Tundu Lissu: Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru

Uzuri wengine tulikuwa tunawesema hivi hivi NCCR wanatuona maboya! Sasa Chadema itakuwa worse kuliko NCCR.
...utabiri ulisomea wapi!

CDM kupotezwa kwenye ramani ya siasa za tz itasababishwa na rafu wanazochezewa wapinzani na chama tawala, pamoja na nguvu ya polisi na tume ya uchaguzi kukibeba chama tawala, lakini sio kwa kuchokwa na wananchi.
 
Kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi. Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru.

Kwamba tumeridhika na viubunge na viudiwani tunavyopata every five years, etc. Kwamba ili tuweze kushinda na kuchukua dola lazima tuache kushiriki uchaguzi hadi hapo tutakapopata Tume Huru, etc.

Hoja hii ni potofu.

Tume Huru ya Uchaguzi haipatikani nje ya mapambano mapana ya kutafuta demokrasia katika nchi yetu. Tume Huru ni sehemu tu ya tatizo la msingi la nchi yetu: tatizo la ukosefu wa demokrasia.

Tume ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa Katiba iliyopo. Inafanya kazi, by and large, kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizopo.

Kupigania Tume Huru maana yake ni kupigania Katiba Mpya; au angalau marekebisho ya Katiba iliyopo. Haiwezekani kupigania Tume Huru au marekebisho ya Katiba ya sasa in vacuo; inapiganiwa katika mazingira halisi ya kisiasa, kikatiba/kisheria na kitaasisi tunamoishi.

Kwa maneno mengine, ili upiganie Tume Huru lazima uwe na jukwaa la kusimamia. Iwe Bunge, au vyombo vya habari au mikutano ya hadhara, au kuchukua silaha na kwenda 'msituni', etc. Yote hayo ni majukwaa.

Sasa hoja ni je, tutumie jukwaa gani ili kupata Tume Huru??? Tukiacha kushiriki uchaguzi, tunabakia na jukwaa gani la kudai Tume Huru??? Mazingira ya vyombo vya habari, kama jukwaa la mapambano, ni rafiki na wezeshi kiasi gani??? Mikutano ya hadhara, jukwaa lingine muhimu, ni rafiki na wezeshi kiasi gani???

Ukiachia hii miaka ya Magufuli, je, mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani imekuwa mirahisi kiasi gani siku za nyuma kama majukwaa ya kudai demokrasia na Tume Huru???

Ukiachia wakati huu, vyombo vya habari vimekuwa rahisi kiasi gani kama majukwaa ya kidemokrasia??? Vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa rafiki na wezeshi kiasi gani katika madai yetu ya demokrasia na Tume Huru???

Ukweli ni kwamba maeneo yote haya yamekuwa na matatizo. Lakini hatujaacha kutumia fursa kidogo zilizokuwapo kudai demokrasia zaidi.

Hatuna uhuru wa vyombo vya habari sasa kuliko ilivyokuwa kabla ya Magufuli. Kuna matatizo mengi kwenye eneo hili kuliko zamani.

Lakini hakuna mtu anayedai vyombo vyetu vya habari viache kukusanya, kuandika na kusambaza habari hadi hapo tutakapopata uhuru kamili wa habari. Vyombo hivyo vinaendelea kufanya kazi zao katika mazingira halisi yaliyopo huku vikiendelea kudai uhuru wa habari.

Vivyo hivyo na sisi tunapaswa kuendelea kudai Tume Huru katika mazingira halisi ya kiuchaguzi yaliyopo.

Hatuwezi kususia jukwaa muhimu kama Bunge, licha ya matatizo yake mengi yaliyopo, unless jukwaa hilo lifungwe kabisa. Hatuwezi kususia uchaguzi, unless jukwaa la uchaguzi lifungwe kabisa, kama ilivyotokea majuzi kwenye uchaguzi wa mitaa na vijiji.

Mjadala huu unanikumbusha mjadala wa 'Mageuzi au Mapinduzi' ('Reform or Revolution') kati ya wanamapinduzi wa kijamaa wa Ulaya zaidi ya miaka mia moja iliyopita.

Wenye 'msimamo mkali' wa kimapinduzi walikuwa wanadai hakuna kushiriki harakati za kimageuzi kama vile mapambano ya kibunge; tufanye mapinduzi kwanza, etc.

