Tundu Lissu kuitwa kwenye Kamati ya maadili ya madiwani Singida

ulichofanya ni sawa na kuwauliza mashabiki wa Yanga kuwa Berko na Kaseja nani mkali, obvious jibu litakuwa Berko ni mkali. Probably na wewe wananchi uliowahoji ni wa chama tofauti na cha Lissu.Halafu kuhusu Lissu kutofanya kitu jimboni kwake. Weka propaganda pembeni na ujiulize swali hili. Hao wabunge waliokaa majimboni kwao miaka 20 wamefanya nini? Sasa ndio umgeukie Lissu na mwaka wake mmoja
Mbona umeni-underestimate kiasi hicho? Yaani niwaulize anti-Lissu pekee badala ya pia pro-Lissu pia? All right, kama unafahamu jambo lolote la maendeleo alilofanya Tundu Lissu au mipango yoyote ya maendeleo aliyo nayo (zaidi ya kupinga michango ya maendeleo) hebu iweke wazi hapa, usipinge hoja kishabiki tu! Mimi namfagilia Lissu kwa kazi nzuri anayoifanya Bungeni, lakini huko Jimboni ni "sound" tuuuu! Usilete hoja za kitoto kwamba eti "waliokaa miaka 20 wamefanya nini!"
 
Watanzania bwana...wamezoea michango kila mahali. Na sasa wapo tayari kudaiwa michango bila taarifa?! Kweli hii nchi imejaa vilaza...
All right, wananchi wa Singida Mashariki mpaka sasa hawachangi michango yoyote wakisubiri waletewe fedha na Tundu Lissu ambaye aliwaahidi kwamba "anajua zilipo!" Kwa hiyo Mh Lissu "akachote" hizo fedha haraka ili azipeleke kwenye maendeleo!
 
Mbona umeni-underestimate kiasi hicho? Yaani niwaulize anti-Lissu pekee badala ya pia pro-Lissu pia? All right, kama unafahamu jambo lolote la maendeleo alilofanya Tundu Lissu au mipango yoyote ya maendeleo aliyo nayo (zaidi ya kupinga michango ya maendeleo) hebu iweke wazi hapa, usipinge hoja kishabiki tu! Mimi namfagilia Lissu kwa kazi nzuri anayoifanya Bungeni, lakini huko Jimboni ni "sound" tuuuu! Usilete hoja za kitoto kwamba eti "waliokaa miaka 20 wamefanya nini!"
Mkuu Buchanan nakuheshimu sana, sikutegemea uite hoja yangu ya kitoto. Niliamini kwa ukomavu wako ungenijibu kwa mifano hao wabunge waliokaa miaka 20 majimboni mwao wamefanya nini. Nway tuache hilo, la pili ni hili ebu toa mifano ya mambo waliyofanya wabunge wapya majimboni katika kipindi sawa na alichokaa Lissu.NB: Mimi sitoi hoja kishabiki, so far sina mahaba na chama chochote cha siasa
 
Sidhani kama Lissu ni Mungu hata asikosolewe! Wewe mwenyewe umetoa allegations ambazo huna support yoyote dhidi ya Arusi ya Nyalandu, sasa mimi na wewe nani anatumia tumbo au kichwa kufikiri?
Hiyo ya Nyalandu ni ya kweli kabisa na zilipatikana kwenye minutes za kikao cha h/kijiji cha Kinyeto. ukitaka nyaraka zipo!!
 
Mkuu Buchanan nakuheshimu sana, sikutegemea uite hoja yangu ya kitoto. Niliamini kwa ukomavu wako ungenijibu kwa mifano hao wabunge waliokaa miaka 20 majimboni mwao wamefanya nini. Nway tuache hilo, la pili ni hili ebu toa mifano ya mambo waliyofanya wabunge wapya majimboni katika kipindi sawa na alichokaa Lissu.NB: Mimi sitoi hoja kishabiki, so far sina mahaba na chama chochote cha siasa
Kusema kweli sina data na Wabunge wengine wamefanya nini ila sio tiketi ya Mheshimiwa Tundu Lissu kutokufanya lolote Jimboni kwake!
 
Nilisimuliwa na wananchi mbali mbali wa Jimbo husika wakilaani vitendo anavyowafanyia Tundu Lissu! Wamedai pia kwamba huyu Lissu hana lolote analofanya Jimboni kwake zaidi ya kutamba eti "amemshtaki hata Spika wa Bunge!" Ni majigambo (sound) tu hana lolote la maendeleo!

