Tundu Lissu: Ngeleja amelidanganya bunge

Kwa mujibu wa hii ya leo, inadhihirisa kwamba, siku zote Mjengoni Mawaziri wamekua wakitoa majibu na maelezo ya uhongo kwa jua kwamba wananchi na wabunge hawajui kinachoendelea, imefika hatua sasa siri zimeanza kubumburuka na huu mpango wa kuwa na vyama (upinzani) matunda yake ndo haya, hakuna hatakaye kubali kudanganyika katika karne hii.

Ngereja amesema alitembelea sehemu husika kwa mara ya mwisho ilikuwa 2007 leo hii anatoa majibu kana kwamba hiyo sehemu ana ukaribu nayo; ni Hatari ktk maendeleo ya Nchi.

Tundu Lissu usife moyo endelea kupambana wengi tuko nyuma yako.
 
Hapa anayetakiwa kuleta udhibitisho,kwa muono wangu ni ngereja.Alete documents zinazoonyesha kuwa hii kampuni imemilikishwa hilo eneo kihalali/kisheria.Sasa sijuhi huyu Lissu atakuja na nini!!! Picha za uwanja wa ndege?au ataleta nini? sielewi hapo.

lisu atapeleka ushahidi wa umiliki wa wananchi,..i dont know for sure,.may be some sort of hati miliki ya kijiji,..hao majambazi wanaweza kutengeneza hati za kufoji kwa msaada wa ngeleja na tibaijuka,..speakin of tibaijuka,..ile kasi yake ya uongo imeishia wapi??viwanja vingapi ni vya wazi amevirudisha??
 
Hapa anayetakiwa kuleta udhibitisho,kwa muono wangu ni ngereja.Alete documents zinazoonyesha kuwa hii kampuni imemilikishwa hilo eneo kihalali/kisheria.Sasa sijuhi huyu Lissu atakuja na nini!!! Picha za uwanja wa ndege?au ataleta nini? sielewi hapo.

Nakuunga mkono kabisa ila huyu mama anauwezo mdogo wa kufikiria kwani Tundu Lisu anachodai ni Ngeleji alete utetezi wake lakini huyu spika anamgeukia Tundu Lisu ndio alete.
Hili bunge la mwaka huu tutaona vioja vingi sana.
 
Nimefatilia huyu speaker baada ya bwana.Mkosamali kutaka utaratibu wa speaker iwapo waziri anaulizwa swali la wilaya fulani naye anajibu wilaya nyingine tofauti, Makinda :waziri atakujibu. MAkofi bungeni na kejeri nyingi
 
Jamani hilo sio jambo la kutafuta, Binafsi ni mhanga wa hao SHANTA GOLD MINE hapa kijijini kwetu mang'onyi, niko tayari kutoa ushirikiano wowote kwa mhe. Lissu aje hata sashivi.
 
Wanajanvi tafadhali nielimisheni kwani kanuni za BUNGE zinasema nini juu ya adhabu stahiki kwa yeyote atakayeliongopea BUNGE?
 
Mi nadhan alternative ya spika kwamba mwongozo sio lazima papohapo ni nzuri. Inampa muda anayetuhumu muda kidogo wa kutafakari na kubana vizuri. Mawaziri wamezoea kujibu hovyo sijui ni kiburi, mazoea au ulevi. Wakati umefika kuwawajibisha inapothibitika. Wabunge wa ccm waache ushabiki maana hata wao wana maswali yao na wakiendekeza watajikuta swali la Namtumbo linajibiwa kama la Karagwe! Cdm komaeni nao hadi kieleweke!
 
Jamani hilo sio jambo la kutafuta, Binafsi ni mhanga wa hao SHANTA GOLD MINE hapa kijijini kwetu mang'onyi, niko tayari kutoa ushirikiano wowote kwa mhe. Lissu aje hata sashivi.

nenda kwenye ofisi ya chadema iliyo karibu nawe, watakuunganisha na Lissu umweleze ulivyoadhirika. Nadhani utakuwa ni ushahidi mzuri na ataweza kuwasaidieni.
 
Mh. Tundu Lissu amemwuliza Ngeleja kuhusu kampuni ya madini ambayo imechukua maeneo ya wakazi wa Singida Mashariki bila fidia na kujenga kiwanja cha ndege kwenye mashamba ya wananchi.

