TUNDU LISSU: Kwa uzito wa msiba wa MANDELA barani AFRIKA kwa nini BUNGE lisiahirishwe?

Kwa kweli Mandela ni mtu wa kipekee sana katika bara la Afrika anapaswa kukumbukwa na kuenziwa kwa mchango wake.
Kama mnaamini hivyo mbona ni gazeti lenu pekee ndio Leo halikuandika kuhusu kifo chake. Acheni kutafuta umaarufu rahisi
 
Mheshimiwa Tundu Lissu ameomba mwongozo huo kwa spika Makinda ili bunge liahirishwe japo kwa leo kwa ajili ya maombolezo ya Mandela ambaye ni kielelezo kikubwa cha kiongozi aliyetukuka barani Afrika kwa mchango wake katika harakati za ukombozi. Hata hivyo spika hakukubaliana na hoja ya Tundu Lissu na kuruhusu bunge liendelee kama kawaida.
mkuu mandela kwangu ni African Icon pengine kuliko wengi ninaowasikia. ila swali langu Je lisu alizungumzia kuhusu kurudisha posho za kodi zetu walizosaini leo asubuhi?
 
Ni Mwanasheria Mkuu wa Chama na mwanafunzi wa Asha Rose Migiro.

Kwa hiyo Kama ni mwanafunzi wa Asha Rose Migiro unataka kutwambia nini. Kwani kuwa mwanafunzi wa mtu fulani kunaondoa uwezo binafsi ulionao? Mbona mnaongea pointi zisizo na maana?
 
Lissu alikuwa sahihi wangeahirisha japo kwa morning session b4 tea break then wangeendelea.Lakini sababu posho ni muhimu kuliko kitu kingine kwa wakati huu.they have let it go.R.I.P Madiba Mandela
 
Serikali imeshatoa maombolezo siku 3. Sasa kiherehere cha nini?
maombolezo ya siku tatu yanafanyikia wapi?unawaambia watu kuna maombolezo halafu taasisi kubwa kama bunge linaendelea na ratiba zake kama kawaida, hayo maombolezo anafanya nani na yanafanyikaje?
 
kachanganyikiwa-hali inayomkuta SLAA mikoani inaashiria kifo cha CDM-vyombo vya habar ambavyo wamekuwa wakifurahia mabadiliko ya siasa yaliyokuwa yakiongozwa na CDM nao sasa wamegundua kuwa ile ni SACCOS na wamepoteza imani na sasa wana wa- blast na sasa anafikiria mikakati yao ya kumngo'a ZZK(kipenzi cha wanyonge-mkataa posho za kukaa) ilivyokwama pamoja na kumbambikizia shutuma kibao kwa uroho wao wa madaraka-na sasa anafikiria yale makosa 11 aliyoyaandika kwa kujinasibu ambayo utadhani yameandikwa WP(Women Police) 123 wa kituo cha Igunguja(vijijini) na sio mwanasheria
Sidhani kama huu ni mchango katika mada hii!
 
Kweli tupo nyuma sana
kifikra tazama CNN kuanzia asubuhi hadi saa hizi ni TATA MADIBA,CITIZEN
pia angalia hiyo TBC majanga....BUNGE lenyewe halina impact kwa
watanzania yaani hata wakisema kusiwe na wabunge hakutakua na shida
yoyote..kazi ni kusubiri posho tu...shenzi shenzi

Wenyewe wanasema ukweli na uhakika!poor TBCCM!!!
 
Mheshimiwa Tundu Lissu ameomba mwongozo huo kwa spika Makinda ili bunge liahirishwe japo kwa leo kwa ajili ya maombolezo ya Mandela ambaye ni kielelezo kikubwa cha kiongozi aliyetukuka barani Afrika kwa mchango wake katika harakati za ukombozi. Hata hivyo spika hakukubaliana na hoja ya Tundu Lissu na kuruhusu bunge liendelee kama kawaida.
Kwanza bunge lenyewe magumashi tu, bunge la miaka 52 likiwa na wabunge waliokaa humo miaka 52 vilevile lakini bado mbunge anauliza serikali ina mpango gani ........., na majibu yanayotolewa ya kimagumashi hayakidhi haja ya swali, aliyeuliza swali hawezi ku emphasize apewe jibu linalotakiwa atanyamazishwa asiulize tena au swali lake lisiulizwe kabisa simply mhishimiwa supika halitaki swali hilo.

Ni bora waje kuomboleza mtaani huku kuliko kukaa hapo kupigana vijembe na mipasho kwa ghalama zetu!
 
wangeahirisha bunge tu waende bar kuangalia bbc na cnn na wengine waende dar kuangalia nyumba ndogo zao.
 
Mheshimiwa Tundu Lissu ameomba mwongozo huo kwa spika Makinda ili bunge liahirishwe japo kwa leo kwa ajili ya maombolezo ya Mandela ambaye ni kielelezo kikubwa cha kiongozi aliyetukuka barani Afrika kwa mchango wake katika harakati za ukombozi. Hata hivyo spika hakukubaliana na hoja ya Tundu Lissu na kuruhusu bunge liendelee kama kawaida.

Hawa jamaa wa CDM waache siasa udandiaji, haohao ndio wanaosema vyama tawala ni wakoloni weusi!! hiyo kauli aliyoitoa lissu ilitakiwa itolewe na mwana-ccm kwani ANC&CCM ni vyama ndugu na harakati zao ni moja, ndio maana rais jacob zuma aliwahi kuja hapa tz kwa mwaliko wa ccm, hii tu inatosha kuonesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya viongozi wa CCM na ANC, labda asubiri kwa wapinzani wenzao wa huko bondeni ila sio kwa mzee madiba.
 
Back
Top Bottom