Mkuu una lako jambo tu,si useme wazi kama unataka kugombea jimbo hilo 2015? Pamoja na wachangiaji wa mada yako kujaribu kukuelewesha lkn umeamua kuziba masikio kabisa na kutaka kusikia kile tu unachopenda kukisikia.
 
Tatizo kuu ni kwamba Wananchi walio wengi, kulingana na utafiti wangu hawakubaliani na vitendo vya Lissu vya kukodi vijana wa kihuni ili kuwapiga wakusanya michango! Madarasa mbalimbali ya Shule za Msingi na Sekondari ujenzi wake mpaka sasa umesimama kwa sababu ya vitisho ya Lissu na vijana wake!

Ninahisi kama unayoyasema hayana ukweli. Lissu ni nani hata aweze kufanya hivyo?
 
Kusema kweli sina data na Wabunge wengine wamefanya nini ila sio tiketi ya Mheshimiwa Tundu Lissu kutokufanya lolote Jimboni kwake!

Buchanan,

Turudi shuleni kipindi kile tupo bweni. Uliomba mzazi akupe elf 20 na huenda matumizi halisia ni elf 10. Kweli ukapewa, na najua kabisa umepewa, kesho unaniomba msaada bila kunieleza zile zako wapi?

Kila wilaya inachukua makadirio yake inapeleka mkoani then taifani na kila mkoa unagawiwa pesa kutokana na idadi ya watu kama sikosei. Wilaya ya singida vijijini ina fungu lake na Tundu Lissu anataka hizi zitumike ndo maana ya kulipa kodi, kusamehe wawekezaji na kazi ya serikali ilioko madarakani. Hizi ndo pesa za Tundu na kwa sababu huu ndo mwaka wake wa kwanza, umewahi sana kumhukumu. Nimetembelea kule kijijini kwake, trust me, watu wanaelewa na ole wao sumu hii ikaenezwa. Kumbuka kauli ya Mkapa, dhana ya chadema kupinga posho na Shibuda kupingana nao ni Mbunge na staili ya wabunge wa CCM kufikiri Mbunge lazima atoe fedha kwa wananchi.

Hivi unajua asilimia kubwa ya watanzania hawajui wajibu wa serikali? i think na wewe hujui. Samahani lakini.

Dhana ya wananchi kuchangia maendeleo ni nzuri na inatumiwa na WB kama njia mojawapo ya kuwafanya wananchi wafeel ownership na pia hio michango inakua-audited hata kama mtu kajitolea nguvu. Mbona mchango wa serikali kwenye uwanja mpya wa Taifa unajulikana interms of money ilhali walimega tu maeneo yao? why not kuku mmoja wasimuuze hata kwa elf1? Mbona tulikuwa happy kuchangia vita ya kagera and not our own classrooms? think twice.

Madiwani kwa Lissu hawatakuwa na hoja huenda nalo ikawa darasa kwao. Naamini Lissu atakuwa na hamu nao sana.

Mkuu unamaanisha Lissu anatakiwa achukue pesa mfukoni mwake ajenge darasa? sasa mbona hataki na posho? It will tale sometimes to understand but trust me, Tundu hataumia ila wananchi wa kule na Tundu can go to any modern society in Tz na kupata ubunge.
 
Mkuu una lako jambo tu,si useme wazi kama unataka kugombea jimbo hilo 2015? Pamoja na wachangiaji wa mada yako kujaribu kukuelewesha lkn umeamua kuziba masikio kabisa na kutaka kusikia kile tu unachopenda kukisikia.
Hapana mzee sina nia ya kugombea ubunge ila nazungumzia "the other side of the coin" ili kumsaidia Kamanda wetu Tundu Lissu aendelee kukubalika Jimboni kwake! Kwa sasa treni yake ya kisiasa imeanza kuwa "derailed" kwa vitendo vyake mwenyewe! Pamoja na kwamba nimejieleza kuwa nimeongea na baadhi ya wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki bado watu wanaona kuwa mimi ni mwongo tu! Je, hawa ndio wachangiaji ambao unadai "wamejaribu kukuelewesha?"
 
