Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kwenye mikutano yako ongelea suala la kurudisha Bunge Live, kurekebisha Makato ya Bodi ya Mikopo na suala zima la Mafao ya Wastaafu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kamanda Lissu; nakushauri,pamoja na mambo mengine, usisahau kuongelea mambo hayo matatu yanayogusa na kuumiza wananchi wengi wa nchi kama ulivyozungumzia suala la TRA na wafanyabiashara pamoja na swala la wafanyakazi kutoongezewa mishahara siku ya jana mkoani Morogoro.

Awamu hii ya tano imepuuza wananchi kwa kiwango kikubwa mno na matokeo yake imepoteza mvuto mbele ya wananchi kwa kiasi kikubwa mno.

Kuiangusha CCM hii panapo Tume Huru, ni sawa na kusukuma mlevi, na hata pasipo Tume Huru, bado tunaweza tu kuipiga mweleka kwa kutokubali kuibiwa kura.

Waacheni wategemee viongozi wa dini sisi tujikite kwa wapiga kura maana wao hawana la kuwaambia.
 
Waacheni wategemee viongozi wa dini sisi tujikite kwa wapiga kura maana wao hawana la kuwaambia.
Leo huamini nguvu ya Bagonza na Dr shoo? Huo ushauri wako ndio unampiteza kabisa mgombea wako,bunge live linamsaidia Nini mkulima wa kawaida anaeshinda shamba kutwa?

Uchaguzi wa mwaka huu utakua mwepesi sana kwa ccm,inaonekana chadema mtakosa kabisa hoja.
 
Leo huamini nguvu ya Bagonza na Dr shoo?
Huo ushauri wako ndio unampiteza kabisa mgombea wako,bunge live linamsaidia Nini mkulima wa kawaida anaeshinda shamba kutwa?
Uchaguzi wa mwaka huu utakua mwepesi sana kwa ccm,inaonekana chadema mtakosa kabisa hoja
Umesoma sera za CHADEMA kuhusu mkulima?
 
Pia atueleze jinsi atakavyowashughulikia wahujumu uchumi, wazembe kazini, makanjanja, matapeli, majambazi n.k

Hapo tangu aanze kujinasibu sijamsikia akielezea! Au nchi hii haina watu wa aina hiyo, waliopo ni wale tu wanaoonewa na serikali ya anko Magu?
 
pia atueleze jinsi atakavyowashughulikia wahujumu uchumi, wazembe kazini, makanjanja, matapeli, majambazi n.k

Hapo tangu aanze kujinasibu sijamsikia akielezea! Au nchi hii haina watu wa aina hiyo, waliopo ni wale tu wanaoonewa na serikali ya anko Magu?
Huko hawezi kugusa Kuna acacia huko
 
  • Thanks
Reactions: ZNM
Leo huamini nguvu ya Bagonza na Dr shoo? Huo ushauri wako ndio unampiteza kabisa mgombea wako,bunge live linamsaidia Nini mkulima wa kawaida anaeshinda shamba kutwa?

Uchaguzi wa mwaka huu utakua mwepesi sana kwa ccm,inaonekana chadema mtakosa kabisa hoja
Kama halimsaidii mkulima mbona baba ako hataki liwe live?
 
Hadi hapo alipofukia kwa hayo maamuzi na kama chama wanatakiwa kywa na ajenda yao, mnaita ilani sijui kama nimeenda sawa.

Sasa kama hadi sasa hivi bado anategemea na kusikilizia anaambiwa aseme nini itakua miluzi mingi. Tusubirie kampeni zianze.

Angalizo: Sijamsikiliza sana jamaa lakini anahitaji kuboresha sana content za hotuba zake na namna anavyozifanya.
 
