Tundu Lissu: Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
FB_IMG_1575449548659.jpg

Kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi. Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru.

Kwamba tumeridhika na viubunge na viudiwani tunavyopata every five years, etc. Kwamba ili tuweze kushinda na kuchukua dola lazima tuache kushiriki uchaguzi hadi hapo tutakapopata Tume Huru, etc.

Hoja hii ni potofu.

Tume Huru ya Uchaguzi haipatikani nje ya mapambano mapana ya kutafuta demokrasia katika nchi yetu. Tume Huru ni sehemu tu ya tatizo la msingi la nchi yetu: tatizo la ukosefu wa demokrasia.

Tume ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa Katiba iliyopo. Inafanya kazi, by and large, kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizopo.

Kupigania Tume Huru maana yake ni kupigania Katiba Mpya; au angalau marekebisho ya Katiba iliyopo. Haiwezekani kupigania Tume Huru au marekebisho ya Katiba ya sasa in vacuo; inapiganiwa katika mazingira halisi ya kisiasa, kikatiba/kisheria na kitaasisi tunamoishi.

Kwa maneno mengine, ili upiganie Tume Huru lazima uwe na jukwaa la kusimamia. Iwe Bunge, au vyombo vya habari au mikutano ya hadhara, au kuchukua silaha na kwenda 'msituni', etc. Yote hayo ni majukwaa.

Sasa hoja ni je, tutumie jukwaa gani ili kupata Tume Huru??? Tukiacha kushiriki uchaguzi, tunabakia na jukwaa gani la kudai Tume Huru??? Mazingira ya vyombo vya habari, kama jukwaa la mapambano, ni rafiki na wezeshi kiasi gani??? Mikutano ya hadhara, jukwaa lingine muhimu, ni rafiki na wezeshi kiasi gani???

Ukiachia hii miaka ya Magufuli, je, mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani imekuwa mirahisi kiasi gani siku za nyuma kama majukwaa ya kudai demokrasia na Tume Huru???

Ukiachia wakati huu, vyombo vya habari vimekuwa rahisi kiasi gani kama majukwaa ya kidemokrasia??? Vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa rafiki na wezeshi kiasi gani katika madai yetu ya demokrasia na Tume Huru???

Ukweli ni kwamba maeneo yote haya yamekuwa na matatizo. Lakini hatujaacha kutumia fursa kidogo zilizokuwapo kudai demokrasia zaidi.

Hatuna uhuru wa vyombo vya habari sasa kuliko ilivyokuwa kabla ya Magufuli. Kuna matatizo mengi kwenye eneo hili kuliko zamani.

Lakini hakuna mtu anayedai vyombo vyetu vya habari viache kukusanya, kuandika na kusambaza habari hadi hapo tutakapopata uhuru kamili wa habari. Vyombo hivyo vinaendelea kufanya kazi zao katika mazingira halisi yaliyopo huku vikiendelea kudai uhuru wa habari.

Vivyo hivyo na sisi tunapaswa kuendelea kudai Tume Huru katika mazingira halisi ya kiuchaguzi yaliyopo.

Hatuwezi kususia jukwaa muhimu kama Bunge, licha ya matatizo yake mengi yaliyopo, unless jukwaa hilo lifungwe kabisa. Hatuwezi kususia uchaguzi, unless jukwaa la uchaguzi lifungwe kabisa, kama ilivyotokea majuzi kwenye uchaguzi wa mitaa na vijiji.

Mjadala huu unanikumbusha mjadala wa 'Mageuzi au Mapinduzi' ('Reform or Revolution') kati ya wanamapinduzi wa kijamaa wa Ulaya zaidi ya miaka mia moja iliyopita.

Wenye 'msimamo mkali' wa kimapinduzi walikuwa wanadai hakuna kushiriki harakati za kimageuzi kama vile mapambano ya kibunge; tufanye mapinduzi kwanza, etc.

Wengine wenye 'msimamo vuguvugu' wakidai kilele cha mapinduzi kinafikiwa kwa njia ya mageuzi ya kiuchaguzi, etc. Lenin aliwatuhumu wenye msimamo mkali kuwa wanasumbuliwa na 'ugonjwa wa utoto' ('an infantile disorder'!!!)