Iko wapi ripoti ya mapato na matumizi katika Halimashauri husika?? wananchi wanataka kujua jinsi pesa zao zilivyofanyakazi. Hiyo ni jeuri ya CCM kuvuruga kila jimbo ambalo linaongozwa na Mbunge kutoka CHADEMA. Wabunge wote wa CHADEMA kuweni makini, tayari CCM wameanza mchezo mchafu. Wamechakachua muafaka wa Arusha, kisha wakaenda kupiga watu Mwanza - machinga hii yote ni kuvuruga amani katika majimbo hayo. Mwenye akili haambiwi tazama.
 
Iko wapi ripoti ya mapato na matumizi katika Halimashauri husika?? wananchi wanataka kujua jinsi pesa zao zilivyofanyakazi. Hiyo ni jeuri ya CCM kuvuruga kila jimbo ambalo linaongozwa na Mbunge kutoka CHADEMA. Wabunge wote wa CHADEMA kuweni makini, tayari CCM wameanza mchezo mchafu. Wamechakachua muafaka wa Arusha, kisha wakaenda kupiga watu Mwanza - machinga hii yote ni kuvuruga amani katika majimbo hayo. Mwenye akili haambiwi tazama.
Kama Tundu Lissu analitakia mema Jimbo lake asiingie kwenye mitego ya magamba ya "Migogoro Syndrome!"
 
inatapisha inatia kichefuchefu huku kwetu mimi nimepiga marufuku mgambo au mwenyekiti wa kitongoji kuja nyumbani kwangu kuchukua mchango wowote. Nimemwambia mke wangu kuwa mchango utakaotoka nyumbani kwangu ni kumchangia mtoto "ALIEFAULU KUINGIA KIDATO CHA KWANZA SAINT KAYUMBA" na wazazi wake hawana uwezo na pesa hizo nitapeleka mwenyewe huko Saint Kayumba. na nipo sirias nimenunua gobori la wazigua kwa ajili hiyo tu. LISSU KEEP ON MOVING anda pull up ur sox. Saa ya ukombozi inakaribia
 
WATANZANIA NA MICHANGO....
TULICHANGISHWA VITA YA NDULI...
TUKACHANGISHWA VIWANJA VYA MICHEZO...
TUKACHANGISHWA UJENZI NA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU...
TUKACHANGISHWA KUFUFUA VYAMA VYA USHIRIKA...
TUNACHANGISHWA DOWANS, IPTL, RICHMONDS, ATCL, MADAWATI, BARABARA, JENZI ZA SHULE, ZAHANATI, VITUO VIDOGO VYA POLISI....
TULICHOBAKIZA NI KUCHANGIA MVUA (tuiponea chupuchupu), HEWA TUNAYOVUTA NA..............
 
Tatizo la Lissu ni kujiingiza kichwa kichwa, na ndio mtego wenyewe wa magamba, kwa kuwaambia wananchi kuwa wasichangie michango kwa kuwa yeye anajua fedha zilipo, kwa hiyo wananchi wanasubiri hizo "fedha za Lissu" ili waendelee na ujenzi wa madarasa!
Nafikiri huu ni mwanzo mzuri na ni mwanzo tu, mbona wananchi wanahaki ya kuandamana kudai maendeleo? Nadhani chadema itoe tamko katika halmashauri zenye wabunge wake hamna mchango wala nini. Na kama watasusia kupeleka maendeleo wananchi ni kufanya maandamano mpaka kieleweke. Naliona hili Arusha litakuja very soon maana magamba wanandhani kuleta maendeleo ni hisani yao kwa wananchi kumbe ni lazima na ndiyo wajibu wao.Kama wanadhani wananchi watakaa kimya waendelee kusota eti magamba hawapeleki maendeleo kisa hawakuchaguliwa sehemu hiyo, itakula kwao maana hii ni cdm siyo cuf.
 
Unapotosha mada.umebadili lalamiko lako la awali la Mh. Lissu kuzuia wananchi kuchangia pesa kisheria, then hapa umegeuka na kusema anatumia vijana kufanya vurugu kwa wakusanya michango hiyo. Acha ushabiki usio na mashiko! Tetea ulichosema awali.

Kwanza kwa akili ya kawaida, mtu mzima mwenye heshima zake tena mwanasheria kama Tundu Lisu hawezi kufanya kioja cha kukodi wahuni wa kupiga wakusanya kodi. That is next to impossible.
Pili, hao madiwani wa CCM wa drs la saba Singida mashariki wataumbuka siku akienda kuongea nao. Mawaziri wanamwogopa sana. JK aliwaambia kule Singida, Heri Dr Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge. Sembuse madiwani wa CCM?
 