Mleta mada uko sahihi, aongelee

1. Bunge live
2.Makato yalivyo makubwa bodi ya mikipo
3. Azungumzie sana korosho, mbaazi na ufuta
4.Azungumzie waliovunjiwa nyumba zao ubungo-mbezi na aahidi kuwalipa kifuta machozi
5. Azungumzie Viongozi wa dini ya waislamu wanavyosota jela bila haki
6.Azungumzie maslahi ya watumishi wa umma
7. Azungumzie kuchoma nyavu za wavuvi
8. Azungumzie kejeli, sexism, dhidi ya wanawake
9. Azungumzie kutojali watu, mfano Tetemeko la Kagera, na la njaa etc
10.Azungumzie kutoheshimu sheria na katiba na watu kupotezwa, maiti kuokotwa kwenye viroba
11. Azungumzie uminywaji wa uhuru wa habari
12. Azungumzie uonevu kwa wafanyabiashara, kubambikiziwa kodi
13. Azungumzie tatizo la utapiamlo ambapo vitoto vichanga zaidi ya 30% vina tatizo la utapia mlo nchini
14. Azungumzie tatizo la ajira kwa vijana, serikali haiajiri huku inajenga uwanja wa ndege usiokuwa na maslahi wa Chato
15. Azungumzie kushuka kwa exports zetu zitokanazo na kufa kwa kilimo na uzalishaji viwandani (Wasaidizi wake wamsaidie kumpa data za hali halisi)
16. Azungumzie kufeli kwa diplomasia nchini, aeleze jinsi nchi yetu ilivyokuwa juu na yenye ushawishi miaka michache iliyopita lakini leo Magufuli ameipotezea heshima hiyo

17. Azungumzie kuhusu halmashauri kunyang'anywa vyanzo vya mapato na matokeo yake zinashindwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama vile usafi etc

18. Azungumzie kuhusu 20000 za vitambulisho vya wamachinga kuwa siyo haki kwa sababu zimewekwa kinyume cha sheria za serikali za mitaa au sheria ya kodi

19. Azungumzie kuhusu Kikotowo, kuwa serikali ya Magufuli imeahirisha tatizo kijanja kupisha upepo wa uchaguzi, uchaguzi ukishapita italirudisha kinguvu, Lissu aseme kama serikali hsina nia mbaya kwa nini isiifute hiyo sheria ya kikokotowo na badala yake imeahirisha hilo jambo hadi 2023?

Atoe Ahadi zifuatazo
1.Aseme akiwa rais ataleta katiba mpya
2. Akiwa rais naye ataanza kulipa kodi, aseme Magufuli halipi kodi na hataki kubadili utaratibu huo ili alipe kodi
3. Atoe ahadi ya kupambana na rushwa na ufisadi bila kumuangalia mtu usoni. Lissu aseme Magufuli anaangalia watu usoni na kuchagua wa kumshughulikia na nani wa kumuacha, ndiyo maana hajaweka ndani kiongozi yeyote aliyekamatwa kwa matendo ya kifisadi kwa mfano Lugola, Andengenye na wengine ambao yeye mwenyewe anasema anayajua kuwa ni majizi

4.Aeleze kuwa ataboresha mapungufu yaliyokuwemo kwenye mchakato wa gesi na kuuendeleza kisha atajenga mtambo wa kuzalishia Umeme wa Gesi kama ilivyokuwa kwenye plan hapo awali

5. Aeleze kuwa ataendelea na SGR lakini kwa utaratibu bora zaidi. Lissu akosoe utaratibu wa ujenzi wa reli ya sasa kuwa unategemea mkopo mkubwa sana utakaotuletea shida mbeleni

6. Atoe ahadi ya kupanua wigo wa elimu bure, hadi kidato cha sita tofauti na sasa ambapo Magufuli ameishia kidato cha nne na bado kuna usanii mwingi kwenye hiyo elimu bure

8. Asisahau kabisa kuzungumzia Afya na Maji, na Chakula aeleze kuhusu BIMA ya afya kwa wote, na aweke kwenye katiba kuwa haki ya kula na kunywa ni haki ya binadamu, hii itailazimisha serikali kusaidia watu wake kipindi cha njaa, na pia kuhakikisha inafanya iwezavyo ili kila mtu apate maji safi ya kunywa (Hii point itaresonate na umma sana)

7. Kiufupi Lissu inabidi amnyang'anye Magufuli talking points zake kwa kuzitoboatoboa matobo kila mahali!

Lissu akitambaa na hizi nondo, Umma utamuelewa sana!
 
Mleta mada uko sahihi, aongelee

1. Bunge live
2.Makato yalivyo makubwa bodi ya mikipo
3. Azungumzie sana korosho, mbaazi na ufuta
4.Azungumzie waliovunjiwa nyumba zao ubungo-mbezi
5. Azungumzie Viongozi wa dini ya waislamu wanavyosota jela bila haki
6.Azungumzie maslahi ya watumishi wa umma
7. Azungumzie kuchoma nyavu za wavuvi
8. Azungumzie kejeli, sexism, dhidi ya wanawake
9. Azungumzie kutojali watu, mfano Tetemeko la Kagera, naa la njaa etc
10.Azungumzie kutoheshimu sheria na katiba na watu kupotezwa, maiti kuokotwa kwenye viroba
11. Azungumzie uminywaji wa uhuru wa habari
12. Azungumzie uonevu kwa wafanyabiashara, kubambikiziwa kodi
13. Azungumzie tatizo la utapiamlo ambapo vitoto vichanga zaidi ya 30% vina tatizo la utapia mlo nchini
14. Azungumzie tatizo la ajira kwa vijana, serikali haiajiri huku inajenga uwanja wa ndege usiokuwa na maslahi wa Chato
15. Azungumzie kushuka kwa exports zetu zitokanazo na kufa kwa kilimo na uzaloshaji viwandani (Wasaidizi wake wamsaidie kumpa data za hali halisi)
16. Azungumzie kufeli kwa diplomasia nchini, aeleze jinsi nchi yetu ilivyokuwa juu na yenye ushawishi miaka michache iliyopita lakini leo Magufuli ameiporwzea hwshima hiyo

17. Azungumzie kuhusu halmashauri kunyang'anywa vyanzo vya mapato na matokeo yake zinashindwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama vile usafi etc

18. Azungumzie kuhusu 20000 za vitambulisho vya wamachina kuwa siyo haki. kwa sababu zimewekwa kinyume cha sheria za serikali za mitaa au sheria ya kodi

Atoe Ahadi zifuatazo
1.Aseme akiwa rais ataleta katiba mpya
2. Akiwa rais naye ataanza kulipa kodi, aseme Magufuli halipi kodi na hataki kubadili utaratibu huo ili alipe kodi
3. Atoe ahadi ya kupambana na rushwa na ufisadi bila kumuangalia mtu usoni. Lissu aseme Magufuli anaangalia watu usoni na kuchagua wa kumshughulikia na nani wa kumuacha, ndiyo maana hajaweka ndani kiongozi yeyote aliyekamatwa kwa matendo ya kifisadi kwa mfano Lugola, Andengenye na wengine ambao yeye mwenyewe anasema anayajua kuwa ni. majizi

Lissu akitambaa na hizi nondo, Umma utamuelewa sana!
Pia aongelee suala mafao ya watumishi wa sector binafisi, hususani kurejeshwa fao la kujitoa Nssf. Haiwezekani MTU anapoteza ajira akiwa kwenye 30's anaambiwa asubiri mafao yake hadi atakapofikisha umri wa kustaafu yaani 55-60yrs.

Cc:
CHADEMA
Tumaini Makene
 
Huko hawezi kugusa Kuna acacia huko
Pole Lissu,Mungu atakuponya,Pole Lissu.

Leo nimemsikiliza Katibu mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji akielezea hali ya Tundu Lissu,nimestuka sana kwamba mguu na mkono wa kushoto pamoja na nyonga zimevunjwa,mara ya kwanza nilipopata taarifa za Lissu Kupigwa Risasi,nilichagua kukaa kimya nisiseme wala kuandika kitu,niwasikilize zaidi wengine.

Baadae nilianza kuona picha na taarifa mbalimbali za jinsi Lissu alivyojeruhiwa,niliumia sana kuona binadamu mwenzangu alivyoumizwa,sikuwa na taarifa sahihi jinsi Lisu alivyoumizwa.

Kesho yake nikamuona Spika akitoa taarifa bungeni na kuueleza umma kuwa Lisu alimiminiwa Risasi 32,nilistuka sana,kwa nini Risasi 32 zimiminwe kwa mwanadamu?mtu ambaye si jambazi?inakuwaje Risasi zaidi ya 30 zimiminwe kwa Mwanasiasa na mwanasheria?.

Nilibaki natetemeka,nikikuomba Mungu anipe moyo wa kujifunza kwa wengine na nijue hasa kwa nini mwanasiasa na mwanasheria amiminiwe Risasi zaidi ya 30?kakosa nini?

Kwa nini najiuliza maswali mengi mpaka sasa na kubaki njia panda?

