Tundu Lissu: Ngeleja amelidanganya bunge

Wasiwasi ushaidi ukikamilika atamuambia auwasilishe kwa njia ya maandishi halafu ata upotezea kama alivyofanya kwa Pinda. Pinda alidanganya na yeyote aliyesoma ule ushahidi wa lema anajua. Makinda anawalinda mawaziri wa chama chake lakini ajue kuwa itamtokea puani siku moja yeye na chama chake. Watanzania wameamka na wanajua nyeusi na nyeupe.
 
Huo ni mwanzo tu tutaona mengi. Lisu shikilia hapo hapo mpaka kieleweke
 
Swala la Arusha, sijui kama wataweza kupotezea hata kama miaka 10 itapita sana sana watachelewesha tu....
 
Mh. Tundu Lissu amemwuliza Ngeleja kuhusu kampuni ya madini ambayo imechukua maeneo ya wakazi wa Singida Mashariki bila fidia na kujenga kiwanja cha ndege kwenye mashamba ya wananchi.

Na akamwuliza kwanini serikali haijachukua hatua ikiwemo kuwafungulia mashtaka hao wawekezaji. Ngeleja amekanusha na kusema kampuni imemilikishwa kisheria.

Lissu ameomba mwongozo na kutaja kifungu kinachohusu kudanganya bungeni na kusema waziri amedanganya. Kama kawaida Anne Makinda amemwambia akafanye uchunguzi alete huo uongo bungeni.

Hapa patamu ngoja tuone au wataizima kama ile ya Lema.

Unajua shida hapa si waziri ila mkuu wa kaya kawazoeza hawa mawaziri kujibu bila taarifa sahihi, hushangai mkuu wa kaya analalamika kwenye media badala ya kutekeleza wananchi waone vitendo tu??

Umewahi kuona wapi amiri jeshi mkuu analalamika kwamba vikosi haviwahi mazoezini, viytani nk bila kuchukua hatua!
 
Watabana sn, mwsho wa cku itabd wanyoshe mikono. Wameligeuza bunge ni mali ya CCM, Huyu spika anapnda kuwabana wbnge wa Cdm, angekuwa ni wa Ccm kasema wazr kadnganya wla acngeambiwa athbtshe! Kwnza hakn mwny ubav wa kumsema wazr! Wanalindana!

Sweetlady,

Huyo spika anajua kilichomfikisha pale.Kama kawaida wakileta mchezo Bungeni tunarudi kwa wananchi,tutacheza michezo yote.Wabaki kuipa majina tu,michezo hatarishi,uchochezi,treason,nk.

CCM ni weak,kuna watu wamewka taaluma yao nyuma ya kivuli cha ushabiki na uzandiki.CHADEMA tuendelee kuwa Aggressive,itapendeza sana kuanzia 2015 CCM watakapokuwa chama cha Upinzani.Uwezo wa kuwaweka benchi tunao na hatuzuiliki tena
 
wamekutana wote ni wanasheria lakini kwa uwezo Lissu ni kama tingatinga na ngeleja ni kama bajaj au mshono (boda boda)(pikipiki)
 
Mh. Tundu Lissu amemwuliza Ngeleja kuhusu kampuni ya madini ambayo imechukua maeneo ya wakazi wa Singida Mashariki bila fidia na kujenga kiwanja cha ndege kwenye mashamba ya wananchi.

Na akamwuliza kwanini serikali haijachukua hatua ikiwemo kuwafungulia mashtaka hao wawekezaji. Ngeleja amekanusha na kusema kampuni imemilikishwa kisheria.

Lissu ameomba mwongozo na kutaja kifungu kinachohusu kudanganya bungeni na kusema waziri amedanganya. Kama kawaida Anne Makinda amemwambia akafanye uchunguzi alete huo uongo bungeni.

Hapa patamu ngoja tuone au wataizima kama ile ya Lema.

Sasa mbona uongo ukithibitishwa yule anayedanganya hachukuliwi hatua kwa mujibu wa kanuni za bunge? Au hatu zitachukuliwa pale tu itakaposhindikana kuthibitisha?
Picha lingine hili, tusubiri tuone.
 
Ngeleja kwa Lisu kama Yanga kakutana na Aston villa patachimbika labda spika aizime. LISSU LAZIMA AWAPIGANIE WAPIGA KURA WAKE KWA GHARAMA YOYOTE ILE. Af nawashauri mawaziri wa ccm wakiulizwa swali waangalie nani kauliza sio kupurumuka kujibu wabunge wengine ni wafuatiliaji sio kama hao wenzao wa ccm wanaopiga weza siku inaisha lazima wajipange.

Simba na Tout Puisant Mazembe Englebert.
 
Kitaeleweka tu kwani CCM wamezoea kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu ni tabia yao lakini itafika mwisho kwa aibu
 
Raha na utamu ungekuwepo sana kama Mzee Six angekuwa spika. Huyu mama amekosa kasi na viwango matokeo yake sisi wengine hautuambii tena habari ya kusikiliza bunge. Thanx JK kwa kutujuza... Mzee 6 angemuacha waziri ahangaike na zigo lake la uongo lakini huyu mama pandikizi la EL anaingilia kati kila kitu na kufanya bunge liwe kama kikao cha serikali ya kijiji. Aache watu walumbane kwa hoja na sio kuruhusu bunge kuwa gulio la mawaziri kudanganya. Mwenzie Pinda anajuta.
 
Garbage in garbage out!! I never take Ngeleja seriously. "Mgao utakuwa historia!" kesho yake ukapitishwa mgao giza totoro! "Dowans lazima ilipwe" wabunge wenzie (CCM) wakasema stop. Boys will always be boys.
 
Bado Celina Kombani naona nae ameanza kuruba kazi anayo. Ngoja huo mjadala wa katiba uanze tutaona mengi.
 
Tatizo hapa sio kwa Mh. Lisu kuleta ushahidi, atauleta tu. Tatizo ni hatua zitazochuliwa baada ya hapo. Mmesahau alipoambiwa Mh. Lema apeleke ushahidi wa "UONGO" wa Pinda? Baada ya Mh. Lema kutoa ushahidi 10 wa uongo wa Pinda ilikuwaje? Wanalindana hawa na hakutakuwa na mabadiliko yoyote hadi tumewatoa.
 
Mh. Tundu Lissu amemwuliza Ngeleja kuhusu kampuni ya madini ambayo imechukua maeneo ya wakazi wa Singida Mashariki bila fidia na kujenga kiwanja cha ndege kwenye mashamba ya wananchi.

Na akamwuliza kwanini serikali haijachukua hatua ikiwemo kuwafungulia mashtaka hao wawekezaji. Ngeleja amekanusha na kusema kampuni imemilikishwa kisheria.

Lissu ameomba mwongozo na kutaja kifungu kinachohusu kudanganya bungeni na kusema waziri amedanganya. Kama kawaida Anne Makinda amemwambia akafanye uchunguzi alete huo uongo bungeni.

Hapa patamu ngoja tuone au wataizima kama ile ya Lema.

Hapa anayetakiwa kuleta udhibitisho,kwa muono wangu ni ngereja.Alete documents zinazoonyesha kuwa hii kampuni imemilikishwa hilo eneo kihalali/kisheria.Sasa sijuhi huyu Lissu atakuja na nini!!! Picha za uwanja wa ndege?au ataleta nini? sielewi hapo.
 
Mh. Tundu Lissu amemwuliza Ngeleja kuhusu kampuni ya madini ambayo imechukua maeneo ya wakazi wa Singida Mashariki bila fidia na kujenga kiwanja cha ndege kwenye mashamba ya wananchi.

Na akamwuliza kwanini serikali haijachukua hatua ikiwemo kuwafungulia mashtaka hao wawekezaji. Ngeleja amekanusha na kusema kampuni imemilikishwa kisheria.

Lissu ameomba mwongozo na kutaja kifungu kinachohusu kudanganya bungeni na kusema waziri amedanganya. Kama kawaida Anne Makinda amemwambia akafanye uchunguzi alete huo uongo bungeni.

Hapa patamu ngoja tuone au wataizima kama ile ya Lema.

Inaelekea uwongo unakuwa kama mazoea sasa nchini. Angalia kwenye hotuba ya Rais ya kufungua mwaka aliahidi watanzania wote kuwa ataipatia Tanzania Katiba mpya; katika kuanza utekelezaji waziri mwenye dhamana na mwanasheria wa serikali wakaja na version yao ya kwamba hawaoni sababu ya katiba mpya; jamii ikaja juu. Serikali ikajifanya kama vile imekubali kusikia kilio mara hii umekuja muswada wana fanya constitutional review badala ya kuunda katiba mpya. Sasa hapo sijui nani anasema kweli ahadi ya rais au matendo ya mawaziri wake? Ni mfano mbaya kwa viongozi kutokua straight and clear kwenye mambo yanayogusa maisha ya watu hii tu inaondoa uhalali wa wao kuaminiwa na raia wa kawaida kwasababu kila mara wana pindisha mambo hasa pale maslahi ya kundi fulani la jamii yanapoguswa.
 
Back
Top Bottom