Tundu Lissu: Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru

Hao CCM ndio waliowawekea kifungu cha Tume huru ya Uchaguzi kwenye katiba pendekezwa na Bunge la katiba, ulitaka wafanye nini wawabebe mgongoni? Wapinzani waling'ang'ana na Tunu za Taifa wakasahau kuna vifungu chanya ambavyo vingesaidia kuanza na safari ya mabadiliko. Soma kifungu hicho 211.

SEHEMU YA PILI
TUME HURU YA UCHAGUZI
(a) Tume Huru ya Uchaguzi
Kuundwa kwa
Tume Huru ya
Uchaguzi
211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya
Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa
kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi
watakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa, na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa
Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na
ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka
mitano;
(c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii;
(d) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
(6) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa
mujibu wa sheria; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
(7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya
kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi:
(a)
Tulikua na lengo la kuandika katiba ya nchi siyo kufurahisha wapinzani wala nini. Wewe kwa Akili yako uliona kipengele hicho ndo kilikua muhimu kwa nchi yetu ndani ya Hayo mapendekezo ? au Ulitaka wakubaliane na uwepo wa Tume huru ili waingie madarakani na sehemu zingine zikiwa vibovu ?

Nyie ndo Wale wanaodhani wapinzani ndo wanaumizwa kumbe laa..Polisi walikua wakiwakimbiza akina Katambi..Machali..Kafulila...Silaa..Waitara lakini leo ndo wanawapigia saruti na maisha yao na familia yao bado yamebaki pale pale na shida zao.

Mnashauriwa na wanasiasa mdai katiba mpya kwa ajili ya vizazi vyenu Ila mnabaki kukenua meno kua mlipewa Hiki mkaacha..Mbowe hana cha kupoteza bali nchi ndo ina cha kupoteza. Wapinzani ni daraja tu kama daraja la mkapa kuwavusha.
Ujitambui kabisa ;
 
Huyu jamaa Mungu amembariki sana kiakili,kiuwezo wa kupangilia hoja na kiuwasilishaji wa hoja. Kama mtu hukubaliani na hoja zake,ni ngumu sana kuweza kumpinga kwa hoja zaidi ya viroja.
Kongole Tundu.
Yaani kuna li Shetani moja kilaza likapanga kumuua huyu Jamaa...
 
Back
Top Bottom