Binafsi nilimfahamu Lissu kabla hajaingia bungeni mara ya kwanza kukutana nae ilikuwa mwaka 2006,wakati huo Lissu alikuwa mpambanaji mkubwa na makampuni makubwa ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini Tanzania!.

Nilikutana nae wakati huo nikiwa nimejikita zaidi kwenye uandishi wa habari za madini,tulijikuta wote tupo kwenye eneo moja,yeye akifanya kama mwanasheria na mimi nikifanya kama mwandishi wa habari.

Lissu aliniambia amekuwa na mapambano makubwa na kampuni la Barrick,alikuwa akipaza sauti kweli kweli kuhusu wizi unaofanywa na wawekezaji hawa,Lissu alikuwa ni miongoni mwa wanaharakati kutoka chama cha wanasheria wa mazingira waliopaza sauti kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma dhidi ya mgodi wa Bulyanhulu kuwa uliwafukia baadhi ya wachimbaji wadogo,kama sijakosea ilikuwa mwaka 1999.

Lissu aliniambia mapambano yake na Barrick yalimsababishia aishi maisha magumu yaliyojaa hofu,Serikali ilimpinga na kusema Lissu alikuwa anasema uongo na kuwagombanisha wawekezaji na wananchi.

Lisu akaniambi alilazimika kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea tuhuma dhidi ya Barrick,mkutano ule aliufanya muda mfupi kabla hajaondoka kwenda masomoni Nchini Marekani,mkutano ule ulimsababishia ugomvi mkubwa na Serikali ya Awamu ya tatu,aliitwa majina mengi,kubwa lilikuwa mchochezi.

Lissu alipotoka kwenye masomo yake ya shahada ya pili,aliendelea na harakati zake za kupambana na wawekezaji kwenye sekta ya madini.

Lissu aliporudi alikuta kundi kubwa la wananchi wanaoshi pembezoni mwa migodi wakiwa kwenye vifungo baada ya kukutwa na makosa ya uvamizi kwenye migodi,Lissu aliamua kuanza mchakato wa kuwatetea na hata kukata rufaa kwa watu waliokuwa wamewekwa ndani kwa makosa ya kuvamia migodi,makumi kwa mamia ya watu walitetewa bure na kutoka jela kwa utetezi wa Lissu bila malipo,Lisu alipataza sauti kuwa uwekezaji umegeuka kuwa unyama nchini Tanzania.

Harakati zake zilimsababishia ugomvi na serikali pamoja na wawekezaji,mwaka 2011,Baadhi ya wakazi wa Nyamongo waliingia kwenye mgodi kusaka mabaki,wakapogwa Risasi na Polisi na watu wawili nakumbuka walifariki dunia.

Lissu akiwa kwanza ndiyo ameingia bungeni,alikwenda Nyamongo,aliitisha mikutano,familia na wanajamii ya nyamongo,ziligoma kuzika maiti zilizopigwa Risasi.

Lissu akiwa Nyamongo alikamatwa na kuwekwa ndani kwa makosa ya kuwachochea wananchi wawachukie wawekezaji,Lissu aliwekwa ndani akafikishwa mahakamani na baadae kuamriwa asikanyage Nyamongo kwani amekuwa anachochea chuki wananchi wa Tarime wawachukie Barrick,sidhani kama katazo hilo lilifutwa.

Mwaka 2006,jumuiya ya viongozi wa dini nchini hapa ni viongozi wa dini zote na madhehebu yote,nakumbuka mara mbili nilifuatana nao,kwa kushirikiana na Lissu ilizunguka migodi yote nchini kuwatetea wananchi waliokuwa wananyanyaswa na wawekezaji.

Nakumbuka kwenye tema hiyo alikuwemo Shehe Fereji,Askofu Munga,Askofu Mkuu Ruzoka na viongozi wengi,hawa walipaza sauti kuiambia serikai kuhusu wizi na unyama unaofanyika kwenye sekta ya madini nchini.

Mpaka leo nalikumbuka chozi la Aksofu Munga na Shehe Fereji walipofika kwenye mgodi wa RUSU huko Nzega mkoani Tabora baada ya kukuta wananchi wakiteseka na kuishi maisha ya simanzi na umasikini wa kutopea,kwa kila aliyepaza sauti aliitwa mchochezi ana wivu wa maendeleo.