Na sisi pia hatutakiwi kuwa na ugonjwa huo. Kila jukwaa la mapambano ya kidemokrasia ni muhimu litumike. Kutumia njia mojawapo tu haitaleta matunda. Tunahitaji kutumia fursa zote zilizopo.
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
 
Bravo Lissu, Mwanzilishi wa hoja hii majuzi kati wakati wa press yake hakufafanua ni jukwaa lipi angetumia kudai hiyo Tume huru yake ya uchaguzi? na mbaya zaidi waliokuwa wanamhoji hawakumwuliza swali hilli la msingi kabisa, sasa sijui kwa kusahau au kwa kutokujua kwao... anyway ndiyo waandishi wetu wa siku hizi.

Lakini pointi inabakia palepale kwamba ukisusa uchaguzi maana yake hutaki tena kutumia jukwaa la Kibunge, Je kuna jukwaa lipi lenye unafuu ambalo unaweza kutumia kwenye harakati zako za kuidai hiyo Tume huru ya uchaguzi kati ya hizo alizodadavua nguli wa Siasa / Sheria nchini.?
 
Sasa subiri uchaguz mwakani. We tundu lissu ivi unayafaham masisiem yasivyo nahaya yatakomba majimbo yote labda yataliacha la cuf moja hapo ndotajua umuhimu wa kupigania tume huru kwa sasa.. We endeleeni na ngonjera zenu. Af mkiibuwa mje kutuambia tukaandamane yaan nitamtukana tusi moja tuu ambalo nitapigwa ban karne moja
 
Huyu jamaa Mungu amembariki sana kiakili,kiuwezo wa kupangilia hoja na kiuwasilishaji wa hoja. Kama mtu hukubaliani na hoja zake,ni ngumu sana kuweza kumpinga kwa hoja zaidi ya viroja.
Kongole Tundu.
ukipata watu kama 10 wa sampuli hii na ukaamua kuwatumia vilivyo kusugua bongo zao - hii nchi lazima isonge mbele na hao wakamata ndege zetu na wazee wa makinikia hutawasikia tena.
 
Tume huru tunayoitaka ni ile inayoamuru maafisa watendaji wa vijiji na kata kuwaondoa wagombea wa upinzani ili kukidhi matakwa ya dikteta Meko.
 
Whether u like it or not: sisi wananchi tulio wengi tunapoteza imani kila siku zinavyokwenda. Hivyo kwa kiasi kikubwa hatutokaa foleni kubariki najisi itayofanywa. Sababu kubwa kama hizi za mh Lissu vyama vya upinzani hamko tayarikuunganisha nguvu (alliance). Na njia kepee ya kuunganisha alience ni kwa kuuwa vyama vyote vilivyopo na kuwa na chama kipya kikuu cha upinzani.

Mko tayari kusikiliza kilio cha wananchi au mpo tayari kusikiliza matumbo yenu.
 
Lissu anamjibu Prof Safari kiaina! Lissu, kwa yanayoendelea Chadema sasa alafu unaishia kudakia hoja kama hii unaanza kufanya uonekane wale wale team Mbowe!

Kubaki na heshima yako ni bora ukosoe wazi mwenendo wa chama hasa upande wa democracy au ukae kimya ukiendelea kurejesha afya yako.

Otherwise siku moja utakaa kwenye kona moja kujaribu kuweka sawa hili hata kama utakuwa nje ya Chadema!
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
Sikujua kama we jamaa ni mjinga kiasi hiki !
 
....wewe sijui utakuwa mkimbizi toka nchi gani!
 
Lissu anamjibu Prof Safari kiaina! Lissu, kwa yanayoendelea Chadema sasa alafu unaishia kudakia hoja kama hii unaanza kufanya uonekane wale wale team Mbowe!

Kubaki na heshima yako ni bora ukosoe wazi mwenendo wa chama hasa upande wa democracy au ukae kimya ukiendelea kurejesha afya yako.

Otherwise siku moja utakaa kwenye kona moja kujaribu kuweka sawa hili hata kama utakuwa nje ya Chadema!
...hutaki atoe maoni yake sio, unataka afunge mdomo ili wewe na wenzako muendelee kupiga makelele yenu Mbowe dikteta sijui na nini!, kama Mbowe huwa anajiteua mwenyekiti peke yake!, wacha ushamba.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom