Tundu Lissu Ndani ya BBC--Focus On Africa

Tundu Lissu Ndani ya BBC--Focus On Africa

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa chama cha mawakili Tanzania (TLS) amehojiwa na kipindi cha BBC-focus on Africa juu ya hali ya kisiasa nchini na jaribio la mauaji ambalo yeye ameliita la 'kisiasa'.

Alipoulizwa na mwanahabari wa BBC (Victor Kenani) iwapo anahisi usalama kurudi nchini, Lissu amesema haisi kuwa salama kutokana na hali ilivyo ya kisiasa nchini siku za hivi karibuni.

Kadhalika aliulizwa iwapo familia yake imetaka asijihusiishe na mambo ya kisiasa, Lissu amesema, hata mke wake ametishia kumtaliki iwapo tu ataacha au kuupa kisogo msimamo wake.

Lissu ambaye tangu shambulizi dhidi yake limetokea mjini Dodoma kwenye eneo la makazi yake, amekuwa akifuatiliwa na maelfu ya watu ambapo jana wakati akizungumza na wanahabari moja kwa moja kutoka hospitalini Nairobi, watu laki tatu na nusu walikuwa wakifuatilia kipindi hicho kilichorushwa kupitia ukurasa wa BBC kwenye mtandao wa kijamii wa facebook. Lissu alitumia lugha zote mbili yaani Kiswahili na Kiingereza kwa ajili ya kurahisisha zoezi la ku-cover story kwa wanahabari wote. Uzungumzaji wa lugha zote mbili ulikuwa ni fasaha, huku wakati fulani akiwatania Wakenya kwa kusema 'Kiswahili chenu ni cha mashaka mashaka'.

Lissu ambaye alimshukuru Mungu kwa kusalimika, pia aliwashukuru madkatari wa Dodoma, Nairobi, Watanzania kwa ujumla kwa sala na michango kwa matibabu yake na uongozi mzima wa CHADEMA kutokana na kuchukua tahadhari tangu siku ya tukio hadi hivi sasa.

Leo, alfajiri tarehe: 6-Jan-2018, Tundu Lissu amesafirishwa kwenda nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi kutokana na shambulio la risasi toka kwa watu wasiojulikana miezi minne iliyopita.
Chanzo: BBC.com
 
Back
Top Bottom