Tundu Lissu: Mahakama ya gizani sio Mahakama huru au ya haki, Haki haiwezi kufanyika gizani na ikaonekana imefanyika

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
892
1,000
Mh. Tundu Lissu, baada ya kupewa taarifa juu ya ukandamizwaji wa haki za wasikilizaji na wafuatiliaji wa case ameandika;

"Nimetaarifiwa kwamba Polisi na/au Mahakama wanazuia watu kuingia na simu mahakamani ili kudhibiti utoaji wa taarifa za yanayoendelea kwenye kesi ya uongo dhidi ya Mwenyekiti Mbowe. Haki lazima ifanyike na ionekane imefanyika. Haki haiwezi kufanyika gizani na ikaonekana imefanyika"

"Mahakama lazima iruhusu watu kusikiliza kesi hii ya kihistoria bila vizingiti visivyo & msingi. Ni lazima watu waingie & simu ili kutuhabarisha juu ya kinachoendelea mahakamani. Ni haki yetu kujua. Mahakama ya gizani sio mahakama huru au ya haki. Tunataka mahakama huru & ya haki!"

Kwenye Mahakama za Kenya kesi kubwa zinaendeshwa hadharani & kuonyeshwa on 'Live TV.' Kwenye Mahakama za Tanzania ya Chifu Hangaya, wanataka kesi kubwa & ya kihistoria kama hii iendeshwe gizani & mafichoni. Haikubaliki! Mahakama ya gizani & mafichoni sio mahakama huru au ya haki!
 
Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,321
2,000
Kwa Mamlaka niliyo nayo kuanzia Leo mtu akiongea Mambo ya kijinga jinga tutasema ameongea Jambo la Kingai.
Au kwa tafsiri nyingine ni kuwa maana neno UJINGA ni Kingai.

CC BAKITA

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,815
2,000
Mh. Tundu Lissu, baada ya kupewa taarifa juu ya ukandamizwaji wa haki za wasikilizaji na wafuatiliaji wa case ameandika;

"Nimetaarifiwa kwamba Polisi na/au Mahakama wanazuia watu kuingia na simu mahakamani ili kudhibiti utoaji wa taarifa za yanayoendelea kwenye kesi ya uongo dhidi ya Mwenyekiti Mbowe. Haki lazima ifanyike na ionekane imefanyika. Haki haiwezi kufanyika gizani na ikaonekana imefanyika"

"Mahakama lazima iruhusu watu kusikiliza kesi hii ya kihistoria bila vizingiti visivyo & msingi. Ni lazima watu waingie & simu ili kutuhabarisha juu ya kinachoendelea mahakamani. Ni haki yetu kujua. Mahakama ya gizani sio mahakama huru au ya haki. Tunataka mahakama huru & ya haki!"

Kwenye Mahakama za Kenya kesi kubwa zinaendeshwa hadharani & kuonyeshwa on 'Live TV.' Kwenye Mahakama za Tanzania ya Chifu Hangaya, wanataka kesi kubwa & ya kihistoria kama hii iendeshwe gizani & mafichoni. Haikubaliki! Mahakama ya gizani & mafichoni sio mahakama huru au ya haki!
Wanaficha aibu. No more, no less.
 
Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
24,568
2,000
Kwa hiyo kabla ya hizi simu za viganjani hazijagundulika mahakama ilikuwa inafanyika gizani? Ha ha ha, Lisu aendelee tu kila mishkaki na kunywa mvinyo huko ubelgiji.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,885
2,000
Kwa hali inavyoelekea, Chifu Hangaya ana uhakika wa ushindi kupitia vyombo vya dola 2025.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom