Tundu Lissu kurejea Nchini January 25, 2023

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Tundu Lissu ametangaza kurejea rasmi nchini January 25, 2023 saa 7 mchana baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.

View attachment 2479728

"Hatuwezi kuendelea kuishi uhamishoni bila ukomo. Hivyo basi, ninapenda kuwafahamisha kwamba, panapo majaliwa, nitakanyaga udongo wa ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano ya tarehe 25 Januari, 2023, majira ya saa saba na dakika 35 mchana." amesema

Ameongeza, “Kwa muda huo, ninatarajia kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia nikitokea Brussels, Ubelgiji, kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Nitafurahi sana kwa mapokezi yoyote siku hiyo."

Kuhusu suala la Katiba Mpya, Mhe. Lissu amesema “Kwa vyovyote itakavyokuwa, mwaka huu utakuwa mwaka muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Ni mwaka ambao, kama tukiamua kwa dhati ya mioyo yetu, tutapata Katiba Mpya na ya kidemokrasia, yenye mfumo huru wa uchaguzi, inayojali na kulinda haki za wananchi na inayoweka misingi imara ya uwajibikaji wa viongozi wetu kwa wananchi na wawakilishi wao.”

Anarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu wa 2023, anaamini kwamba, kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu kwa nchi yetu, tutaandika kitabu kizuri.

Mwanasiasa huyo machachari, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki ambae pia ni mwanasheria Nguli nchini alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi za moto na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 wakati vikao vya Bunge vikiendelea Jijini Dodoma.

Pamoja na kutangaza kurejea kwake, bado ameonesha wasiwasi juu ya mambo mbalimbali yasiyo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati huo. Hata hivyo, anaamini kuwa Mungu anaiwazia mema nchi hii.

"Ninafahamu kwamba, licha ya ahadi ya Mheshimiwa Rais na licha ya utayari wangu na wetu, siku zijazo hazitakuwa rahisi. Ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi."

“Mwenyezi Mungu anatuwazia sisi Watanzania “mawazo ya kutustawisha na wala sio ya kutuumiza, mawazo ya kutupa tumaini kwa siku zetu zijazo. Tukiweka nia ya dhati na kuitekeleza kwa dhati, tutayashinda majaribio na magumu yaliyo mbele ya safari yetu."

Chanzo: Twitter Spaces (Tundu Lissu)

Habari mbaya sana hii kwa chawa wa kile chama jingine 😀
 
Lissu kurudi ni jambo jema lakini sio kubwa Sana maana Tz ni kwao, ni nchi aliyopewa na Mungu wake.
Ni jambo kubwa mno kwetu sisi wafuasi na Mashabiki wake...

Kumbuka kuwa huyu ndiye Rais wa JMT aliyechaguliwa kwa sanduku la kura halali Oktoba, 2020 lakini hakutangazwa tu na NEC na badala yake kwa hila akatangazwa yule muuaji wa CCM (Magufuli) na tayari yeye ndo hivyo tena, keshatangulia kufa...!!

Cha ajaabu eti unamshauri Tundu Lissu akaabudu kaburi la "ALIYEKWISHA KUFA" huko CHATO..!!

You're possibly out of your mind au hujui unasema nini...!

Jambo kubwa ambako akifanikiwa kulifanya ni Kutangaza hadharani kumsamehe Marehemu Mwendazake na wote waliotaka kumdhulumu uhai.
Msamaha si lazima utamkwe hadharani. Na msamaha ni kati ya mtu personal na Mungu wake..

Lakini jambo moja lililo KWELI na HAKIKA ni kuwa, kusameheana wanadamu ni agizo la Mungu wetu aliye hai...
Sambamba na msamaha huo, apange kwenda kutembea Chatho, akaone makaburi ya watu maarufu pamoja na kumsalimu Janeth. That will mean and attract love and set a reference point in humanity
Nyie huko CCM kama huwa mnaabudu makaburi ya wafu, shauri lenu...

Hakuna uhusiano kati ya walio hai na wafu....

Tundu Lissu knows this more than you can imagine...!!
 
Nashukuru umelitambua kuwa Lissu alikosewa na sasa unataka awasamehe waliomkosea. Lissu afanyi kwa ajili yake bali anafanya kwa ajili ya wataka haki wote, hivyo ni vyema familia ya aliyemkosea Lissu ndio imuombe Lissu msamaha ili iwe fundisho kwa wengine. Pia swala la laana lipo pale pale kama mtashupaza shingo basi laana hiyo itatembea kwa vizazi kadhaa.

Swala la Lissu lipewe uzito wake na tusilichukulie kwa wepesi hata kidogo. Waliopanga na kushiriki Lissu kupigwa risasi ni lazima wafahamike mchana kweupe na haitajalisha ni muda gani utapita.
Watanganyika wapi! labda tumbo lake; aliyekuwa akimpinga Magufuli kwa vitisho vikali,mala tutanyolewa na vipande vya chupa pasipo maji,mala tutashitakiwa Miga mpaka nchi itafiliska,kumbe alikuwa ameisha vuta mpunga kwa akina accecia.Kama Sio kiburi cha Magufuli accecia bado wangelikuwa wanatamba mjini.
 
