Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Mzee Mtei?
Kwani hiki chama ni mli yzee mtei mpakaawatshie wenzie kuwafukuza?
 
nafikiri huu utakuwa ni mwisho wao kwa staili hiiii wamekwishaaa
 
si riwaya bali ni habari za kweli.................... subiri matokeo.
 
Lakin Lizabon naanza kukubaliana na ww hata kipind cha lowasa kwenda chadema ulikuwa unaleta taarifa kama hivi lakn mm ni miongon mwa watu waliokuwa wanakuponda kuwa unaleta taarifa za uongo. Lakn baadae ikawa kweli na hii naanza kukubaliana na ww.

Naona slaa hataki kuwa nyumbu kama yalivyo manyumbu chadema wote na mbowe wao
 
Last edited by a moderator:
Dr.Slaa katuangusha sana kwa kujifanya haoni manufaa ya kumpokea Lowassa.

Hajawaangusha, tatizo deal limepigwa na Wachaga tu. Wakati wa kujenga chama walikuwa wote. Hata Lisu alisikia tu harufu, kwa kuwa Lisu ana double standard amewageuka wenzake.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Taarifa nilizopata hivi punde kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa Tundu Lissu ndiye atakayemrithi Dr Slaa endapo chama kitapata taarifa rasmi za kujiuzulu kwake. Chanzo hicho kinasema kuwa tayari Dr Slaa ameandika barua ya kujiuzulu na imefika kwenye mamlaka husika.

Chanzo hicho kinasema kuwa baada ya ujio wa Lowasa, hali ndani ya chama hicho ilikuwa tete hasa baada ya Tundu Lissu, John Mrema, John Mnyika na Dr Slaa kuanza mgomo wa kutoafiki maamuzi ya chama ya kumchukua Dr Slaa. Chanzo hicho kimenitokeza kuwa, chanzo cha mgomo huo ni kutokana na kukerwa na kauli ya mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei aliyetishia kuwafukuza viongozi hal endapo wangeendelea kuwa na msimamo wa kupinga ujio wa Lowasa. Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimenidokeza kuwa ilibidi Freeman Mbowe amuombe Mzee Mtei abatilishe msimamo wake wa kuwafukuza wanasiasa hao.

Kutokana na maombi hayo ya Mbowe kwa Mtei, hatimaye deal lilifanyika ambapo juzi Jumatano kilifanyika kikao cha falagha baina ya Lissu, Mbowe na Mtei. Katika kikao hicho Lissu alisema kuwa aliwafikishia ujumbe wenzake wa kuhudhuria kikao hicho isipokuwa wamekataa. aidha, Lissu alitoa maelezo yake kwa nini aliungana na Dr Slaa kupinga ujio wa Lowasa. kubwa alilolieleza ni tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowasa na kwamba watakuwa na wakati mgumu wawapo majukwaani kumnadi mwanasiasa huyo.

Hata hivyo, Mzee Mtei aliwaeleza kuwa tishio la kuwafukuza wanasiasa hao lilitolewa kwa ghadhabu na kwamba suluhu zaidi inahitajika kuliko mabavu. Pia alisema kuwa wakati uliopo mchango wao unahitajika sana na yeye yupo tayari kufuta kauli yake endapo watamhakikishia kuwa watakuwa tayari kumnadi Lowasa na kubadilisha fikra za Watanzania ili waamini kuwa tuhuma za ufisadi hazikuwa za msingi. Aidha, kutokana na Dr Slaa kuendelea na mgomo, Mzee Mtei alimuomba Lissu kujitokeza kwenye Media na kutoa maelezo kuwa yupo pamoja na Lowasa. Aidha, Lissu pia aeleze kwa nini Lowasa alijumuishwa kwenye List of Shame na aeleze kwamba ni yeye ndiye aliyeandaa orodha hiyo na kwamba alimpa tu Dr Slaa aisome. Likifanyika hilo, Mzee Mtei alisema kuwa watakuwa wamefanikiwa kuondoa List of Shame kutoka mikononi mwa Dr Slaa na kwamba kazi ya kumsafisha Lowasa itakuwa nyepesi.

Aidha, kwa vile Dr Slaa ameonekana kuendelea kukataa kumuunga mkono Lowasa, kikao hicho kilifanya maamuzi ya kumteua Tundu Lissu kujaza nafasi ya Dr Slaa. Kutokana na maamuzi hayo, ni dhahiri kwamba, Tundu Lissu ndiye atakayekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuziba nafasi ya Dr Slaa.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni kutolewa kwa taarifa rasmi ya kujiuzulu Dr Slaa ndipo taratibu za kichama zifanyike.

Mjumbe hauawi.

Lizaboni, wakati mwingine huwa mnakosa cha kufanya mwisho wa siku mnaendeleza utamaduni wa maccm wa kuwapuuza wananchi na kuwafanya wajinga always.
Tangu lini umekuwa msemaji wa Chadema, na unapotaka kuwaaminisha watu taarifa za uongo basi ni afadhali ungegusia baadhi ya mambo ya ukweli bila kusahau kueleza mchakato wa kumpata katibu mkuu, hicho kikao unachokisema ni kikao gani wajumbe wake ni kina Nani, kiliitishwa na nani lini na wapi?

Mmekaa tu kutunga uongo kwa kufikiri kwamba ndio itakuwa silaha ya maangamizi kwa chadema, na itakuwa ngao ya kuwa king a na ugonjwa wa mpasuko ndani ya ccm, mnajiongopea

ukweli ni kwamba katibu mkuu wa Chadema bado ni Dr Slaa, haya ya kina Lizaboni yapuuzeni ni upuuzi kama upuuzi mwingine
 
Sijaweweseka mkuu na sina sababu ya kuwa hivyo. Nimeandika haya nikiwa na akili timamu
Heee! Kumbe ukiwa na akili timamu unaandika hivyo!? Sasa ukiweweseka itakuaje!?acha double standards, ungeeleweka zaidi na kukisaidia chama chako kipindi hiki ambacho kwenu rushwa ni km Sara, katibu wako kashikwa akitoa rushwa, mna haki ya kupiga watu na magongo tena hadharani kwa kuwa nyinyi ni miungu watu, Mmmh ! Mnatufanya wajinga sana watanzania na mnadhani tutaendelea kuwa wajinga! ----- we!
 
Mkuu Lizaboni siku zote nimekuwa sipuuzi habari zako, ila huwa nazitumia kuunganisha data.
 
Last edited by a moderator:
Raia Tanzania linajaribu kuvutia wateja kwa habari za UZUSHI.
 
Back
Top Bottom