Tundu Lissu: Silipwi na Ubelgiji mimi sio Mkimbizi wa Kisiasa

Habari Zote

New Member
Sep 15, 2022
2
11
SILIPWI NA UBELGIJI, MIMI SIO MFUNGWA WA KISIASA - LISSU.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Antipas Mugway Lissu amesema halipwi na Serikali ya Ubelgiji wala Shirika la Wakimbizi kwa kuwa hakuomba ukimbizi wa Kisiasa (political asylum) nchini humo.

Akijibu swali aliloulizwa na miongoni mwa wasikilizaji wa mtandao wa Clubhouse katika chumba kilichoandaa mkutano huo wa mtandaoni kinachojulikana kama Courtroom, Lissu alisema “Mimi sio mkimbizi wa kisiasa, sikutuma maombi ya kuomba kuwa mkimbizi wa kisiasa Ubelgiji kwa sababu unakuwa mtumwa wao, huwezi kwenda popote bila kibali chao, ni lazima wakuruhusu," alisema Tundu Lissu.

Hata hivyo Tundu Lissu aliongeza kwa kusema kuwa: “Maneno wanayosema watu kuwa ninalipwa si ya kweli na ninaomba yapuuzwe kwa sababu Political Ssylum ina masharti yake, na ninyi ni mashahidi, nilikuja Ubelgiji kwa ajili ya matibabu na nimetibiwa kwa michango yenu na pesa zenu."

Lissu akizungumza juu ya nani anahudumia mahitaji yake akiwa Ubelgiji, Lissu alisema kuwa anaishi kwa kazi ya utafiti anayoifanya ambayo ndiyo humpatia fedha, anasema: “Sikiliza, ninafanya utafiti, huo ndiyo unaonilipa na kuishi pamoja na michango yenu."

Aidha, akijibu swali la kwa nini harudi nyumbani wakati mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan yalifanyika na kuhakikishiwa usalama Tundu Lissu alijibu kwa kusema kuna mambo bado hayajakamilika na pindi yatakapokuwa tayari atarejea nyumbani, aliongeza kusema kuwa angesharudi tangu mwezi wa 7, 2022 kama taratibu zote zingekuwa zimekamilika.

Akizungumzia masuala ya uchaguzi Nchini Tanzania, Tundu Lissu alisema mfumo wa uchaguzi umeharibika na kuharibiwa kiasi cha kuhitaji kurekebishwa ili kuweka uhuru wa Mtu kuchaguliwa na Wananchi kuchagua mtu wanayeina anafaa kuongoza.

“Hakuna asiyejua kwamba uchaguzi wa mwaka 2020 uliharibiwa na Tume pamoja na aliyekuwa Rais wa wakati huo,” alisema Lissu.

Akifafanua juu ya sifa ya kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Lissu alisema ibara ya 67 (1) ya Katiba ya Tanzania inayotumika sasa ya Mwaka 1977 inayotambua sifa ya kujua kusoma na kuandika kama sifa Kuu ya mtu kuchaguliwa kuwa Mbunge haitoshi.

Ametaja sababu miongoni mwa Majukumu ya Mbunge ni kutunga Sheria za Nchi huku alikosoa pia sifa ya mtu kuchaguliwa katika nafasi ya Rais wa Nchi ambapo Katiba inatamka kuwa awe na sifa za Mbunge ambazo ni kujua kusoma na kuandika, Lissu alisisitiza kwa kudai kwamba hii inaweza kupelekea kupata Rais asiye na uwezo wa kuongoza nchi.

Tundu Lissu alielezea zaidi na kusema kuwa Mbunge ambaye anatakiwa kuchambua ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, kuchambua vitabu vya bajeti, kutunga katiba kwa kuwa Bunge letu lina mamlaka hiyo, kupitisha Mikataba ya Kimataifa, kupitia nyaraka zinazohusu pesa za Umma, na kusema kuwa kwa kiwango cha Mbunge kujua kusoma na kuandika tu itakuwa ni ngumu kwa Mbunge huyo kuchambua maswala mazito kama hayo ya Taifa kwa kuwa uwezo wao hautoshelezi na kwamba anatakiwa kuwa na uelewa wa mambo mengi.

Lissu ameongelea Sheria za Kikoloni ambazo pamoja na ukandamizaji wake bado zilitamka kuwa nafasi ya Uwakilishi inahitaji Elimu lakini baada ya Uhuru na Mfumo wa Vyama Vingi sifa ya Uwakilishi ikatamkwa kuwa iwe kusoma na kuandika.

Akiongelea kutokuwepo usawa katika mgawanyo wa Majimbo ya Uchaguzi Tundu Lissu amesema kuwa wakati wa Chama Kimoja pamoja na Katiba kutamka kuwa na mgawanyo sawa wa Majimbo kulingana na idadi ya watu.