JamiiForums1327454580.jpg
 
Mwitikio bado ni mdogo sana wapinzani wapambane sana kurudisha lile vibe la Dr Slaa.

Rais wa awamu ile aliwasakama sana kupita kiasi.

Ilisemekana alitaka kuufuta
kabisa nchini.

Lakini kumbe Upinzani uko ndani ya mioyo ya watu.

Sasa werevu wanajiuliza iwapo alikuwa na nia thabiti ya kweli ya uadilifu Kwanini alichukia upinzani?

Je mbona ilipaswa kushirikiana nao kufanya kazi na kuwatumia Kama watch dogs ?

Je jamaa si wangetumika kumstua mahala Penye upigaji ambapo yamkini yeye angekuwa bado hajafahamu?
 
Wale wote aliowachukua jiwe ni wabunge ambao walikubali kujivua sifa ya upinzani na kuvalishwa uhalisia wa wana ccm
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Tundu Lissu ametangaza kurejea rasmi nchini January 25, 2023 saa 7 mchana baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.

View attachment 2479728

"Hatuwezi kuendelea kuishi uhamishoni bila ukomo. Hivyo basi, ninapenda kuwafahamisha kwamba, panapo majaliwa, nitakanyaga udongo wa ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano ya tarehe 25 Januari, 2023, majira ya saa saba na dakika 35 mchana." amesema

Ameongeza, “Kwa muda huo, ninatarajia kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia nikitokea Brussels, Ubelgiji, kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Nitafurahi sana kwa mapokezi yoyote siku hiyo."

Kuhusu suala la Katiba Mpya, Mhe. Lissu amesema “Kwa vyovyote itakavyokuwa, mwaka huu utakuwa mwaka muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Ni mwaka ambao, kama tukiamua kwa dhati ya mioyo yetu, tutapata Katiba Mpya na ya kidemokrasia, yenye mfumo huru wa uchaguzi, inayojali na kulinda haki za wananchi na inayoweka misingi imara ya uwajibikaji wa viongozi wetu kwa wananchi na wawakilishi wao.”

Anarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu wa 2023, anaamini kwamba, kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu kwa nchi yetu, tutaandika kitabu kizuri.

Mwanasiasa huyo machachari, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki ambae pia ni mwanasheria Nguli nchini alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi za moto na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 wakati vikao vya Bunge vikiendelea Jijini Dodoma.

Pamoja na kutangaza kurejea kwake, bado ameonesha wasiwasi juu ya mambo mbalimbali yasiyo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati huo. Hata hivyo, anaamini kuwa Mungu anaiwazia mema nchi hii.

"Ninafahamu kwamba, licha ya ahadi ya Mheshimiwa Rais na licha ya utayari wangu na wetu, siku zijazo hazitakuwa rahisi. Ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi."

“Mwenyezi Mungu anatuwazia sisi Watanzania “mawazo ya kutustawisha na wala sio ya kutuumiza, mawazo ya kutupa tumaini kwa siku zetu zijazo. Tukiweka nia ya dhati na kuitekeleza kwa dhati, tutayashinda majaribio na magumu yaliyo mbele ya safari yetu."

Chanzo: Twitter Spaces (Tundu Lissu)
karibu rais wawa nyonge mzimu ulisha kufa usihofu
 
Siasa outdated hizi, ww lazima utakuwa ni mzee ndio maana unaendekeza hizi propaganda outdated. Waambie kabila lenu nao waanzishe chama.
Huyo jamaa namjua kwao ni kibaigwa pale Nazareti
 
Watanganyika wapi! labda tumbo lake; aliyekuwa akimpinga Magufuli kwa vitisho vikali,mala tutanyolewa na vipande vya chupa pasipo maji,mala tutashitakiwa Miga mpaka nchi itafiliska,kumbe alikuwa ameisha vuta mpunga kwa akina accecia.Kama Sio kiburi cha Magufuli accecia bado wangelikuwa wanatamba mjini.

..magufuli aliwadai acacia usd 191 billion.

..acacia wakakimbilia ktk mahakama ya kimataifa.

..barrick ambao ni wamiliki wa acacia wakaingilia kati.

..magufuli akanywea na kukubali kulipwa kidogo-kidogo kishika uchumba usd 300.

..baadae magufuli akasaini mkataba na barrick na kiwango cha kishika kikapunguzwa.

..wakati wa uchaguzi magufuli akampa ubunge Deo Mwanyika aliyekuwa makamu wa raisi wa acacia / barrick.

..kwa msingi huo Lissu alikuwa sahihi. Kwanza tulishtakiwi. Pili hatukulipwa usd 191 billion.
 
Shetani ana nguvu sana hapa duniani kwa wanaotanguliza matumbo. Kuna € m50 imetolewa, lazima ionekane kazi inafanyika.
 
"Sikutoa salamu za mwaka sababu M/Kiti alikua na kikao na Rais @SuluhuSamia baada ya kikao nimeridhika Rais anania njema na Taifa letu, natangaza 25 Jan, 2023 itakua J/tano nitarudi Tanzania kufanya kazi ya demokrasia na Rais Samia" - Tundu Lissu

Mwisho wa kunukuuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom