Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Hii mada ni ya siku nyingi sana lakini bado ina mashiko. Kitendo cha Lowassa jana kusema kuwa viatu vya Dr. Slaa ni vikubwa ni dhahiri anajiona yeye ndiye anafaa kuwa katibu Mkuu.
 
Kilichokuwa kimefanyika na CHADEMA ni biashara purely, walifikiri kuwa popularity ya Lowasa ingewaingiza Ikulu, siyo kwamba hawakujua udhaifu wa Lowasa. Kwa wale watu waliosoma Economics wanajua vizuri kitu kinachoitwa "Tyrany of Majority"- kwa kifupi ni pale majority/ wingi unapotumika kufanya maamuzi ambayo hayana logic simply tu kwa sababu sheria inasema wengi wakishasema ndiyo basi hilo jibu sahihi. CHADEMA walitaka ku- take advantage hiyo huku wakijua kwamba majority were wrong but their selection would prevail
 
kikao baina ya MBOWE,LISSU na MTEI.Ina maana wewe ni nani kati ya hao mpaka utoe taarifa as if ulihudhuria
 
Wadau amani iwe kwenu.

Taarifa nilizopata hivi punde kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa Tundu Lissu ndiye atakayemrithi Dr Slaa endapo chama kitapata taarifa rasmi za kujiuzulu kwake. Chanzo hicho kinasema kuwa tayari Dr Slaa ameandika barua ya kujiuzulu na imefika kwenye mamlaka husika.

Chanzo hicho kinasema kuwa baada ya ujio wa Lowasa, hali ndani ya chama hicho ilikuwa tete hasa baada ya Tundu Lissu, John Mrema, John Mnyika na Dr Slaa kuanza mgomo wa kutoafiki maamuzi ya chama ya kumchukua Dr Slaa. Chanzo hicho kimenitokeza kuwa, chanzo cha mgomo huo ni kutokana na kukerwa na kauli ya mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei aliyetishia kuwafukuza viongozi hal endapo wangeendelea kuwa na msimamo wa kupinga ujio wa Lowasa. Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimenidokeza kuwa ilibidi Freeman Mbowe amuombe Mzee Mtei abatilishe msimamo wake wa kuwafukuza wanasiasa hao.

Kutokana na maombi hayo ya Mbowe kwa Mtei, hatimaye deal lilifanyika ambapo juzi Jumatano kilifanyika kikao cha falagha baina ya Lissu, Mbowe na Mtei. Katika kikao hicho Lissu alisema kuwa aliwafikishia ujumbe wenzake wa kuhudhuria kikao hicho isipokuwa wamekataa. aidha, Lissu alitoa maelezo yake kwa nini aliungana na Dr Slaa kupinga ujio wa Lowasa. kubwa alilolieleza ni tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowasa na kwamba watakuwa na wakati mgumu wawapo majukwaani kumnadi mwanasiasa huyo.

Hata hivyo, Mzee Mtei aliwaeleza kuwa tishio la kuwafukuza wanasiasa hao lilitolewa kwa ghadhabu na kwamba suluhu zaidi inahitajika kuliko mabavu. Pia alisema kuwa wakati uliopo mchango wao unahitajika sana na yeye yupo tayari kufuta kauli yake endapo watamhakikishia kuwa watakuwa tayari kumnadi Lowasa na kubadilisha fikra za Watanzania ili waamini kuwa tuhuma za ufisadi hazikuwa za msingi. Aidha, kutokana na Dr Slaa kuendelea na mgomo, Mzee Mtei alimuomba Lissu kujitokeza kwenye Media na kutoa maelezo kuwa yupo pamoja na Lowasa. Aidha, Lissu pia aeleze kwa nini Lowasa alijumuishwa kwenye List of Shame na aeleze kwamba ni yeye ndiye aliyeandaa orodha hiyo na kwamba alimpa tu Dr Slaa aisome. Likifanyika hilo, Mzee Mtei alisema kuwa watakuwa wamefanikiwa kuondoa List of Shame kutoka mikononi mwa Dr Slaa na kwamba kazi ya kumsafisha Lowasa itakuwa nyepesi.

Aidha, kwa vile Dr Slaa ameonekana kuendelea kukataa kumuunga mkono Lowasa, kikao hicho kilifanya maamuzi ya kumteua Tundu Lissu kujaza nafasi ya Dr Slaa. Kutokana na maamuzi hayo, ni dhahiri kwamba, Tundu Lissu ndiye atakayekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuziba nafasi ya Dr Slaa.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni kutolewa kwa taarifa rasmi ya kujiuzulu Dr Slaa ndipo taratibu za kichama zifanyike.

Mjumbe hauawi.
Kuna mahali umekosea hapo juu. Umeandika kuwa John Mrema, Lissu Mnyika & Co walikuwa wanapinga CHADEMA kumchukua Dr.Slaa? Ndio shida ya habari za kutunga, lazima ukosee tu!
 
Asanteeeeee Mjumbe Lizaboni Lowassa. Japo posti ilikuwa ya mwaka jana.
 
Kuna mahali umekosea hapo juu. Umeandika kuwa John Mrema, Lissu Mnyika & Co walikuwa wanapinga CHADEMA kumchukua Dr.Slaa? Ndio shida ya habari za kutunga, lazima ukosee tu!
Kaka huyu anatamani awe mwanachama lakini anamuogopa Mwenyekiti wao wa chama chao
 
namtakia uongozi mwema lkn sidhani km iyo nafas ataiweza lissu kwa ukigeu geu wake
 
Kuna mahali umekosea hapo juu. Umeandika kuwa John Mrema, Lissu Mnyika & Co walikuwa wanapinga CHADEMA kumchukua Dr.Slaa? Ndio shida ya habari za kutunga, lazima ukosee tu!
MUSSA ALLAN, inaelekea ama hujui historia ya Mgogoro ndani ya CHADEMA baada ya Lowasa kuinunua CHADEMA ama unajifanya taahira. Unakumbuka kikao kilichofanyika nyumbani kwa Dr Slaa baina ya Lissu, Mnyika na Mrema? Unajua nini walizungumza? Kama huelewi kitu ni bora ungeuliza kwanza
 
Back
Top Bottom