Tundu Lissu ukiwa kwenye mstari wa mbele wa mapambano, yafanye yote kwa weledi na kadiri

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Mheshimiwa Tundu Lissu historia ya vita yako ya kutetea haki na utawala bora Tanzania imeandikwa kwa damu yako mwenyewe, na sina shaka hata kidogo wewe ni mpambanaji wa wapambanaji katika nchi yetu. Kati ya watu wachache wanaoweza kuelezea machungu ya kupigania haki na utawala bora duniani, basi wewe ni mhanga aliye hai na una kila moral authority ya kuelezea jinsi harakati hizo zilivyo ngumu na hatari!

Kwa bahari nzuri pia Mheshimiwa Freeman Mbowe, mwenyekiti wako, naye ni mpambanaji mahiri na yeye pia anajua machungu ya kupambana na walio madarakani, amepitia hatari nyingi, kupoteza mali na fedha nyingi, kupigwa na kufungwa miezi mingi gerezani. Chadema tunajivunia kuwa na viongozi wanaoongoza kwa mifano ya maisha yao wakiwa tayari kumwaga damu zao kusimamia wanachokiamini. Hicho ni kipeo cha juu zaidi cha uongozi na hakuna ujasiri zaidi ya huo!

Mheshimiwa Tundu Lissu, endelea na mapambano lakini usiwe too radical najua hiyo ndio tabia yako ya ndani. Sikuambii haya ili kukutia maji, wala kukuogopesha, au kukuepusha na shari, la hasha, nakuambia haya kukukumbusha ukae kwenye mstari na wapambanaji wengine, ukiwaongoza kwa weledi na kadiri.

Don’t forget to be diplomatic and that you are more than an activist! Remember you are a politician and you should know how to play politics for the good of the people.

Tunahitaji Chadema imara yenye umoja na mshikamano! Maridhiano ya vyama vya siasa ndio msingi na mwanzo wa kurudi na kukua kwa demokrasia nchini mwetu. Taratibu yote yatakuwa sawa.

Siasa za mafanikio zina weledi wake. Usiwe mkali mno ukaogopwa hata na rafiki zako! Usiwe mtata mno ukashindwa kueleweka hata na wanachama na viongozi wenzako! Kuwa na kadiri katika misimamo yako, kaa katika mstari na wengine ukijua kuwa hisia za watu zinatofautiana, na pia upo wakati utapata nafasi ya kuongoza na utawajibika kuwasamehe hata wale waliofanya jaribio la kukatisha maisha yako!

Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa uliyopitia umeandika sio tu historia yako mwenyewe, bali historia ya Watanzania wote katika kudai haki na utawala bora. Nakutakia hekima, kadiri na uvumilivu katika harakati za ukombozi wa Taifa letu dhidi ya udhalimu, uzembe na ufisadi.
 
Lissu ni mwanaharakati...sio mwanasiasa wala sio Kiongozi...
Wanaharakati Wana sifa moja ...ubishi wa kubadilika kulingana na nyakati...

Kwenye siasa za majadiliano na maridhiano ..watu radical kama Lissu lazima watapwaya..
 
Lissu ni mroho wa madaraka, hata mambo ya COVID 19 Chadema tunaona sio issue sana, ila kwa kuwa mchepuko wake alikosa nafasi, akaanza kupata kichaa, na kukomaa waondolewe kwenye ubunge.
 
Mheshimiwa Tundu Lissu historia ya vita yako ya kutetea haki na utawala bora Tanzania imeandikwa kwa damu yako mwenyewe, na sina shaka hata kidogo wewe ni mpambanaji wa wapambanaji katika nchi yetu. Kati ya watu wachache wanaoweza kuelezea machungu ya kupigania haki na utawala bora duniani, basi wewe ni mhanga aliye hai na una kila moral authority ya kuelezea jinsi harakati hizo zilivyo ngumu na hatari!

