Tundu Lissu kuitwa kwenye Kamati ya maadili ya madiwani Singida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu kuitwa kwenye Kamati ya maadili ya madiwani Singida

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jul 17, 2011.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni kwa sababu ya kuzuia michango ya maendeleo hadi taarifa za michango hiyo zitolewe! Baadhi ya Madiwani wamemwagiza Tundu Lissu atoe michango hiyo toka mfukoni mwake kama hataki watu wachangie, lakini Diwani mmoja amedai kwamba anajua kwamba Lissu ni mwanasheria lakini matendo yake hayafanani na taaluma yake! Hata hivyo Tundu Lissu ameshikilia msimamo wake wa kuzuia wananchi kuchangisha michango! Kwa hiyo imeamuliwa afikishwe kwenye Kamati ya Maadili ya Madiwani ili kumjadili! Source: Habari, Star Tv. My take: Kamanda Lissu kubali tu yaishe, Jimboni kwako hali si shwari kuhusu wewe! Ni ushauri usiohitaji malipo yoyote!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakuu mna maoni gani hapa?
   
 3. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kama habari hii ni kweli!!!
  Hivi kwa nini maamuzi ya wananchi yategemee mtu?
  Tuache kuwafanya watu watumwa wa mawazo ya viongozi, waacheni waamue wanavyotaka.
  Siasa ziwe na mipaka.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo unafikiri wananchi wanaweza kujiendesha wenyewe bila viongozi?
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Achange si mbaya

  atarudisha heshima kubwa sana kuliko msomi feki
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wananchi hao hawalipi kodi, yaani kuitwa na madiwani wa ccm wasiojua sheria kama lisu ndio unaona kuna jambo singida, kumbuka singida kwa lisu halmashauri inaongozwa na ccm haya yanategemewa huoni kama ni magamba tu haya. Yaani maendeleo yaletwe kwa michango huoni kama haelewani na ccm na si wananchi? Unapocukua take try to be more critical ndio maana hoja hii inaonekana hovyo
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijakuelewa, unamaanisha Tundu Lissu achange michango peke yake badala ya wananchi?
   
 8. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa nini watu hawataki kukubali pia hoja za Lissu. Jamani lini na wapi serikali imewahi kutoa taarifa za michango hiyo ya mbuzi, kuku, ngombe, shilingi elfu kumi cjui na vitu gani vingine nje ya utaratibu? Hoja za Lissu zijibiwe kwa hoja. Ni kweli wananchi wamezoeshwa kuonewa sasa ndo waendelee kuonewa tu? Kwa mfano amekuwa akisema kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya madawati, kujenga madarasa na masuala mengine ya maendeleo na zipo katika taarifa za PM akisoma bungeni. Yaani iwapo fedha hizo zingetumika wananchi ama wasingechangiswa ama wangechangishwa kiasi kigogo wanachomudu wala wasingekimbizana na mgambo na kufanyiwa kila aina ya unyama huko vijijini.

  Lakini fedha hizo hazionekani, kwa sababu hiyo miradi haikufanyika. Sasa mawili, ama serikali inadananya kuwa imepeleka fedha wakati haijapeleka (tena anasema PM bungeni) au fedha zimepelekwa halafu zimeliwa! Mbona hakuna majibu ya hoja hizi. Lakini pia kwa nini fedha hizo za michango zisiwekwe katika utaratibu wa kukaguliwa na CAG, Serikali inaogopa nini kujibu hoja hizi. Hata ninyi watetezi wa hoja za madiwani hao na serikali ya kinyonyaji ya Singida. Hiyo michango iko kwa mujibu wa sheria ipi, maana Lissu amekuwa akitumia sheria kuipinga.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hoja hii ni ovyo kivipi wakati nchi nzima michango inachangwa, kwa nini Singida Mashariki pekee ndio michango isiwepo?
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa uelewa wangu ni hivi: Serikali kuu imekuwa inatoa hela za miradi ya maendeleo kwa local government. Lakini kwa sababu wanazozijua wao wenyewe unakuta baadhi ya Halmashauri za local government hawazitumii hela zote na mara baada ya mwaka wa fedha (Financial Year) kupita inaelezwa kuwa wanarudisha/wamerudisha kwa serikali kuu. Sasa swali kubwa hela hizi ni kweli zinarudi serikali kuu? au kuna kupoteza 'muda' then duara inachezwa? Kwa nini warudhishe hela halafu wawambie wananchi wachange? Wananchi wanachanga kwa sababu serikali haina fedha au mkakati wa kujazaia huu 'mduara'?