Na akamwuliza kwanini serikali haijachukua hatua ikiwemo kuwafungulia mashtaka hao wawekezaji. Ngeleja amekanusha na kusema kampuni imemilikishwa kisheria.

Lissu ameomba mwongozo na kutaja kifungu kinachohusu kudanganya bungeni na kusema waziri amedanganya. Kama kawaida Anne Makinda amemwambia akafanye uchunguzi alete huo uongo bungeni.

Hapa patamu ngoja tuone au wataizima kama ile ya Lema.

----------------------------
Jamani, tunateseka bure kusubiria msonobari uzae maembe, utakufa pasi na kupata matunda unayolenga!

Kwa maoni na dhamira yangu, Ngeleja alitakiwa hata asithubutu kujibu swali lolote linalohusu Wizara ya Madini na Nishati maana ni kati ya Mawaziri - robot, ambao ni kama vile 'wanabonyezwa kwanza' ndio sauti inatoka kuelezea jambo lililo ktk mjadala, iwe anajibu ukweli au uwongo hiyo ni hatua ya pili. Ngeleja kimsingi hana majibu yoyote yanayoweza kujibu hoja au maswali ya umma wa kawaida, sembuse ya wabunge ambao wanazo data za msingi.

Tukumbue alivyokuwa mdhoofu kuelezea suala la Dowans - ambalo boss wake wa zamani (ambaye pia ndiye boss wa sasa indirectly) alikuwa 'anabonyeza tu button' kuwa aseme wamiliki feki au la! Tusisahau kuwa hata huko Machimbo ya Singida, huyu 'boss wake' kama akiamua Ngeleja ataongea au la. Atasema kukanusha, au uongo au lolote! Nani wa kuumwajibisha? Nani wa kuufumua ukweli na kuulinda? Ni Spika? Yupi huyo? Hapo bungeni ni vituko tu vitaendelea, kwani sisi tunatarajia la maana? Makinda anajua analofanya na msishangae maana waliomtoa Sitta, walijua mambo kama hayo mtayauliza na matokea walishayatabiri, ndio maana Makinda ndio mtendaji wao.
 
Wanajanvi tafadhali nielimisheni kwani kanuni za BUNGE zinasema nini juu ya adhabu stahiki kwa yeyote atakayeliongopea BUNGE?

kanuni zinasema mbunge akishindwa kudhibitisha aliyoyasema bungeni atatakiwa kukanusha aliyoyasema bungeni. Asipofanya hivyo, mbunge yeyote anaweza kutoa hoja ya kulitaka bunge limwadhibu kwa kumsimamisha kuhudhuria baadhi ya vikao vya bunge.
 
Jamani hilo sio jambo la kutafuta, Binafsi ni mhanga wa hao SHANTA GOLD MINE hapa kijijini kwetu mang'onyi, niko tayari kutoa ushirikiano wowote kwa mhe. Lissu aje hata sashivi.

Twambie hali halisi iko je?
 
Najiivunia kuwa mwana Singida mashariki na kumpigia kampeni mh Lissu mpaka akawa muwakilishi wetu.....Lissu pambana kaka..tuko pamoja....Njaghamba iuhoma ilolo aghwida!
 
Lissu ni sawa na wabunge 50 wa ccm tena wale nafuu nfuu nafuu akiwamo sitta, mwakyembe, mwandosya, achana na wanaopewa ubunge kwa kugawa utamu.
 
Tatizo huyo mama anna, anawafanyia kazi ccm, akiletewa ushahidi atatupotezea tuu kama ya lema...ni bora hata akaweka wazi ushahidi wake kwa njia ya vyombo vya habari na siyo kuuwasilisha kwa huyo mama.
 
Hawa Ccm walizoea kufanya kazi na vilaza,watakoma sasa! Hii nchi ishawashinda waawaachie wenyewe
 
Mwanasheria, huyu spika nae saa zingine naona kama ana kichaa kama siyo ubishi wa kijinga. Kutwaaaa kuwambia watu wathibishe wakati hata sisi wananchi tunaona ukweli uko wapi.
 
Back
Top Bottom