Kuna mabadiliko makubwa yatatokea katika kipindi hiki na mojawapo ni ku diffuse tension kwa kuachia watu wazungumze na mikutano ya siasa itaruhusiwa.Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Bwana Tundu Lissu kaondoka Hospital ya Nairobi kuelekea Ubelgiji kwa matibu zaidi baada ya kunusurika kifo kutokana na shambulio la risasi 38 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka uliopita.
Pamoja na mijadala mingi mitandaoni kuwa ni nani kwa hakika alihusika na shambulio lile lakini mhanga mkuu Tundu Lissu hakumung'unya maneno kila alipopata nafasi ya kuongea.
Ameituhumu serikali na mamlaka ya juu kwa kile kinachoitwa 'assassination attempt' jaribio la kutaka kuua....!!!
Kwa serikali zinazojali utawala wa sheria hizi ni tuhuma nzito za aibu na zenye kuitia DOA kubwa serikali kitaifa na kimataifa. Hapa kwetu tunaenda kibongobongo.Fix nyingi siasa nyingi, vitisho na ukatili usio na sababu.
Tangu litokee shambulio lile la Lissu, ambalo aliepuka kifo kwa muujiza tu. Mabadiliko mengi yametokea. Yametokea kwa haraka na kwa muda mfupi ni wazi washambuliaji wake hawakutegemea apone. Kupona kwake ni kihoro na jinamizi kubwa kwao.
Wanamfahamu vema Lissu ni mtukutu, mjanja kwenye siasa na makini kwenye sheria, ana kipawa cha kujenga hoja zikakubalika. Sio mwoga! Haogopi ni msomi mzuri wa sheria na ni mpambanaji asiyeshindwa.
Watesi wake wanatambua vema kuwa risasi zile licha ya kukosa kumnyofoa roho lakini zimeshindwa kabisa kuleta madhara kichwani kwenye injini ya fikra pevu na maarifa.
Wanatambua vema kuwa kwa kipindi chote alichokuwa hospital, licha ya majeraha makubwa aliyopata lakini mwili na akili vimepata mapumziko ya kutosha.
Atarejea kwa nguvu mpya kasi mpya na ari mpya...!!! Na hapa ndio penye kutatiza sana! Sasa hivi jumuiya za kimataifa zinajua fika nini kimempata na nini kimetokea... CV imechafuliwa vibaya kabisa.!!
Mkakati uliopo ni kuanza kutunga sheria za makosa mitandaoni na vyombo vya habari haraka na kuanza kuvichukulia hatua hata kama makosa yenyewe ni mepesi na hayana mashiko.
Kila anachoongea sasa kinarekodiwa na kuhifadhiwa...! Hivi karibuni serikali imesema SI VEMA KUBISHANA NA MGONJWA. ' Anasubiriwa apone...!
Anasubiriwa arudi. Kuna upande hauko tayari kumuona tena anatamalaki jukwaa ni na kwenye vyombo vya habari na mitandaoni..!!
Mashtaka ya uhaini na kukashifu mamlaka yanamsubiri lakini TUTAUKOMBOA WAKATI...!!!!
Hii itasababisha hata atakaporudi mengi yatakuwa tayari yamezungumzwa na joto limeshuka.
Jambo la pili ni kuwa kesi zinazomkabili zimesimama lakini akirudi zitaanza upya na utakuwa ni mwendo wa mahakama moja kwenda nyingine na kwa hulka ya binadamu atachoka mno!!
Jambo la tatu ni hali ya maisha ya wote wanaolalamika nchini,kuna unafuu unakuja na kelele zimesaidia, kwa kuachiwa billions za kulipia madeni ya ndani,mzunguko utaanza kuonekana na kelele za waswahili na usaulifu wao mambo yatakuwa swafiiii.
Pia tusiusahau ule usemi maarufu "Usalama wa watu wengi ni muhimu zaidi kuliko wa mtu mmoja"
Hapa ni kwetu na JPM ndiye Raisi wetu!!