Tundu Lissu kurejea Nchini January 25, 2023

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Tundu Lissu ametangaza kurejea rasmi nchini January 25, 2023 saa 7 mchana baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.

2263138A-7099-4019-B526-FEAEC20D5679.jpeg

"Hatuwezi kuendelea kuishi uhamishoni bila ukomo. Hivyo basi, ninapenda kuwafahamisha kwamba, panapo majaliwa, nitakanyaga udongo wa ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano ya tarehe 25 Januari, 2023, majira ya saa saba na dakika 35 mchana." amesema

Ameongeza, “Kwa muda huo, ninatarajia kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia nikitokea Brussels, Ubelgiji, kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Nitafurahi sana kwa mapokezi yoyote siku hiyo."

Kuhusu suala la Katiba Mpya, Mhe. Lissu amesema “Kwa vyovyote itakavyokuwa, mwaka huu utakuwa mwaka muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Ni mwaka ambao, kama tukiamua kwa dhati ya mioyo yetu, tutapata Katiba Mpya na ya kidemokrasia, yenye mfumo huru wa uchaguzi, inayojali na kulinda haki za wananchi na inayoweka misingi imara ya uwajibikaji wa viongozi wetu kwa wananchi na wawakilishi wao.”

Anarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu wa 2023, anaamini kwamba, kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu kwa nchi yetu, tutaandika kitabu kizuri.

Mwanasiasa huyo machachari, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki ambae pia ni mwanasheria Nguli nchini alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi za moto na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 wakati vikao vya Bunge vikiendelea Jijini Dodoma.

Pamoja na kutangaza kurejea kwake, bado ameonesha wasiwasi juu ya mambo mbalimbali yasiyo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati huo. Hata hivyo, anaamini kuwa Mungu anaiwazia mema nchi hii.

"Ninafahamu kwamba, licha ya ahadi ya Mheshimiwa Rais na licha ya utayari wangu na wetu, siku zijazo hazitakuwa rahisi. Ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi."

“Mwenyezi Mungu anatuwazia sisi Watanzania “mawazo ya kutustawisha na wala sio ya kutuumiza, mawazo ya kutupa tumaini kwa siku zetu zijazo. Tukiweka nia ya dhati na kuitekeleza kwa dhati, tutayashinda majaribio na magumu yaliyo mbele ya safari yetu."

Chanzo: Twitter Spaces (Tundu Lissu)
 
Lissu kurudi ni jambo jema lakini sio kubwa Sana maana Tz ni kwao, ni nchi aliyopewa na Mungu wake.

Jambo kubwa ambako akifanikiwa kulifanya ni Kutangaza hadharani kumsamehe Marehemu Mwendazake na wote waliotaka kumdhulumu uhai.

Sambamba na msamaha huo, apange kwenda kutembea Chatho, akaone makaburi ya watu maarufu pamoja na kumsalimu Janeth. That will mean and attract love and set a reference point in humanity
 
Lissu kurudi ni jambo jema lakini sio kubwa Sana maana Tz ni kwao, ni nchi aliyopewa na Mungu wake.
Jambo kubwa ambako akifanikiwa kulifanya ni Kutangaza hadharani kumsamehe Marehemu Mwendazake na wote waliotaka kumdhulumu uhai. Sambamba na msamaha huo, apange kwenda kutembea Chatho, akaone makaburi ya watu maarufu pamoja na kumsalimu Janeth. That will mean and attract love and set a reference point in humanity
Wewe ungeweza?

Unajua kapitia mangapi aisee, umewahi kuona ile miguu yake siku hizi?

By the way kwanini amsamehe? Why yaani? Unamsameeje mtu aliyekupitisha magumu vile aisee? Hapana, hebu msilazimishe vitu visivyotakiwa
 
Lissu kurudi ni jambo jema lakini sio kubwa Sana maana Tz ni kwao, ni nchi aliyopewa na Mungu wake.
Jambo kubwa ambako akifanikiwa kulifanya ni Kutangaza hadharani kumsamehe Marehemu Mwendazake na wote waliotaka kumdhulumu uhai. Sambamba na msamaha huo, apange kwenda kutembea Chatho, akaone makaburi ya watu maarufu pamoja na kumsalimu Janeth. That will mean and attract love and set a reference point in humanity
Ni wakati muafaka wakupata wahalifu wote walio taka kutoa Roho yake,na sisi kwa yeye tu,na wote waliyoteswa enzi za Mwendazake
 
Back
Top Bottom