Kwa bahari nzuri pia Mheshimiwa Freeman Mbowe, mwenyekiti wako, naye ni mpambanaji mahiri na yeye pia anajua machungu ya kupambana na walio madarakani, amepitia hatari nyingi, kupoteza mali na fedha nyingi, kupigwa na kufungwa miezi mingi gerezani. Chadema tunajivunia kuwa na viongozi wanaoongoza kwa mifano ya maisha yao wakiwa tayari kumwaga damu zao kusimamia wanachokiamini. Hicho ni kipeo cha juu zaidi cha uongozi na hakuna ujasiri zaidi ya huo!

Mheshimiwa Tundu Lissu, endelea na mapambano lakini usiwe too radical najua hiyo ndio tabia yako ya ndani. Sikuambii haya ili kukutia maji, wala kukuogopesha, au kukuepusha na shari, la hasha, nakuambia haya kukukumbusha ukae kwenye mstari na wapambanaji wengine, ukiwaongoza kwa weledi na kadiri.

Tunahitaji Chadema imara yenye umoja na mshikamano! Maridhiano ya vyama vya siasa ndio msingi na mwanzo wa kurudi na kukua kwa demokrasia nchini mwetu. Taratibu yote yatakuwa sawa.

Siasa za mafanikio zina weledi wake. Usiwe mkali mno ukaogopwa hata na rafiki zako! Usiwe mtata mno ukashindwa kueleweka hata na wanachama na viongozi wenzako! Kuwa na kadiri katika misimamo yako, kaa katika mstari na wengine ukijua kuwa hisia za watu zinatofautiana, na pia upo wakati utapata nafasi ya kuongoza na utawajibika kuwasamehe hata wale waliofanya jaribio la kukatisha maisha yako!

Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa uliyopitia umeandika sio tu historia yako mwenyewe, bali historia ya Watanzania wote katika kudai haki na utawala bora. Nakutakia hekima, kadiri na uvumilivu katika harakati za ukombozi wa Taifa letu dhidi ya udhalimu, uzembe na ufisadi.
Kola kitu kwa kadri! Lakini ukweli usemwe. Maridhiano hakuna kitu. CCM haiwezi kukubali katiba bora, bali bora katiba!
 
Lissu ni mwanaharakati...sio mwanasiasa wala sio Kiongozi...
Wanaharakati Wana sifa moja ...ubishi wa kubadilika kulingana na nyakati...

Kwenye siasa za majadiliano na maridhiano ..watu radical kama Lissu lazima watapwaya..
Ngoja tumkumbushe aweze pia kuwa mwanadiplomasia na mwanasiasa mzuri.
 
Umeandika ujumbe mzuri sana, big up.

Wengi humu ndani kwao Lissu ni malaika, hakosei, hawana uwezo kabisa wa kupima kile anachoongea waone kama kipo sawa au hapana, kwao ilimradi amesema Lissu, ni big - YES.

Mental slavery.
Wewe ukipima anachoongea unapata ngapi ndugu?
 
Lissu na Lema wanakigharimu sana Chama Chao kwa uropokaji japo kwa upande mwingine ni faida kwa Chama tawala

Tangu arudi kila akisimama lazima aharibu, alianza na boda boda, akaja kwny vicoba ma sasa kageukia Ma Sheikh kutangaza kuwa wataenda Motoni na wahuni wataenda Peponi

Kulikuwa na haja gani kudhalilisha Ma Sheikh wetu kuwa wana kula kiti moto hata kama ni kweli kwny Jukwaa la Siasa

Ajifunze kwa Mhitimu wa Havard Colonel Kinana

anajua kuzungumza hata kama ni fix…Wakati wa Jakaya alishambulia sana Serikali ya JK ilipohitajika kushambuliwa hadi kuwaita Mawaziri pendwa kina Shukuru Kawambwa kuwa ni mizigo

Jana kawapanga Jamaa kasema anaenda kupigania Serikali iruhusu kupandisha 'Mshkaki 'kwny boda boda

Siasa ni uongo na kujiepusha na kudhalilisha Jamii fulani kwny mijadala ya kisiasa…ukiweza umemaliza

Hata Nyerere kupitia uongo wake mengi alifanikiwa
 
Back
Top Bottom