Tundu Lissu: Nitarejea Tanzania iwapo nitaruhusiwa kuanika ‘Maovu’ ya Utawala wa Magufuli

Lissu yaliyopita si ndwele. Sasa hata ukimuanika kishakufa. Haitasaidia. Najiuliza hivi wizara ya Elimu itaendelea na mchakato wake wa Somo la Historia ?
Itasaidia sana. Itaweka kumbukumbu ili wengine wasije kurudia. Huu tunaita utamaduni wa kiafrika eti marehemu hasemwi unatocost sana. Kila siku tunarudia makosa yaliyofanywa na babu zetu kisa tunakataa kukiri kuwa walikosea. Makosa ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Magufuli yakiwekwa wazi na tukajifunza hatuwezi kuyarudia na tutakuwa tunapiga hatua badala ya mark time
 
Mimi sina ushabiki wa vyama akae yeyote yule najionea sawa tu alimradi tu mambo yaende ila lisu kuna huo mstari wa haki za kibinadamu anapenda sana kuurudia rudia najua zipo haki nyingi tu za kibinadamu kinachonitisha ukaribu wake mkubwa na wazungu hawezi kuruhusu ushoga kweli huyu km tunampa nchi? Kooote namuelewa hapo tu kdg napata wasiwasi
 
Lissu,
Kukaa kimya kipindi hiki kutakutofautisha kitabia na unayemshutumu, vinginevyo watu watashindwa kuwatofautisha kwa hulka na kudhani unaendekeza kisasi na mtu asiyekuwepo.
Kaa utulie sabiri wamalize yao utakuwa na uwanja mpana wa kusema mpaka utachoka.
 
Hakuna kipindi kibaya kwa Serikali ya CCM kama kipindi hiki. Hofu kwa Watendaji wa Serikali imetoweka ghafla. Ni kipindi cha kila kundi kulipiza kisasi wa wabaya wao. Makundi hayo ni
1.CCM Asili
2.CCM Mtandao
3.CCM Mpya.

Wakati huo huo ni furaha kwa Wapinzani kwani hakutukuwepo na kundi litakalokuwa na nguvu ya kupambana nao moja kwa moja.

CCM kuna uwezekano mkubwa kutofika 2025 wakiwa wamoja. Hii ni kutokana ba misimamo ya kila kundi.
N kweli lkn CCM ni ile ile hakuna punguzo lolote, walikuwepo wengi wakapita na watakuja wengi na watapita
 
Kwa hatua aliofikia Lissu sidhani kama ni mzalendo wa kuikabidhi nchi kuiongozaa, Maana mzalendo wa kweli hawezi kuihujumu nchi au kuipotray in a negative ways ili kumkomoa mtu mmoja ambaye yupo madarakani, ni wazi kabisa Yuko na personal interests au kuna kitu he gains for being "Western kibaraka".

Ajipange vizuri kama anahitaji uongozi ,akija na hizo kashfa na madhalilisho kuhusu taifa letu si tutamchukulia kama wahujumu uchumi wengine au Simba alieingia zizini na ngozi ya kondoo ,we won't trust him Ajipange na sera pevu na hekima ya ushawishi wa kuleta positive changes na sio kuja na package ya mirija for Western to get what they want kwa kumtumia yeye.Europens are not fools to take care of him kwa kipindi chote hicho there must be some "bogus contracts "amefanya nao ili kuwalipa fadhira, tuko macho na tunamsubiri aje na hizo sera zake.
 
Lissu yaliyopita si ndwele. Sasa hata ukimuanika kishakufa. Haitasaidia. Najiuliza hivi wizara ya Elimu itaendelea na mchakato wake wa Somo la Historia ?
Angalizo zuri sana!
Hii nafikiri imekutana na "natural death"
 
Haya yote ya nini? Bwana mdogo atumie busara na hekma la sivyo atajidhalilisha, mbona hukuyasema kabla? Sio wakati wa kupandikiza chuki, kumbuka marehemu ameacha familia, ndugu, jamaa, marafiki na wafuasi kibao..... sidhani Kama Kuna serikali ya kuoza itakayo kubali huo utopolo wako bwana Lissu.
 
Huyu atulie tumemchoka sasa! Marehemu astiriwe hakuna Kiki ya marehemu ajipange upya tuu
 
CCM wote ni wanafiki amekufa Mzee Nyerere waliomboleza mwezi mzima lakini kilichofuatia ni kuiba juu ya kuiba,ufisadi juu ya ufisadi huko butiama ukiondoa kaburi la Nyerere kitu gani kimeendelezwa?

Madini yote mnagawana na ndugu zenu,leo kwenye maradio,tv ,magazeti yameandikwa mpakaaaa lakini hakuna kitakacho endelea ,bado mnataka tumpende mwendazake kwa lipi?

Leo hii mtandao wa twitter umefungwa ili mradi watu wasijadili mambo ya nchi yao !huyo marehemu Joni tutampenda kwa lipi?Tuachieni mitandao yetu
Wanalazimisha tumpende

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uhuru anaoutaka ulikwepo kipindi Fulani ivi ila haukutufikisha popote zaidi ya kila kukicha huyu kapiga uku yule kapiga kule.
 
Hakuna kipindi kibaya kwa Serikali ya CCM kama kipindi hiki. Hofu kwa Watendaji wa Serikali imetoweka ghafla. Ni kipindi cha kila kundi kulipiza kisasi kwa wabaya wao. Makundi hayo ni
1.CCM Asili
2.CCM Mtandao
3.CCM Mpya.

Wakati huo huo ni furaha kwa Wapinzani kwani hakutukuwepo na kundi litakalokuwa na nguvu ya kupambana nao moja kwa moja.

CCM kuna uwezekano mkubwa kutofika 2025 wakiwa wamoja. Hii ni kutokana na misimamo ya kila kundi.
Bado pia Ni hisia zako tu, CCM Ni Ile Ile.
 
Back
Top Bottom