Viongozi wa dini hawa walitafuta wataalam kutoka ndani na nje ili wafanye utafiti wa kisayansi kuhusu mchango wa sekta ya madini nchini.

Walikuwa ni Curtus na Tundu Lissu ndiyo waliozunguka migodi yote nchini na kutoka na ripoti ya kina kuhusu hali ya uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Lissu na Curtus walikusanya ushahidi kutoka mgodini,serikalini na kwa wananchi wa kawaida,wakatoka na ripoti iliyoitwa
"THE GOLDEN OPPORTUNITY",ripoti hii waweza ipata mtandaoni,iliandikwa na Lisu huyu ambaye muda huu anateseka kitandani huko Nairobi.

Mwaka 2009,wakati huo nikifanya uchunguzi kuhusu ukweli wa sumu za mti Tigite huko Nyamongo,na hii ni baada ya baadhi ya wakazi wa Nyamongo kubabuka na wengine walipoteza maisha kutokana na kilie kilichodaiwa kuwa ni Sumu,nilipokuwa Nyamongo,kila familia niliyoitembelea,walikuwa wananiambia niwasaidie kumwambie Lissu aende kwani wanakufa na Sumu.

Watu wale walimuona Lisu ndiyo kimbilio lao,mwaka Huo huo,ili kuionesha ushahidi serikali kuwa mgodinwa Barrick umetiririsha sumu kwenye vyanzo vya maji huko Nyamongo,Lisu huyu anayeteseka huko Nairobi muda huu na chama cha wanasheria za mazingira walilazimika kuwasafirisha kwa ndege waathirika wa sumu za mto Tigite.

Lissu alimsafirisha mzee Mwikwabe ambaye mwili wake ulikuwa umebabuka na sumu za mto Tigite,ilikuwa ni usiku kupitia Channel Tena,Lissu akiwa na Mzee Mwikwabe,walijitikeza kwenye mjadala na Lissu akawa anaongea kwa ukali akiiambia Serikali,"Mnataka niwape ushahidi upi ili muamini kuwa huko Nyamongo kuna watu wanakufa kwa sumu zinazotiririshwa na mgodi"

Lisu hakusikilizwa,Mgodi ulikana,Serikali
ilikana,bunge liliunda kamati ,kama sikosei spika wa sasa wakati huo akiwa mwenyekiti wa kamati walikwenda Nyamongo ba baadae wakasema hakuna ushahidi kuwa zile ni sumu.

Nakumbuka siku kamati ilipokuwa Nyamongo,mimi na team yangu tulikuwa Nyamnongo,katika kijiji cha Kewanja,wananchi waliwaambia wabunge wa kamati ya mazingira kuwa kama wanadhani maji hayana sumu wanaguse ama kunywa,hakuna mbunge aliyegusa.

Ni Lissu na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Christopher Gamaina wakati huo akiwa na Gazeti la Mtanzania ndiyo waliosema kuna watu wameungua kwa sumu.

Lissu alisimama na kusema bila hofu kuwa wawekezaji hawa wanaliibia taifa,wanaua watu kwa bunduki na sumu zinazitirirka kwenye vyanzo vya maji,lakini akaitwa mwanaharakati anayetaka wagombanisha wawekezaji na wananchi.

Nakumbuka wakati tunachunguza ukweli wa sumu kwenye mto Tigite,moja ya nyaraka tulizotumia ni Ripoti za Lissu,nakumbuka kwenye makala za uchunguzi huko Geita,tulitumia mapendekezo ya ripoti Lisu na Curtus kuitaka serikali ifanye
mabadiliko ya kisera na kisheria ili watanzania wanufaike na madini,Ripoti ya Lisu ndiyo ilikuwa mwongozo wa nini tufanye?

Najiuliza,mbona Lissu amekuwa mpambanaji wa mali za umma,tangu ubarubaru wake leo anatesema kiasi hiki na hata kudhihakiwa na baadhi ya watu wakati huu akitesema huko Nairobi?

Muda,Ujasiri,kujitoa kwake kupambana na wawekezaji wa Lissu hautoshu wote tunuombee badala ya wengine kumdhihaki?,ni kweli kazi na upambanaji wa Lissu haujulikani?

