Tundu Lissu: Kama msimamo wa Rais Samia ndio huu, tujiandae kwa mapambano makali na magumu mbeleni

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
"Kama msimamo wa Samia Suluhu Hassan ndio huu aliousema juzi, maana yake ni kwamba tujiandae kwa mapambano makali na magumu mbeleni. Huyu mama ni Magufuli wa kike, kwa hii kauli yake kuhusiana na haki za vyama vya siasa na katiba mpya ni anataka kuendeleza Umagufuli bila Magufuli mwenyewe kuwepo, anataka kuendeleza Magufulism without magufuli. Tujiandae na mapambano makali na magumu mbeleni"- Tundu Antipas Lissu


Pia soma > Lissu: Samia Suluhu Hassan has finally revealed her true colors
 
Tanzania hii tukitaka tusonge mbele kiuchumi na kidemokrasia dawa ni kuiondoshea mbali ccm. Ikishindikana kwenye ballot box basi hata kaa mtutu.
Watawala ndio hayo wanayoyataka, kila muda unavyokwenda raia wanakosa kabisa utu na uvumilivu, uoga umeshawaondoka.

In time, tanzanians will be farmers by day, soldiers by night.
 
Tanzania hii tukitaka tusonge mbele kiuchumi na kidemokrasia dawa ni kuiondoshea mbali ccm. Ikishindikana kwenye ballot box basi hata kaa mtutu.
CCM haiwezi kuondoka madarakani bila ya watu kuchinjana..that's for sure..yaani ni lazima watu wakichafue mbaya mbovu.

Shida ni kuwa upinzani nao umepoteza dira..upoupo tu,wanadandia hili wanaliacha wanaenda na lingine bila lolote kukamilika.

Mfano,ishu ya wale wabunge 18 inatosha kuonyesha ni kwa kiasi gani wapinzani wanafeli.
 
Huu ni ujinga tuu , mtu yupo mile 7500 away anawahutubia watu na wao bila kufkri wanapiga makofi , what a nonsense , si arudi tukichafue pamoja , kama anahofia maisha yake vip hawa waliopo wao hawapaswi kuhofia maisha Yao? Hata hvyo ni mda sasa wa kuifanya Tanzania iwe nchi tano
 
Ama kweli mama ana kazi kubwa mbele yake. Kwa upande mmoja dizaini za akina Lissu hawafahamu lolote zaidi kustawi kwa njia ya kupiga domo na kupinga lolote lililo mbele yao.

Watu wa aina hii uwe wao usiwe wao watakupinga tu. Kwa upande mwingine mama ashatuudhi sisi ambao mwanzoni tulikuwa upande wake -- kwa kujifanya kwenda kinyume na falsafa ya JPM kiuchumi na kitabia (mfano, ndani ya miezi mitatu kujiamini na kuthubutu kote kama taifa tulikokajenga chini ya JPM kamepukutika hivi hivi).

Mama, sasa jitetee mwenyewe!
 
Daaa mama samia Kazi anayo tena ..!

Kama unahasira za haraka ,unaweza kuchukua chuma na kuwapeleka mbinguni bowe na Lissu ..

Hizo kauli ni za dharau ,mimi tu binadamu wa kawaida sina madaraka ukinambia hivo lazima nikuwashie moto ..

Sijui mama Samia huko anajisikiaje kuambiwa "magufuli wa kike"
 
Aiseee hivi kwanini viongozi wa chadema wanakuwa hawana shukrani? Hivi kweli hawa watu wameshindwa kuwa na staha hata kidogo kwa Rais Samia? wanashindwa kuvumilia? kwanini hawana adabu hawa?
 
Huyu bwana siku hizi anajiona Yuko juu Sana,amekuwa msemaji na mtoa kauli za ajabu ajabu ,sishangai maana anafaili pale mirembe.

Lakini wafuasi wake wajiulize Mapambano gani huyu lisu anasema ikiwa wakati wa uchaguzi alituahidi kuwa asipokuwa rais nchi hii haitakalika na kinyume chake yeye ndo hakuikalia nchi mpaka leo Yuko kwa mabwana zake ,wafuasi wake mpuuzeni huyu Jonas savimbi.

Hivi huyu aliyesalitiwa na watanzania wa enzi za Magufuli anaamini kabisa watanzania wa Samia watamuunga mkono.?

Kama anataka Mapambano aje kwa motherland apambane nasio kutoa kauli za kijinga akidhani kuwa watanzania ni wapuuzi Kama alivyo yeye.
 
Ama kweli mama ana kazi kubwa mbele yake. Kwa upande mmoja dizaini za akina Lissu hawafahamu lolote zaidi kustawi kwa njia ya kupiga domo na kupinga lolote lililo mbele yao. Watu wa aina hii uwe wao usiwe wao watakupinga tu. Kwa upande mwingine mama ashatuudhi sisi ambao mwanzoni tulikuwa upande wake -- kwa kujifanya kwenda kinyume na falsafa ya JPM kiuchumi na kitabia (mfano, ndani ya miezi mitatu kujiamini na kuthubutu kote kama taifa tulikokajenga chini ya JPM kamepukutika hivi hivi).

Mama, sasa jitetee mwenyewe!
Rais hahitaji kutetewa na watu wa Aina yako ,katetee familia yako japo leo upate kula ugari na dagaa sio kila siku ugali tembele
 
..kama ni uongo basi Rais Samia Suluhu atuonyeshe kwa VITENDO.

1. Aivunje tume ya uchaguzi na kuanza mchakato wa kuunda tume mpya na huru.

2. Sheria ya vyama vya siasa iandikwe upya ili itoe haki sawa kwa vyama vyote.

3. Vyama vya siasa viruhusiwe kufanya shughuli zao bila kuingiliwa na kubugudhiwa na dola.

..Rais Samia akirekebisha hayo basi atakuwa amethibitisha kwamba yeye siyo " magufuli wa kike. "
 
E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Back
Top Bottom