Amesema suala hilo limepuuzwa baada ya mfumo wa vyama vingi ambapo kwa sasa mgawanyo huo haupo sawa na kueleza kuwa Mikoa yenye idadi kubwa ya watu ambayo inaunga mkono Upinzani Majimbo ni Machache ukilinganisha na Mikoa yenye watu wachache ilyogawanywa kupata Majimbo mengi kwa sababu ni ngome ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na utafiti aulioufanya, Lissu anasema wenye Mamlaka ndiyo wametumika kuhujumu Demokrasia kwa masilahi yao wanayoyajua.

Ameitaja Mikoa yenye idadi kubwa ya wapiga Kura kuwa ni Dar es Salaam yenye Majimbo 10 ikiwa na wapiga kura 3,427,000, ukifuatiwa na Mkoa wa Mwanza 1,845,000 ikiwa na Majimbo 9 ya Uchaguzi, Morogoro ni ya 3 ikiwa na wapiga kura 1,612,000 Majimbo 11, Tabora wapiga kura 1,463,000 Majimbo 12, Kagera, Dodoma, Tanga, Arusha, Geita na Mbeya.

Amesema Mikoa tajwa hapo juu ndiyo yenye Idadi kubwa ya Wapiga Kura walioandikishwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020 ikiwa na wapiga kura Milioni 16 na Majimbo ya Uchaguzi 94, huku Mikoa iliyobaki ikiwa na Wapiga kura takribani Milioni 13 na Majimbo 120 ya Uchaguzi ikiwa na 45% ya Idadi ya Wapiga kura na 56% ya Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi.

Aliongelea mahitaji ya kupata Katiba mpya na kusema kuwa madai ya Katiba Mpya hayajaanza leo kwa kuwa Katiba imekuwa ikifanyiwa marekebisho mara kwa mara inapohitajika na tangu miaka ya 1990 kumekuwepo madai ya kupata Katiba mpya.
png_20220915_174155_0000.jpg
 
Akiongelea kutokuwepo usawa katika mgawanyo wa Majimbo ya Uchaguzi Tundu Lissu amesema kuwa wakati wa Chama Kimoja pamoja na Katiba kutamka kuwa na mgawanyo sawa wa Majimbo kulingana na idadi ya watu, swala hilo limepuuzwa baada ya mfumo wa vyama vingi ambapo kwa sasa mgawanyo huo haupo sawa na kueleza kuwa Mikoa yenye idadi kubwa ya watu ambayo inaunga mkono Upinzani Majimbo ni Machache ukilinganisha na Mikoa yenye watu wachache ilyogawanywa kupata Majimbo mengi kwa sababu ni ngome ya Chama cha Mapinduzi (Ccm).

August 6, 2022


Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, Source: Mwanzo

 
SENSA NA DEMOKRASIA
Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

Source : Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita
 
Ni Watanzania wangapi walikuwa na elimu ya Sekondari tulipopata uhuru? Let's be fair and realistic.
 
Dah huyu jamaa bhana, c alisema amekimbia nchi kutokana na kutokuwa salama baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu. Sasa kukimbia nchi yako ina maana gani kama sio mkimbizi wa kisiasa.?
 
Dah huyu jamaa bhana, c alisema amekimbia nchi kutokana na kutokuwa salama baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu. Sasa kukimbia nchi yako ina maana gani kama sio mkimbizi wa kisiasa.?
Hakuna mtanzania mwenye uzalendo kwa nchi au chama kuliko tumbo lake.
AMINI KWAMBA.....

HAKUNA.....

Factor kubwa ya wao kukimbia nchi ilikua ni claim kwamba Magufuli alitaka kuwaua.

Haya Magufuli kafa warudi.....
Wanasema serekali ituhakikishie usalama wetu..tangu last year ndo ilikua sababu.

Waziri Masauni katoa tamko bungeni kwa wale wote walo ikimbia nchi warudi na watahakikishiwa usalama wao,
Lema akahojiwa na azam kuhusu tamko la waziri akawa enthusiastic kwamba this Christmas atailia uchagani.

September hii bob, wanakwambia kunamambo bado.
 
Tundu Lissu aache urongo, hawezi kuishi nchini Ubelgiji (kwa muda alokaa) kwa kulipwa peza za tafiti.
 
Tundu Lissu aache urongo, hawezi kuishi nchini Ubelgiji (kwa muda alokaa) kwa kulipwa peza za tafiti.
Member kama hujui haya mambo uliza kwa watu wa kitabu. Watakusaidia sana mpaka utaelewa. Kwa sasa jifunze toka kwa wenzio wenye ufahamu. Itakusaidia baadaye
 
Member kama hujui haya mambo uliza kwa watu wa kitabu. Watakusaidia sana mpaka utaelewa. Kwa sasa jifunze toka kwa wenzio wenye ufahamu. Itakusaidia baadaye
Na wewe kama ni mwanataaluma utakuwa wajishushia sana hadhi kama wakubali upuuzi aloongea jamaa kwamba aishi kwa malipo ya fedha za tafiti.

Angesema analipwa kwa kufanya mihadhara angeeleweka, maana fedha ya mihadhara "after dinner speech/ Workshops" ni nzuri kuliko hizi "handouts".
 
Back
Top Bottom