Pole Lissu,Mungu anajua kazi za akili na mikono yako,naamini utapona Lissu,nayaona maumivu uliyonayo muda huu hapo hospitali,Naamini Utapona,naaamini Mungu anayaona maumivu na machozi.
 
Mkuu unataka asiongelee namna alivyo pigwa risasi..
Wewe ndo utampatia Kura za Huruma.

Acha Aendelee kutia huruma majukwaani Watanzania tuna huruma Sana tutamuhurumia.
 
Mkuu unataka asiongelee namna alivyo pigwa risasi..
Wewe ndo utampatia Kura za Huruma.

Acha Aendelee kutia huruma majukwaani Watanzania tuna huruma Sana tutamuhurumia.

Hilo la kupigwa risasi ni muhimu sana aendelee kuliongelea, maana kupigwa kwake risasi halafu serikali hii haichunguzi suala hilo ni ushahidi kuwa tuna serikali mbaya ambayo tunahitaji kuing'oa madarakani
 
Kamanda Lissu; nakushauri,pamoja na mambo mengine; usisahau kuongelea mambo hayo matatu yanayogusa na kuumiza wananchi wengi wa nchi kama ulivyozungumzia suala la TRA na wafanyabiashara pamoja na swala la wafanyakazi kutoongezewa mishahara Siku ya jana mkoani Morogoro.

Awamu hii ya tano imepuuza wananchi kwa kiwango kikubwa mno na matokeo yake imepoteza mvuto mbele ya wananchi kwa kiasi kikubwa mno.

Kuiangusha CCM hii panapo Tume Huru, ni sawa na kusukuma mlevi na hata pasipo Tume Huru, bado tunaweza tu kuipiga mweleka kwa kutokubali kuibiwa kura.

Waacheni wategemee viongozi wa dini sisi tujikite kwa wapiga kura maana wao hawana la kuwaambia.
Baada ya uteuzi wa NEC tarehe 26/08 kampeni zitaanza tarehe 26/08 ambazo zitakuwa za siku 60. Tusubiri muda wa kampeni ufike, ni mambo mengi ya kuyasemea na mengi nafikiri yapo kwenye ilani yao ya chama. hoja zako ni nzuri, ni vizuri wazisemee wakati wa kampeni.
 
Kamanda Lissu; nakushauri,pamoja na mambo mengine; usisahau kuongelea mambo hayo matatu yanayogusa na kuumiza wananchi wengi wa nchi kama ulivyozungumzia suala la TRA na wafanyabiashara pamoja na swala la wafanyakazi kutoongezewa mishahara Siku ya jana mkoani Morogoro.

Awamu hii ya tano imepuuza wananchi kwa kiwango kikubwa mno na matokeo yake imepoteza mvuto mbele ya wananchi kwa kiasi kikubwa mno.

Kuiangusha CCM hii panapo Tume Huru, ni sawa na kusukuma mlevi na hata pasipo Tume Huru, bado tunaweza tu kuipiga mweleka kwa kutokubali kuibiwa kura.

Waacheni wategemee viongozi wa dini sisi tujikite kwa wapiga kura maana wao hawana la kuwaambia.
Nani mshauri wake wa masuala ya kodi au anaropoka tu kama kawaida yake. Dunia itatuona watuwa ajabu kama tutaongozwa na LISSU, kwa hali hiyo hatutampa nafasi hiyo ili kuepuka dhahama
 
Kamanda Lissu; nakushauri,pamoja na mambo mengine; usisahau kuongelea mambo hayo matatu yanayogusa na kuumiza wananchi wengi wa nchi kama ulivyozungumzia suala la TRA na wafanyabiashara pamoja na swala la wafanyakazi kutoongezewa mishahara Siku ya jana mkoani Morogoro.

Awamu hii ya tano imepuuza wananchi kwa kiwango kikubwa mno na matokeo yake imepoteza mvuto mbele ya wananchi kwa kiasi kikubwa mno.

Kuiangusha CCM hii panapo Tume Huru, ni sawa na kusukuma mlevi na hata pasipo Tume Huru, bado tunaweza tu kuipiga mweleka kwa kutokubali kuibiwa kura.

Waacheni wategemee viongozi wa dini sisi tujikite kwa wapiga kura maana wao hawana la kuwaambia.
Pensheni za wastaafu wa TRC bilioni 50+ zililiwa. Ukiuliza hamna jibu.
 
Back
Top Bottom