Wengine wenye 'msimamo vuguvugu' wakidai kilele cha mapinduzi kinafikiwa kwa njia ya mageuzi ya kiuchaguzi, etc. Lenin aliwatuhumu wenye msimamo mkali kuwa wanasumbuliwa na 'ugonjwa wa utoto' ('an infantile disorder'!!!)

Na sisi pia hatutakiwi kuwa na ugonjwa huo. Kila jukwaa la mapambano ya kidemokrasia ni muhimu litumike. Kutumia njia mojawapo tu haitaleta matunda. Tunahitaji kutumia fursa zote zilizopo.
Nadhani sio sahihi kulinganisha shuguli za kila siku za vyama vya siasa na tukio moja la uchaguzi katika miaka mitano (one event in a five year period).
Shughuli zote za mapambano ya kisiasa kupitia maandamano ya amani, magazeti, mikutano ya hadhara nk ni maandalizi kuelekea siku moja ya UCHAGUZI.
Kwahiyo 'KUSHIRIKI UCHAGUZI' ni event inyohitimisha na kudhihirisha uwepo haki na uhalali wa democracy katika mfumo mzima wa kisiasa nchini.
Pili ni makosa kusema upinzani walipanga kutoshiriki UCHAGUZI. Kwasababu wagombea wao waliondolewa, full stop!
Ni kama gazeti lako likifungiwa halafu mtu aseme umejiamulia kufunga gazezi lako mwenyewe!
 
Lissu ana kumukumbu ya Bunge la Katiba mpya? Katiba iliyopendekezwa ilikuwa na kifungu cha kuwapo tume huru ya uchaguzi lakini kwa ulevi wa kutaka Kikwete aonekane amekwamishwa kutuletea katiba mpya, mliongoza harakati za mkwamo huo. Kwa nini hamkutumia nafasi hiyo?
 
Kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi. Kuna dhana inajengwa kwamba viongozi wa Chama chetu hawataki kupigania uwepo wa Tume Huru.

Kwamba tumeridhika na viubunge na viudiwani tunavyopata every five years, etc. Kwamba ili tuweze kushinda na kuchukua dola lazima tuache kushiriki uchaguzi hadi hapo tutakapopata Tume Huru, etc.

Hoja hii ni potofu.

Tume Huru ya Uchaguzi haipatikani nje ya mapambano mapana ya kutafuta demokrasia katika nchi yetu. Tume Huru ni sehemu tu ya tatizo la msingi la nchi yetu: tatizo la ukosefu wa demokrasia.

Tume ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa Katiba iliyopo. Inafanya kazi, by and large, kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizopo.

Kupigania Tume Huru maana yake ni kupigania Katiba Mpya; au angalau marekebisho ya Katiba iliyopo. Haiwezekani kupigania Tume Huru au marekebisho ya Katiba ya sasa in vacuo; inapiganiwa katika mazingira halisi ya kisiasa, kikatiba/kisheria na kitaasisi tunamoishi.

Kwa maneno mengine, ili upiganie Tume Huru lazima uwe na jukwaa la kusimamia. Iwe Bunge, au vyombo vya habari au mikutano ya hadhara, au kuchukua silaha na kwenda 'msituni', etc. Yote hayo ni majukwaa.

Sasa hoja ni je, tutumie jukwaa gani ili kupata Tume Huru??? Tukiacha kushiriki uchaguzi, tunabakia na jukwaa gani la kudai Tume Huru??? Mazingira ya vyombo vya habari, kama jukwaa la mapambano, ni rafiki na wezeshi kiasi gani??? Mikutano ya hadhara, jukwaa lingine muhimu, ni rafiki na wezeshi kiasi gani???

Ukiachia hii miaka ya Magufuli, je, mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani imekuwa mirahisi kiasi gani siku za nyuma kama majukwaa ya kudai demokrasia na Tume Huru???

Ukiachia wakati huu, vyombo vya habari vimekuwa rahisi kiasi gani kama majukwaa ya kidemokrasia??? Vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa rafiki na wezeshi kiasi gani katika madai yetu ya demokrasia na Tume Huru???

Ukweli ni kwamba maeneo yote haya yamekuwa na matatizo. Lakini hatujaacha kutumia fursa kidogo zilizokuwapo kudai demokrasia zaidi.

Hatuna uhuru wa vyombo vya habari sasa kuliko ilivyokuwa kabla ya Magufuli. Kuna matatizo mengi kwenye eneo hili kuliko zamani.

Lakini hakuna mtu anayedai vyombo vyetu vya habari viache kukusanya, kuandika na kusambaza habari hadi hapo tutakapopata uhuru kamili wa habari. Vyombo hivyo vinaendelea kufanya kazi zao katika mazingira halisi yaliyopo huku vikiendelea kudai uhuru wa habari.

Vivyo hivyo na sisi tunapaswa kuendelea kudai Tume Huru katika mazingira halisi ya kiuchaguzi yaliyopo.

Hatuwezi kususia jukwaa muhimu kama Bunge, licha ya matatizo yake mengi yaliyopo, unless jukwaa hilo lifungwe kabisa. Hatuwezi kususia uchaguzi, unless jukwaa la uchaguzi lifungwe kabisa, kama ilivyotokea majuzi kwenye uchaguzi wa mitaa na vijiji.

Mjadala huu unanikumbusha mjadala wa 'Mageuzi au Mapinduzi' ('Reform or Revolution') kati ya wanamapinduzi wa kijamaa wa Ulaya zaidi ya miaka mia moja iliyopita.

Wenye 'msimamo mkali' wa kimapinduzi walikuwa wanadai hakuna kushiriki harakati za kimageuzi kama vile mapambano ya kibunge; tufanye mapinduzi kwanza, etc.

Wengine wenye 'msimamo vuguvugu' wakidai kilele cha mapinduzi kinafikiwa kwa njia ya mageuzi ya kiuchaguzi, etc. Lenin aliwatuhumu wenye msimamo mkali kuwa wanasumbuliwa na 'ugonjwa wa utoto' ('an infantile disorder'!!!)

Na sisi pia hatutakiwi kuwa na ugonjwa huo. Kila jukwaa la mapambano ya kidemokrasia ni muhimu litumike. Kutumia njia mojawapo tu haitaleta matunda. Tunahitaji kutumia fursa zote zilizopo.
Mh.Lissu,upo vizuri sana.Kwangu Mimi were ni Mzalendo wa kweli na halisi.Tungekuwa na Watanzania hata asilimia nusu kama wewe,tungefika mbali Sana kama Taifa.Tunahitaji watu jasiri wanaojielewa,elimu ya Uraia inahitajika mno sasa.
Hakika bila Katiba wezeshi,Chaguzi guru na Uhuru kamili wa wananchi,tuna hali mbaya
Watanzania tusilale lale.....
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
wee mzee wacha bangi ivi ikitokea tume ya uchaguzi wote ni chadema nyinyi mutaingia kwenye uchaguzi. wapi umeona muamuzi na washikavibendera ni wa upande mmoja wa time inayocheza ? bangi mzee wacha
 
Lissu ana kumukumbu ya Bunge la Katiba mpya? Katiba iliyopendekezwa ilikuwa kifungu cha kuwapo tume huru ya uchaguzi lakini kwa ulevi wa kutaka Kikwete aonekane amekwamishwa kutuletea katiba mpya, mliongoza harakati za mkwamo huo. Kwa nini hamkutumia nafasi hiyo?
again bangi nyinyi zinawazuru ivi wewe ni kipofu au bunge la katiba ilikuwa ni miccm mitupu utaweza kufanya lolote hapo laamaana?
 
Mzee sumaye karudi nyumbani alifata madaraka 😃😃😃😃
Yaani namshangaa hata kama kureact angesubiri upepo wa uchaguzi upite, kitendo cha kutoka hadharani kwa wakati huu wa uchaguzi na kurusha tuhuma zilezile zinazo tumiwa na washindani wa CDM,marengo yake ni kuleta sintofahamu ndani ya chama,kwa holi anamfanyia kazi mtu. Na ameshindwa
 
again bangi nyinyi zinawazuru ivi wewe ni kipofu au bunge la katiba ilikuwa ni miccm mitupu utaweza kufanya lolote hapo laamaana?
Hao CCM ndio waliowawekea kifungu cha Tume huru ya Uchaguzi kwenye katiba pendekezwa na Bunge la katiba, ulitaka wafanye nini wawabebe mgongoni? Wapinzani waling'ang'ana na Tunu za Taifa wakasahau kuna vifungu chanya ambavyo vingesaidia kuanza na safari ya mabadiliko. Soma kifungu hicho 211.

