Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Kumbe chama kina Mmiliki wake? Kwa hiyo akiamua anatimua tu watu na kuwapa misamaha pale anapohakikishiwa kuwa watuhumiwa watajirudi na kuunga Mkono maamuzi yake binafsi. Hivi vyama vingine hivi!
 
Mkuu, utatapatapa sana!! hadi sasa umekuwa kama umechanganyikiwa, kwani hata hueleweki, kila dk una ibuka na upuuzi mpya, baada ya muda tena unaukana, unakuja na jingine. pichu zitawabana sana.

Endelea tu kuwaka, umeambiwa chama kina Mmiliki wake anaetimua wanachama pale wasipoeleweka na kuwarudisha akiridhika na misimamo yao, halafu unasema ni chama kinachotetea maslahi ya kila Mtanzania kidemokrasia Kwa kufuata katiba.
 
Mkuu lisu anashida kichwani ataweza kumudu uongozi siyo kwamba anaweza kuwalipukia?

Anabehave kama downlink ya Dish lililocheza, muda wote signal inasearch halafu apewe madaraka, watu hawako serious kweli aisee.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Taarifa nilizopata hivi punde kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa Tundu Lissu ndiye atakayemrithi Dr Slaa endapo chama kitapata taarifa rasmi za kujiuzulu kwake. Chanzo hicho kinasema kuwa tayari Dr Slaa ameandika barua ya kujiuzulu na imefika kwenye mamlaka husika.

Chanzo hicho kinasema kuwa baada ya ujio wa Lowasa, hali ndani ya chama hicho ilikuwa tete hasa baada ya Tundu Lissu, John Mrema, John Mnyika na Dr Slaa kuanza mgomo wa kutoafiki maamuzi ya chama ya kumchukua Dr Slaa. Chanzo hicho kimenitokeza kuwa, chanzo cha mgomo huo ni kutokana na kukerwa na kauli ya mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei aliyetishia kuwafukuza viongozi hal endapo wangeendelea kuwa na msimamo wa kupinga ujio wa Lowasa. Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimenidokeza kuwa ilibidi Freeman Mbowe amuombe Mzee Mtei abatilishe msimamo wake wa kuwafukuza wanasiasa hao.

Kutokana na maombi hayo ya Mbowe kwa Mtei, hatimaye deal lilifanyika ambapo juzi Jumatano kilifanyika kikao cha falagha baina ya Lissu, Mbowe na Mtei. Katika kikao hicho Lissu alisema kuwa aliwafikishia ujumbe wenzake wa kuhudhuria kikao hicho isipokuwa wamekataa. aidha, Lissu alitoa maelezo yake kwa nini aliungana na Dr Slaa kupinga ujio wa Lowasa. kubwa alilolieleza ni tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowasa na kwamba watakuwa na wakati mgumu wawapo majukwaani kumnadi mwanasiasa huyo.

Hata hivyo, Mzee Mtei aliwaeleza kuwa tishio la kuwafukuza wanasiasa hao lilitolewa kwa ghadhabu na kwamba suluhu zaidi inahitajika kuliko mabavu. Pia alisema kuwa wakati uliopo mchango wao unahitajika sana na yeye yupo tayari kufuta kauli yake endapo watamhakikishia kuwa watakuwa tayari kumnadi Lowasa na kubadilisha fikra za Watanzania ili waamini kuwa tuhuma za ufisadi hazikuwa za msingi. Aidha, kutokana na Dr Slaa kuendelea na mgomo, Mzee Mtei alimuomba Lissu kujitokeza kwenye Media na kutoa maelezo kuwa yupo pamoja na Lowasa. Aidha, Lissu pia aeleze kwa nini Lowasa alijumuishwa kwenye List of Shame na aeleze kwamba ni yeye ndiye aliyeandaa orodha hiyo na kwamba alimpa tu Dr Slaa aisome. Likifanyika hilo, Mzee Mtei alisema kuwa watakuwa wamefanikiwa kuondoa List of Shame kutoka mikononi mwa Dr Slaa na kwamba kazi ya kumsafisha Lowasa itakuwa nyepesi.

