Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

Tundu Lissu kumrithi Dr. Slaa

hivi Lizaboni unahisi CCM itatawala milele?? Tambua wewe ni mfaidika wa utawala uliopo....furahi, ila tambua kila kilicho na mwanzo akikosi mwisho

Hatubadiliki na machapisho yako, badala ya kuja hapa na kutueleza mazuri ya mgombea wako....we ni kueleza hisia za kile unachokiombea kwa UKAWA kiwe.

Utalia sanaaaa

Tuko na LOWASA............tuko na UKAWA
 
Last edited by a moderator:
Mpaka dakika hii ma-ccm yamekamatika kisawasawa! UKAWA tunawaomba wawe watulivu sana maana haijapata kutokea na haitakaa itokee tena kuyakamata ma-ccm kiasi hicho!! Mwaka huu lazima yapigwe tu!!!
 
Hata habari za yule Mzee mroho wa madaraka wa kule Monduli kwenda cdm zilianza kama tetesi huku wafuasi wa cdm wakipinga kwa nguvu zote ila leo tumeona watu wanakula walichotapika, na hili la Mzee Slaa tungoje tu muda ukifika tutajua ukweli.

ila ni vyema Mzee Slaa asiondoke ili mkishindwa October msiwe na kisingizio.
 
Atafanya mkutano na waandishi wa habari leo saa 8 mchana ktk ukumbi wa maelezo.wahini nafasi ni chache.pia atakuwepo katibu mwenezi wa ccm akimsindikiza.chanzo ni mhusika mwenyewe.kwa vile umezoea uzushi wapelekee na waajiri wako habari hii.watakuongezea dau.!
 
Alichosema Mdau Lizaboni huwenda ni sahihi maana ktk uzi mzima sijaona anayempinga zaidi ya kumshushia matusi. Keep it up Lizaboni usihofu maana 'mti uzaaao matunda ndio upopolewao'. Wanange tu hao wapenda ufisadi.


Unaweza kutoa sababu kwanini asitukanwe kwa haya aliyoandika hapa
 
Hiv huyu jamaa...story za lumumba ....umekosa unatafuta za chadema......ya chadema waachie chadema usilo lijua ni kama usiku wa giza
 
HABARI ZA HIVI PUNDE: "HAKUNA SINTOFAHAMU YOYOTE KATI YA YANGU MIMI Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika, Tundulisu na wengineo kwa ujio wa mgeni Mhe. Lowassa wala hakuna chochote kilichoharibika ndani ya CHADEMA, NCCR, NLD, CUF wala kwa wanachama, wafuasi na wapenzi wa UKAWA.
Myaonayo na myasikiayo kwenye mitandao ya kijamii ni kauli za wafa maji. Tulichokifanya UKAWA ni kuunganisha dhamira zetu pamoja. Narudia tena; tulichokifanya kama UKAWA ni kuunganisha dhamira zetu pamoja
Zaidi sana napenda kusisitiza jambo hili kwa umma kwamba NDANI YA VYAMA VINAVYOUNDA UKAWA HAKUNA MWENYE DHAMANA WALA MAMLAKA YA JUU ZAIDI YA MWINGINE HATA KWA KWA YULE MSHABIKI"
By. Dr. Wilbroad Slaa (katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo-CHADEMA)
 
CCM safari hii mmmeshikwa pabaya, hamna jipya au kipya mnachoweza kutuaminisha. Kuna member mmoja humu kasema eti Dr. Slaa kaamua kuondoka CDM kwa sababu ni mkewe kamzuia kuendelea na na ukatibu mkuu wake kwenye chama. Na kuna wengine wanakuja na allegations kwamba Lowassa kaja CDM kwa sababu ya uroho wa madaraka. WHAT ABOUT hao CCM wanaotoana ngeo na kuhatarishana kutoana uhai, hao hawana uroho wamadaraka? Wengine wanaenda mbali saaana hadi kwa sangoma kutafuta ubunge, huko si kuwa na uroho wa madaraka? Watafutao ubunge wa CCM ni zaidi ya wawili hadi sasa hivi wamenaswa na TAKUKURU sijamsikia hata mmoja kutoka Ukawa.
Ukimya wa Dr. Slaa unawachanganya mno CCM kuliko CDM kwenyewe.
 
Time will tell, asante kwa habari (kama ni za kweli) ila tambua Dk Slaa with due respect mgomo wake hauna athari kubwa kwa CDM kama inavyodhaniwa. Chadema ni taasisi strong sana na imejengwa kwa miaka mingi sio kwa ushabiki wa Dk Slaa pekee. Ukawa sasa tunajipanga kuongoza nchi sio tena kuhofia propaganda za marahemu mtarajiwa CCM
 
Magufuli mtandaoni kafutika ghafla,hata huko mikoani alikopita amesahaulika ghafla.
 
Lizaboni hana jipya yeye kila mada ni UAWA, CHADEMA na Dr.Slaa tafuta kwa miccm wenzaki uandike mf;Nape ahojiwa na takukuru kwa kuhonga wapiga kura wa ccm jimbo la Mtama- Lindi ahojiwa kwa saa tano, mbunge wa babati ccm akimbia takkuru na kuacha gari yake, Wasira amtwanga mwenyekiti mkoa wa mara ccm, naibu spika amtwanga Mgombea mwenza kwa rungu, naibu waziri wa Fedha ahojiwa na Takukuru kwa kutoa rushwa na taarifa nyingine nyingi ni taarifa ambazo ni za kweli si tetesi kama za Dr.Slaa kujiuzulu. Pole Lizaboni na ukada wako wa CHAMA CHA MAJAMBAZI (CCM).
 
Jamani nauliza hivyo huyu mzee mtei, hafungwi na katiba za chama, mbona anaingilia mambo mengi ya chama. Anawezaje kuamu katibu na mwanasheria wafukuzwe . He jamaani angalieni kibali cha chama pengine ni Mali yake pekee kwa hivyo anao uwezo wa kumfukuza mtu yoyote kazi.
 
Jamani nauliza hivyo huyu mzee mtei, hafungwi na katiba za chama, mbona anaingilia mambo mengi ya chama. Anawezaje kuamu katibu na mwanasheria wafukuzwe . He jamaani angalieni kibali cha chama pengine ni Mali yake pekee kwa hivyo anao uwezo wa kumfukuza mtu yoyote kazi.

Hiyo ni kuonesha kuwa chama ni cha mtu mmoja, anaweza kuamua lolote, bado watanzania hatulioni hilo? Tujiulize 10 bil alizotoa EDO ni za nini?
 
Nadhani ungeachana na habari za chadema ujikite zaidi kutoa habari za Magufuri

Mkuu nadhani si haki kumfunga mipaka ya kuandika taarifa. Zote jamaa huwa anatupia jf akipata. Safi sana Lizabon.
 
Back
Top Bottom