SEHEMU YA PILI
TUME HURU YA UCHAGUZI
(a) Tume Huru ya Uchaguzi
Kuundwa kwa
Tume Huru ya
Uchaguzi
211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya
Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa
kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi
watakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa, na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa
Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na
ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka
mitano;
(c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii;
(d) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
(6) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa
mujibu wa sheria; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
(7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya
kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi:
(a)
 
Lissu anamjibu Prof Safari kiaina! Lissu, kwa yanayoendelea Chadema sasa alafu unaishia kudakia hoja kama hii unaanza kufanya uonekane wale wale team Mbowe!

Kubaki na heshima yako ni bora ukosoe wazi mwenendo wa chama hasa upande wa democracy au ukae kimya ukiendelea kurejesha afya yako.

Otherwise siku moja utakaa kwenye kona moja kujaribu kuweka sawa hili hata kama utakuwa nje ya Chadema!

Nadhani ndiyo hivyo anakosoa! Mawazo yaliyoko sasa hivi miongoni mwa wanasiasa na wafuasi wa upinzani ni kutoshiriki uchaguzi ujao bila tume huru! Hii nayo ni option. Lakini Lissu anatahadharisha kuhusu mtazamo huo ikizingatiwa kuwa upande wa wenye madaraka hawana tena rationality. Kwao wao kushika madaraka ya umma kwa njia za kistaarabu na zinazokubalika kimataifa is meaningless! Kuhusu hili la demokrasia ndani ya vyama mimi sijui chama chama chochote cha siasa nchi hii chenye demokrasia! Bora hata vyama vulivyoko nje ya serikali kwani havina mabavu ya kutumia. Kwa mtu aliyesoma na kuelimika, hata kama unashabikia chama kimojawapo, kwenye jukwaa kama hili, ni vizuri kujitahidi kuwa objective. Kwa mfano, mpaka sasa watawala wetu chini ya chama kinachowashutumu wenzake kuwa hawana demokrasia wamekataa katakata mgombea binafsi! Je, huko ndiyo kustawisha demokrasia? Mfano mwingine ni wale wanachama, tena viongozi wa chama kikongwe waliotiwa ndani ili wasishiriki mkutano mkuu wa chama chao, kisha kuachiwa mara tu baada ya mkutano! Katika hizi nchi zetu changa guided democracy ni muhimu sana. Siasa zetu siku hizi zimekuwa za kijima sana. Badala ya kujenga vyama vyao kwa wananchi kazi kubwa inayofanyika sasa ni kuhujumu na kudhoofisha washindani wao! Nyerere alipata kutahadharisha kuwa mambo ya msingi katika nchi husimamiwa. Ndivyo ilivyo kwenye vyama pia hasa katika kipindi kama hiki ambapo madaraka ya umma na ofisi za umma hutumia kinyume na katiba, sheria na ustaarabu wa kisiada. Bila kusimsmia mambo ya msingi leo muungano ungekuwepo?
 
Tatzo la lisuuu anakuwa kama anacheza mchezo wa kombolela, anajifulicha bahati mbaya sana anasahau kuwa Kopo ambalo anataraji alibutue jamaa anatembea nalo, mwisho wa siku hakuna ushindi ataonekana tu...

Hakuna alicho ongea cha maana kama Anahisi kaongea ya mAana azungumzie democrasia ndan ya Cdm ndpo aje na hzo blabla zake...

By the way lin anakuja dar?
 
Mwanahabari Huru,
WAKUU HAPA NDIPO PATAMU, PROF SAFARI HUKO ULIKO HOJA IPO MEZANI - MAELEZO TAFADHALI..
Kakufanza ubaya Sheikh??

Maana sikuelewi ati!
tapatalk_1568814208740.jpeg
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
Stupid shut up..!
 
Africa/Tanzania tunahitaji sana wanamikakati (strategists). Kuwashinda CCM just tu kwa siasa za provocation itachukua muda sana na kufanikiwa ni majaliwa siyo Kassim.
 
Tume huru ipi anayoona inatakiwa kuwepo, ni ile ya kutangaza wapinzani wameshinda hata kama wameshindwa? Ni ile ambayo vyama vinajitangazia ushindi vyenyewe kama alivyofanya Maalim Seif 2015 ? Ni ile ambayo Mbowe akisema mshindi ni Fulani ni lazima ashinde ?

Katika suala la tume ya uchaguzi, malalamiko yalikuwepo toka enzi na enzi na si malalamiko ya msingi Bali ni malamiko ya kudai kuporwa ushindi ambako hawajawahi wala kutegemewa kushinda. Hawa ndio wapinzani wa Tanzania
Hata huko kwao hakuna tume huru ya uchaguzi, hujaona waivurugana
 
Back
Top Bottom