Nyangomboli
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 3,501
- 1,955
watanzania tunasahau mapema au hatutaki kufikiri. Mzazi au Baba nyumbani kuchangisha watoto si dalili za kushindwa kuwa Baba ambaye ni responsible jamani? Pia, watanzania hulipa kodi mbalimbali, zinatumikaje? Kazi ya kodi ni kuleta maendeleo, za kwetu huenda wapi? Madawati, madawa, madarasa na vinginevyo ni jukumu la serikali na si watu kuchangishwa. Lissu yuko sahihi. Hawa watu wanatuchezea akili sana. Kodi ni nyingi twalipa then wanaishia kuzichakachua. Jaribu kufikiria halmashauri inapopewa kwa mfano milioni mia saba mwezi wa sita na ndo mwezi wa mwisho kumaliza mwaka wa fedha, inazitumiaje? Ni kwamba zinarudi hazina na kutafutiwa pa kuzitolea ili ziliwe. Tanzania mfumo wa uongozi umechoka sana. Wapo wachache sana but hawana nguvu ya kubadili chochote.