All right, wananchi wa Singida Mashariki mpaka sasa hawachangi michango yoyote wakisubiri waletewe fedha na Tundu Lissu ambaye aliwaahidi kwamba "anajua zilipo!" Kwa hiyo Mh Lissu "akachote" hizo fedha haraka ili azipeleke kwenye maendeleo!

ni haki yao kujua matumizi ya pesa zao. Acha wa-exercise haki yao. Ivi unadhani kwa nini Uingereza ilipoteza mamlaka ya kifalme? Ukifuatilia nchi zilizoendelea na historia zao, zilipitia kipindi kama hichi cha kudai haki zao kutoka kwa watawala. Tofauti ni kuwa huko haya mambo yalitokea miaka 300+ iliyopita. Ndio maana nawaambia wengi kuwa Africa ipo about 500yrs behind the developed world. Na pia husema maendeleo sio kujenga barabara, bali kufungua fikra. Huwezi kuwa na maendeleo bila kuwa na fikra/akili iliyoendelea/funguka. Na hili ni kweli hata uwe na doctorate degree. Angalia effect za hizo doctorate degrees kwa wanasiasi walionazo...zero!!
 
kamanda wembe ule ule, Hata waziri bungeni alishindwa kuthibitisha mahesabu ya michango na ngapi zimekusanywa
yaani Mkurugenzi na mkuu wa wilaya na madiwani it seems lao moja kula michango,
Hivyo kamanda lisu alisema wpaewe mahesabu na kiwango cha kuchanga ndio halafu waendelee kuchanga
 
Kwani Lissu ni nani ndani ya halmashauri? Je Lissu ana kurangapi ndani ya baraza la madiwani?
Au ndio kiwete ndani ya kundil la vipofu.
 
Ndugu zangu,​
Nimesoma habari hiyo hapa chini. Imenikanganya, maana, siioni mantiki katika hoja ya Tundu Lissu kukataza michango ya maendeleo jimboni kwake. Tafsiri yangu; katika maelezo yake naona vitu viwili; michango na matumizi ya michango. Kwa mtazamo wangu, kuwepo kwa sheria au kusiwepo na sheria, bado umuhimu wa wananchi kuhimizwa au kuhimizana kutoa michango kwa maendeleo yao unabaki pale pale, mahali popote pale. Michango hiyo yaweza kuwa ha hali na mali. Kilichopaswa kujadiliwa ni matumizi ya michango hiyo. Na hapa Ole Sendeka ametoa rai ya busara kabisa. Kuwa madiwani wakae na diwani mwenzao Tundu Lissu. Wajadiliane na wafikie muafaka. Na muafaka hauwezi kuwa wananchi wasichangie michango ya maendeleo yao bali namna watakavyochanga na usimamizi wa matumizi ya michango hiyo. Sijui wengine mna mtazamo gani?
Maggid​

Soma yenyewe..
Habari hii na Nathaniel Limu

MBUNGE wa jimbo la jimbo la Singida mashariki-Chadema ,Mheshimiwa Tundu Lissu,ameendelea kuwasha moto baada ya kuagiza tena,kwamba hakuna michango ya aina yo yote itakayochangwa jimboni kwake na kiongozi au mtendaji atakayethubutu kuchangisha, kitakachompata,asije akalaumu mtu.​

Moto huo ameukoleza tena mwishoni mwa wiki hii wakati akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini.Akionekana kujiamini ,Tundu alisimama na kusema“Mwenyekiti,naomba nirudie tena na tena,kwamba wananchi wa jimbo langu hawatachangia mchango wo wote na atakayethubutu kuchangisha,atakiona cha moto”.​

Akifafanua zaidi, amesema sababu kuu ya kutoa katazo hilo, ni kwamba hakuna po pote iwe kijijini,kata,halmashauri ya wilaya au hata serikali kuu yenyewe kunakoainisha sheria ya kumlazimisha mwananchi kutoa michango ukiwemo wa maendeleo.​

Wakati akiendele kutoa ufafanuzi wake huo,madiwani na hasa wa CCM ambao wako 263 dhidi ya sita wa CHADEMA,zaidi ya robo tatu mikono yao ilikuwa juu ikiomba nafasi ya kujibu mapigo huku baadhi wakitamka “mwenyekiti kwa taarifa”.​