  Mh. Lissu aliwaambia wananchi wasichange mara baada ya kugundua kuna hela zimerudishwa 'serikali kuu' bila maelezo ya kina! Sasa kama kamati ya maadili inamuita inabidi kamati hiyo iwe na maelezo kwa nini Halmashauri inaacha kutumia hela walizopewa na Serikali (ambazo by the way zimepitishwa na bunge) na badala yake wanawachangia wananchi maskini wanaoomba chakula? Kuna madudu sana kwenye serikali za mitaa na ndio maana wakampa uenyekiti Lyatonga Mrema ili watu 'wasiimbuke'.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo kuu ni kwamba Wananchi walio wengi, kulingana na utafiti wangu hawakubaliani na vitendo vya Lissu vya kukodi vijana wa kihuni ili kuwapiga wakusanya michango! Madarasa mbalimbali ya Shule za Msingi na Sekondari ujenzi wake mpaka sasa umesimama kwa sababu ya vitisho ya Lissu na vijana wake!
   
 12. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kumbe jambo likifanywa na watu wengi ndio linakuwa sahihi?
   
 13. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makosa ya mwanhuzi, bukene, mpanda, songea na kwongineko hayatakasishi kosakuwa sawa. Kama unaonewa utaonewa mpaka lini, sasa lisi kwa kutumia sheria amewakataza wananchi kulipishwa michango zinazokuja kuwa mbwembwe za wanasiasa ana kosa gani. Kwako kama kuonewa sawa usilazimishe wasioonewa waonewe pia. Soma sheria anayosimami lisu uelewe maana wanayochangishwa yako ktk budget ya waziri mkuu
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Watu wenyewe wa singida wanakufa kwa njaa,wachangie nini?pesa za stimulus package wamekula watu wachache leo mnachangisha mlalahoi!KWA SASA HATA KODI TUNAZOLIPA TRA HAZINA FAIDA KWETU SILIPI TENA!
   
 15. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Safi sana mkuu hapa atakayebisha kuhusu hii komendi huna haja ya kumjibu au kubishana naye nilitaka kuchangia lakini niliposoma hii comment sikuona umuhimu wa kuchangia tena maana kila kitu kinajieleza wazi ila ni ukiritimba tu wa hawa tunaowaita viongozi wetu hasa hawa magamba, mi sijui wanaroho gani jamani hawa watu!
   
 16. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  tanzania kuna mambo ya ajabu sana.

  -
  nakumbuka tundu lisu aluiza swali bungenu kuhusu hiyo michango na nikiasi gani kimechangwa na kama zinakaguliwa. Majibu ya waziri wa tawala na serikali za mitaa yalikua haya.
  1. Serikali ya wilaya haina takwimu za kiasi gani kimechangwa na wananchi

  2. Michango mingine waga ni interm of kuku, bata, ngo'ombe na mbuzi so kujua zinasamani gani ni vigumu.

  3. Hayo mahesabu hayakaguliwi na mtu yoyote yule.

  so kwa nini wanachi waendelee kuchangia wakati hela zianaliwa na wajanja?
  Je wananchi hawalipi kodi? Hizo hela zinaenda wapi?

  je ni lini vingozi wakitaifa walitoa hela zao mfukono kuchangia maendeleo?

  Mimi nilikuwa kenya, jamani kule hakuna wananchi kuchangia hata sent tano, na huduma zakijamii ni bora kuliko tz.
  kenya wananchi hawachangi kwa sababu huwa wanachangia kupitia kodi zao

  hii mambo ya wananchi kuchangiswa hela za maendeleo na wakati wanalipa kodi si haki kabisa, imegine wizara kutengewa bilioni nzima kwa ajili ya chai ni haki?

  Riport ya cag inasema robo ya bajeti ya serikali huliwa sasa utawaambiaje wananchi wachangie?

  Watanzania tumekuwa mbumbumbu sana na haya mambo yatatughalimu sana, sisi tuchange viongozi wakatumie na familia zao.
   
 17. M

  Mfinyanzi Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio Michango tatizo tunachangia nn?TUNACHANGIA KITU KILICHO KWENYE BUDGET?
   
 18. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  acha unge.mse. Nge mkuu, tuwekee hapa janvini riport ya utafiti wako huo, wananchi wananjaa watachangia vipi? Hizo za posho za vikao zingejenga shule ngapi huko singida?
   
 19. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama hakuna takwimu zinazo onyesha wananchi wamechanga kiasi gani na zimetumika vipi, namuunga mkono Tundu Lissu kwa 100% mpaka kila kitu kiwe wazi kwa wachangiaji!
   
 20. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,657
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Unapotosha mada.umebadili lalamiko lako la awali la Mh. Lissu kuzuia wananchi kuchangia pesa kisheria, then hapa umegeuka na kusema anatumia vijana kufanya vurugu kwa wakusanya michango hiyo. Acha ushabiki usio na mashiko! Tetea ulichosema awali.
   
Loading...