Tundu Lissu: Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru

Whether u like it or not: sisi wananchi tulio wengi tunapoteza imani kila siku zinavyokwenda. Hivyo kwa kiasi kikubwa hatutokaa foleni kubariki najisi itayofanywa. Sababu kubwa kama hizi za mh Lissu vyama vya upinzani hamko tayarikuunganisha nguvu (alliance). Na njia kepee ya kuunganisha alience ni kwa kuuwa vyama vyote vilivyopo na kuwa na chama kipya kikuu cha upinzani.

Mko tayari kusikiliza kilio cha wananchi au mpo tayari kusikiliza matumbo yenu.
Chama kikuu kimoja cha upinzani? You mean kuungana na akina Cheyo, Mrema, Lipumba, Shibuda nk. You must be joking.
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
swali la msingi si aina ya matokeo bali tume ipo huru???
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
Mkuu mbona umekurupuka? Soma vizuri uzi haya sio mashindano ya kuwahi kujibu punguza papara za Lumumba buku 7 utapata
 
Nadhani sio sahihi kulinganisha shuguli za kila siku za vyama vya siasa na tukio moja la uchaguzi katika miaka mitano (one event in a five year period).
Shughuli zote za mapambano ya kisiasa kupitia maandamano ya amani, magazeti, mikutano ya hadhara nk ni maandalizi kuelekea siku moja ya UCHAGUZI.

Kwahiyo 'KUSHIRIKI UCHAGUZI' ni event inyohitimisha na kudhihirisha uwepo haki na uhalali wa democracy katika mfumo mzima wa kisiasa nchini.

Pili ni makosa kusema upinzani walipanga kutoshiriki UCHAGUZI. Kwasababu wagombea wao waliondolewa, full stop!
Ni kama gazeti lako likifungiwa halafu mtu aseme umejiamulia kufunga gazezi lako mwenyewe!

Ubaya wa mada hizi zinazoletwa hapa kwa niaba ya Lissu huwa hazina mrejesho. Haileleweki kama mwanzilishi wa mawazo yanayojadiliwa hapa huwa anapata fursa naye apitie mawazo ya waliochangia mada yake.

Najua ubovu wa Jukwaa hili la JF, unakutana na kila aina ya majibu, hasa yale '"infatille" kutoka kwa wanaCCM waliopewa kazi ya kupitia jukwaani na kudondosha kinyesi kila sehemu..

Lakini nawaza, kwa mfano, mchango huu wa mkuu 'shoctopus' - kauweka kwa kutumia maneno machache sana, lakini yanayotengeneza hoja nzuri na ya kufikirisha, na ambayo pengine ingestahili mleta mada akaisoma, na kwa aina anayoweza akaichangia na kuipanua zaidi.


Badala yake, mawazo kama haya, yamefutikwa na yasionekane ndani kwa ndani kabisa #43, kurasa za ndani hata yasionekane.

Hii habari ya kususa uchaguzi haina maana kabisa, kwa sababu ndiyo wanayoitafuta CCM.


Lakini unapoacha kususa, na njia zako zote za kupambana zikawa zinazibwa moja baada ya nyingine hata usiweze kufurukuta; hali hiyo pia inakuweka katika mwonekano ule ule wa kususa.

Kwa sababu huwezi ukategemea matokeo mazuri wakati 'viwanja vyako' vyote vya michezo vimechimbwa mahandaki.

Mimi mawazo yangu siku zote yapo kwa wananchi. Huu ndio uwanja pekee ambao hata CCM wanatambua kwamba ukijaribu kuchimba mahandaki huko hutofanikiwa.

Rai yangu ni kuwa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani, baada ya viwanja vyao vya kawaida kuharibiwa, wangeelekeza nguvu zao zote huko kwa wananchi.

Juzi tu tuliona mwitikio wa ajabu kutoka kwa wananchi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa. Hawa wananchi baada ya kuonyesha mwelekeo wao huo, ni jukumu la vyama hivi kutafuta njia bora na sahihi za kuwawezesha wananchi hawa kutimiza adhma yao ya kufanya wanayotaka yafanyike ili kuleta mabadiliko katika haya wasiyoyapenda.

Sioni dalili zozote toka kwenye vyama hivi kwamba haya yanafanyika. Hili ndilo linalosikitisha zaidi.

Ili kuondoa 'vagueness' katika bandiko langu hili na kuonekana kutoeleweka, nasema hivi 'specifically:

Vyama vya upinzani wakati huu vingetakiwa viwe vijijini vikifanya kazi na wananchi huko huko vijijini.

Sizungumzii Mbowe na Mashinji wahamie vijijini. Vyama vina wanachama wao huko huko vijijini na viongozi wa ngazi za huko huko vijijini. Wawezesheni kwa kuwapa elimu na mbinu za kuwashawishi wananchi wenzao.

Acheni ubahiri, ruzuku mnazopewa zitumieni kunakohitajika kuvijenga vyama vyenu; huko huko vijijini.

Siasa za majukwaani mlikatazwa, hakuna atakayeweza kukataza siasa za mtu kwa mtu, mlango kwa mlango, klabu ya pombe na klabu ya pombe.