Waliochangia kukosoa sera ya Tundu Lissu ya kupiga wananchi kuchangishwa michango,ni pamoja na diwani wa CCM kata ya Dung’unyi jimbo la Singida mashariki,Buno Natalis.Alianza kwa kusema “mwenyekiti,huyu diwani mwenzangu Tundu Lissu, ni mwongo,jimbo la Singida mashariki sio lake,ni letu sote madiwani tulioko madarakani hadi 2015″.​

Amesema Tundu hawatembelei wananchi ipasavyo kujua matatizo na kero zinazowakabili,kazi zote huwaachia madiwani wa kata ambao hana ushirikiano nao wa kukidhi haja.Natalias alisema Tundu amechafua hali ya hewa jimboni, kwani hata michango ya asilimia tano inayotakiwa na benki ya dunia ili wananchi waweze kuchimbiwa visima,wananchi wamegoma hawachangii.​

Wanaoumia ni wananchi lakini mheshimiwa Tundu, yeye anaendelea kunywa maji safi na salama ya ndani ya chupa.​

“Mpango wa Chakula Duniani (WPF) unaosaidia chakula kwenye shule zetu za msingi, wananchi wamepewa jukumu la kuchangia vitu vichache ili wanafunzi wapate chakula cha mchana bila matatizo,huko nako Tundu kawakataza wasichangie”,alisema Natalias kwa masikitiko makubwa.​
Naye diwani wa kata mpya ya Msange,Elia Digha, alimwomba Tundu kufuta kauli yake hiyo kwa madai kwamba imejaa vitisho na kama hafuti,basi misaada yote yenye masharti ya kutaka wananchi nao wachangie sehemu ndogo,ihamishwe na kupelekwa mahali wananchi wako tayari kuchangia.​

Mbunge wa jimbo la Kiteto mkoani Arusha,Christopher Ole Sedeka,ambaye alikuwa amefuatana na naibu waziri wa viwanda na masoko na ambaye ni mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu,alimwomba Tundu atafakari upya uamuzi wake huo wa kukataza mwananchi kuchangia maendeleo yao.​

Sedeka aliliomba baraza hilo la madiwani,kuangalia uwezekano wa kuchagua baadhi ya madiwani ambao watakaa na Tundu Lissu wamwelimisha juu ya umuhimu wa wananchi kuchangia maendeleo yao.​

“Ndugu zangu na majirani zangu,mahali kuna mafarakano,hapo tena maendeleo ya kweli yanakuwa ndoto,hakikisheni mnaondoa doa hilo,kaeni na Tundu ili mweze kufikia muafaka utakaowanufaisha wananchi wa halmashauri yote ya wilaya ya Singida vijijini”alisema mbunge huyo na kushangiliwa kwa nguvu na madiwani.​

Baada ya mapigo hayo, Tundu alipewa nafasi ya kujibu na aliposimama alisema “Mimi sio kichaa, na hakuna mahali po pote palipoandikwa kwamba niliwahi kuugua kichaa,kwa hiyo ninayoyasema nimeyafanyia uchunguzi wa kina na kubaini kuwa michango yote inayochangishwa jimboni kwangu,haipo kisheria”.​

Amesema mbaya zaidi ni kwamba tangu michango ianzwe kuchangishwa,hakuna hata mwaka moja wachangiaji wamesomewa mapato na matumizi.​

“Nina ushahidi wa kimaandishi,kwamba katika kata ya Kinyeto,michango ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata,iliwahi kutumiwa kuchangia harusi ya mbunge Lazaro Nyalandu, na zingine walipewa wajumbe wa CCM kwa matumizi ya nauli ya kwenda kuhudhuria kikao Singida mjini.​
Wakati mbunge Tundu Lissu,akiwakataza wananchi wake kuchangia maendeleo yao,tayari mwanachama moja wa CHADEMA jimboni kwake, hivi sasa anatumikia jela miezi sita kwa kosa la kuvunja geti linalotumiwa na halmashauri hiyo, kudhibiti ushuru wa mazao ya misitu.​

Pia Diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa na baadhi ya wananchama wa chama hicho,wanakabiliwa na kesi mahakamani kwa tuhuma ya kuvunja ‘geti’ la kudhiti ukwepaji wa ushuru wa mazao ya misitu, na kumpiga vibaya mlinzi wa geti hilo.Kesi hiyo iliyopo mbele ya mahakama ya mkoa,inasimamiwa na Tundu Li
 
Back
Top Bottom