Aidha, kwa vile Dr Slaa ameonekana kuendelea kukataa kumuunga mkono Lowasa, kikao hicho kilifanya maamuzi ya kumteua Tundu Lissu kujaza nafasi ya Dr Slaa. Kutokana na maamuzi hayo, ni dhahiri kwamba, Tundu Lissu ndiye atakayekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuziba nafasi ya Dr Slaa.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni kutolewa kwa taarifa rasmi ya kujiuzulu Dr Slaa ndipo taratibu za kichama zifanyike.

Mjumbe hauawi.
.,
Kama kazi unayo ndugu,unadhani chadema inafanya mambo yake kwa kukurupuka kama ccm
 
Hizi nazo ni kampeni.
Mbaya zaidi anaepigiwa kampeni sio mlengwa
 
Mkuu waonee huruma Makamanda wa BAVICHA Maana wanazidi kuchanganyikiwa.... Hizi habari uwe unazitoa kwa mafungu

Mkuu Lozaboni atauwa! Jamaa hawana uhakika na Lowasa ila hawana namna, sasa uwaletee habari za Dr. Kusepa inawachanganya sana.
 
Kama hii habari ni ya kweli tuambieni bwana. Msituchanganye Chadema wakati mnajua hali tete
utete unatoka wapi mkuu, kama Lowasa alivyokuja UKAWA na yeye aende CCM tumeshachoka na mashauzi yake mtu mzima huyo anaendeshwa na mwanamke?!! Ajue maisha yakimwendea vibaya huyo mama atamkimbia kama alivyomkimbia mme wa kwanza, maji huwa hayasahau njia yake.
 
Mkuu hata wewe unaweza kuchotwa na hekaya za Lizaboni? Achana naye huyu, leo ni siku ya nne kwa saa 24 yupo JF anaanzisha hili linafuata hili kuhusu Chadema, Slaa na Lowassa. Mpaka hata ukimshtua ghafla mgombea wa ccm ni nani anaweza kusema ni JK maana kesha msahau Magufuli. Huyo achana nae

Hivi ndivyo Lizaboni anavyopata mkate wake wa kila siku yeye pamoja na familia yake.Mwacheni ale vya mwisho mwisho cz zimebakia takribani siku 64 tu kitumbua kiingie mchanga
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lozaboni atauwa! Jamaa hawana uhakika na Lowasa ila hawana namna, sasa uwaletee habari za Dr. Kusepa inawachanganya sana.
Kama ndiyo imani yenu imekula kwenu, kwa taarifa yenu alikuwa hana kundi pia tumeshamkatia tamaa. loose one person and receive milions of people
 
T unataka kuitoa CCM na naona u muhimu wa Lowassa ila sitakubali usaliti wa CHADEMA dhidi ya Dr Slaa. Hususani ushiriki wa Tundu Lissu. 2010 Dr Slaa alituambia tumchague Lissu ili akazibe nafasi yake bungeni. Hivyo anamwamini zaidi.
Vinginevyo labda kwenye kuwe na nguvu nyingine iliyomfanya Dr Slaa awe kinyume.
 
CCM safari hii mmmeshikwa pabaya, hamna jipya au kipya mnachoweza kutuaminisha. Kuna member mmoja humu kasema eti Dr. Slaa kaamua kuondoka CDM kwa sababu ni mkewe kamzuia kuendelea na na ukatibu mkuu wake kwenye chama. Na kuna wengine wanakuja na allegations kwamba Lowassa kaja CDM kwa sababu ya uroho wa madaraka. WHAT ABOUT hao CCM wanaotoana ngeo na kuhatarishana kutoana uhai, hao hawana uroho wamadaraka? Wengine wanaenda mbali saaana hadi kwa sangoma kutafuta ubunge, huko si kuwa na uroho wa madaraka? Watafutao ubunge wa CCM ni zaidi ya wawili hadi sasa hivi wamenaswa na TAKUKURU sijamsikia hata mmoja kutoka Ukawa.
Ukimya wa Dr. Slaa unawachanganya mno CCM kuliko CDM kwenyewe

Nimeipenda hiyo statement mkuu
 
I 'm sure you know & see it . Keep praying my dear.

Lowasa is just a new character with no political value added to a crumbling block of people who had lost hope with the intention of rejuvenating its political position which will in turn continue protecting the interests of the selected few.
 
Unatema bigijii [Dk Slaa] kwa Karanga za Kuonjeshwa [lowasa]...chama cha kibiashara asante Mungu kwa kutuonyesha
 
Back
Top Bottom