Mwalimu Nyerere aliachia uwaziri mkuu, akaenda kujenga chama kwa wananchi, na matokeo yalionekana.

Sitasema 'acheni lelemama', kwa sababu najua hamna lelemama mnayoifaidi hapo. Mpo kwenye maumivu makali. Lakini itakuwa haki yenu kuyapata hayo maumivu kama hamtaki kuwafikia wenye uwezo wa kuyaondoa hayo maumivu yenu na kuwasihi wawaondolee maumivu hayo; ambao ni 'uwanja' usioweza kuchimbwa mahandaki.
 
Prof safari ni kama ametemwa kiana kwa sababu anaongea kuikomoa chadema na kujionyesha kwamba yeye safari ndio mtu pekee mwenye mawazo jengefu pale chadema.
 
Hakika tundu lisu ndie mtu pekee alie baki na alie teuliwa na mungu kama mtetezi wa wanyonge na sio huyo anae jivika nghozi ya kondoo kumbe chui.
 
Lissu anamjibu Prof Safari kiaina! Lissu, kwa yanayoendelea Chadema sasa alafu unaishia kudakia hoja kama hii unaanza kufanya uonekane wale wale team Mbowe!

Kubaki na heshima yako ni bora ukosoe wazi mwenendo wa chama hasa upande wa democracy au ukae kimya ukiendelea kurejesha afya yako.

Otherwise siku moja utakaa kwenye kona moja kujaribu kuweka sawa hili hata kama utakuwa nje ya Chadema!

Kosoa wewe....

Iweje utake macho ya mwenzio, masikio ya mwenzio na kichwa cha mwenzio kiwe chako??

Ana namna yake ya kutazama na kuyaona mambo....

Wewe kama unaona tofauti na aonavyo mwenzako, toa hoja ijadiliwe!!
 
Kosoa wewe....

Iweje utake macho ya mwenzio, masikio ya mwenzio na kichwa cha mwenzio kiwe chako??

Ana namna yake ya kutazama na kuyaona mambo....

Wewe kama unaona tofauti na aonavyo mwenzako, toa hoja ijadiliwe!!
Ningekuwa na uwezo ningemshika masikio na pua, nihakikishe amefika hapa na kusoma ujumbe huu makini uliompa.

Huyo ni mmoja kati ya watu wanaostahili jibu kama hilo.
 
ukipata watu kama 10 wa sampuli hii na ukaamua kuwatumia vilivyo kusugua bongo zao - hii nchi lazima isonge mbele na hao wakamata ndege zetu na wazee wa makinikia hutawasikia tena.
Vibaraka wao, wawasumbue kwa nn
 
Sasa subiri uchaguz mwakani. We tundu lissu ivi unayafaham masisiem yasivyo nahaya yatakomba majimbo yote labda yataliacha la cuf moja hapo ndotajua umuhimu wa kupigania tume huru kwa sasa.. We endeleeni na ngonjera zenu. Af mkiibuwa mje kutuambia tukaandamane yaan nitamtukana tusi moja tuu ambalo nitapigwa ban karne moja
Sasa wakifanya hivyo ccm, tatizo ni la Lisu?!
Wangapi wanefanya ya kuhujumu demokrasia, tunamlaumu Lisu pia?!

Mimi nashauri baada ya ku exhaust majukwaa yote wajaribu na lile la MSITUNI sasa kama Kagame na RPF take walijaribu sasa wana kula bata.
 
Sasa wakifanya hivyo ccm, tatizo ni la Lisu?!
Wangapi wanefanya ya kuhujumu demokrasia, tunamlaumu Lisu pia?!

Mimi nashauri baada ya ku exhaust majukwaa yote wajaribu na lile la MSITUNI sasa kama Kagame na RPF take walijaribu sasa wana kula bata.
Hili unalopendekeza kwa sasa hivi haliwezekani bila ya kuwa na wananchi nyuma yao.

Hata mimi siungi mkono hoja ya Tundu Lissu, lakini naelewa anachokisema.

Wapinzani wamekabwa kotekote, Mahakamani, Bungeni, Kwenye kufanya kazi zao za kisiasa, kama kufanya mikutano; mawazo yao hayawezi kusambazwa kwa wananchi na vyombo huru vya habari, n.k, n.k.

Kwa hiyo, hata kupigania 'Tume Huru ya Uchaguzi' iwepo kabla ya uchaguzi mwakani, hilo haliwezi likatokea bila ya kuwalazimisha wanaolikataa, wakubali (kwa kulazimishwa).

Ni nani mwenye uwezo wa kulazimisha: Wananchi wakitaka liwepo, litakuwepo, hilo ninalo uhakika wa asilimia.
Lakini wananchi wanahitaji uongozi wa kusimamia hilo.


Kama Tundu Lissu anaamini kuwa 'kususia' ni kwa vyama vya siasa kujitoa kwa hiari yao kama walivyojitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, basi inamlazimu atambue pia kwamba vyama hivyo vinalazimishwa 'kujitoa/kususia' huku wao wakidhani hawakususa.

Unabaki na kushiriki kwenye uchaguzi ambao unajua wazi huwezi kushinda, huko sio kujitoa kwenye mapambano?
 
Back
Top Bottom