezwa?

Madini yote mnagawana na ndugu zenu, leo kwenye maradio, tv, magazeti yameandikwa mpakaaaa lakini hakuna kitakachoendelea ,bado mnataka tumpende mwendazake kwa lipi?

Leo hii mtandao wa Twitter umefungwa ili mradi watu wasijadili mambo ya nchi yao! Huyo marehemu Joni tutampenda kwa lipi? Tuachieni mitandao yetu.
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,763
2,000
Serikali ya mama Samia haiwezi kukubali upumbavu wake
Hakuna kipindi kibaya kwa Serikali ya CCM kama kipindi hiki. Hofu kwa Watendaji wa Serikali imetoweka ghafla. Ni kipindi cha kila kundi kulipiza kisasi kwa wabaya wao. Makundi hayo ni
1.CCM Asili
2.CCM Mtandao
3.CCM Mpya.

Wakati huo huo ni furaha kwa Wapinzani kwani hakutukuwepo na kundi litakalokuwa na nguvu ya kupambana nao moja kwa moja.

CCM kuna uwezekano mkubwa kutofika 2025 wakiwa wamoja. Hii ni kutokana na misimamo ya kila kundi.
 

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,655
2,000
Lissu yaliyopita si ndwele. Sasa hata ukimuanika kishakufa. Haitasaidia. Najiuliza hivi wizara ya Elimu itaendelea na mchakato wake wa Somo la Historia ?
Mchakato ulishaanza sidhani kama watasitisha, ila tujiulize hiyo Historia ina umuhimu gani?
Nje ya maada juzi kati ulisema mzee yuko sawa na atarudi tuu naona imekua kama yule aliyesema akiwa msikitini kwamba tunasalimiwa na mzee na tuchape kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom